Thursday, February 25, 2016

JE, MASHAHIDI WA YEHOVA NI WAKRISTO?

Ndugu msomaji,
Swali la kwanza la kujiuliza hapa ni hili, Je, Mashahidi wa Yehova wanaamini nini?
Tukianza kuutafakari kwa karibu sana msimamo wa kanuni yao kwa masomo ya IMANI YA KIKRISTO kama, Mwili wa Kristo, Wokovu, Utatu wa Mungu, Roho Mtakatifu na upatanisho wa Mungu na mwanadamu yaonyesha bila shauku yoyote kuwa hawashikilii kanunu ya msimamo wa Kikristo katika masomo haya.
Utadungua kuwa:
1. Mashahidi wa Yehova wanaamini kuwa Yesu ndiye Mikaeli malaika mkuu, kiumbe kikuu. Hii inahitilafiana maandiko mengi ambayo wazi yamtaja Yesu kuwa Mungu (Yohana 1:1,14, 8:58, 10:30).
2. Mashahidi wa Yehova wanaamini kuwa wokovu unapatikana kwa ushirika wa imani, matendo mazuri na itiivu. Hii inahitilafiana maandiko mengi yasiyo hesabika ambayo yasema wokovu unapatikana kwa neema kupitia kwa imani (Yohana 3:16; Waefeso 2:8-9; Tito 3:5).
3. Mashahidi wa Yehova wanakataa utatu wa Mungu, wakiamini kuwa Yesu ni kiumbe na Roho Mtakatifu kuwa ni nguvu za Mungu zizokuwa na uhai (active force/energy).
4. Mashahidi wa Yehova wanakataa dhana ya Kristo kuwa thabihu kwa niaba yetu na badala yake wanashikilia kuwa nadharia ya ukombozi, kuwa kifo cha Yesu fidia ya dhambi ya Adamu.
5. Wanakana kwamba Mungu alifanyika mwili (incarnation) ...kinyume na Yohana 1:14;1Timotheo 3:16
6. Wanakana Kifo mbadala cha Kristo kwa ondoleo la dhambi(substitutionary atonement)..kinyume na aya hizi Mathayo 20:28; Marko 10:45.
7. Wanakana fundisho la Utatu Mtakatifu...kinyume na Yohana 1:1-3; 1 Yohana 5:8
8. .Wanakana Uungu wa Yesu na wanafundisha Yesu ni kiumbe si Muumbaji...kinyume na ya hizi Isaya 9:6; Tito 2:13; Wakolosai 1:16-17; Yohana 1:1-3
9. Wanaamini kuwa wanakazi moja ya kubadili aya zote za Biblia ili ziendane na kile wanachodai kuvuviwa!!! Hii ni kinyume na Wagalatia 1:6-9; Ufunuo 22:18,19.
10. Wameunda bodi yao inayofasiri maandiko na mfuasi wao yeyote hatakiwi kupambanua jambo kinyume na tafsiri hizo!! Bodi hiyo inaitwa Watchtower Bible and Tract Society....na Biblia yao inaitwa New world Translation; ama Le monde neauval Tradiction en Francois. Yaani wana injili yao na Biblia yao, Mungu wao!!
11. Wanakana "Umasihi" 'Ukristo" wa Yesu....kwa hiyo hawa ndo wapinga Kristo hasa.1 Yohana 4:3 kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu.Hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.
12. 1 Yohana 2:22-23 Ni nani aliye mwongo ila yeye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo,yeye amkanaye Baba na Mwana.Kila amkanaye Mwana hana Baba; amkiriye Mwana ana Baba.
Ndugu msomaji,
Inawezekana vipi kwa mtu kujiita Mikristo bila ya Roho Mtakatifu ambaye ni Mungu na anaye ukamilisha Ukristo ndani yetu -sustaining?
Inawezekana vipi mtu au watu kujiita Wakristo bila ya Yesu ambaye ndie Mungu katika Mwili na ndie KRISTO Mwenyewe?
Biblia inasema:
Kwanza: Biblia inatufundisha kuwa Mpinga Kristo ni yule ANAYEKATAA KUWA YESU KRISTO HAJAJA KATIKA MWILI…YANI SIYE MWANA WA MUNGU, Soma (2 Yohana 1:7) na hapa tunawaona Mashahidi wa Yehova wanafauli kuingia katika hili kundi, sasa je, ni nani ni Mpinga Kristo kama si wewe unaye sema kuwa eti, Yesu ni Malaika Gabrieli?
Pili: Mtu yeyote ambaye hamwamini Bwana Yesu ya kuwa ni Bwana na Mwokozi wa maisha yake huyo tayari ni mpinga Kristo kwa sababu hana ushirika nayeye na wala hamuabudu yeye kabisa. Aliye hivyo huyo anaitwa Mpinga Kristo na ule mwisho Yesu akija kuhukumu ulimwengu hatawachukua hao wasiyo mwabudu yeye, na Nabii huyo Yesu wa Nazareti. Nabii huyu watu wanamjua ni nabii wa Mungu na ndiye atakayekuja kuhukumu ulimwengu siku ile ya kiama. Sasa kama hapa tu sasa hivi unampinga, je jiulize swali nayeye atakukubali uende naye uzimani alipo yeye? Jibu hatakuchukua na ameniambia niuambie ulimwengu wote atakaye sikia na asikie atakayekataa shauri lake. Wote wasiomwabudu yeye 100% ni wapingaji wa kumpinga Yesu Kristo na hao ni wapinga Kristo.
Namaliza kwa kusema kuwa, Mashahid wa Yehova sio Wakristo bali wanampinga Kristo kama ilivyo semwa katika 2 Yohana 1:7. Kwa maana wadanganyifu wengi wametokea duniani, wasiokiri ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na mpinga Kristo.
Ni maombi yangu Mungu ayafungue macho ya Mashahidi wa Yehova kwa ukweli wa injili na mafundisho ya kweli ya neno la Mungu.
Mungu awabariki sana.
Ni mimi Max Shimba, mtumwa wa Yesu Kristo,
For Max Shimba Ministries Org,
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2016. ALL RIGHTS RESERVED
Everyone is permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but changing it is not allowed.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW