Ndugu msomaji,
Tunaendela na hadith za msemakweli za Muhammad. Katika hadithi ya leo, tutajifunza kuhusu silaha anazo tumia Allah anapo pigana na mashetani.
Nyota Zinapaswa Kuyapiga Mashetani?
"Uumbaji wa nyota ulikuwa na malengo matatu, yaani kuwa mapambo ya mawingu, kupiga mashetani, na ishara za kuongozea wasafiri. Kwa hiyo, mtu yoyote anapojaribu kutafuta tafsiri tofauti, amekosea na anapoteza nguvu zake..." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 (Mwanzo wa Uumbaji) sura ya 3 maelezo ya mwenye kutafsiri kabla ya na. 421 uk.282.
Hebu tujifunze kwanza maana ya Nyota:
Kwa kutumia darubini na vifaa vya kisasayansi imegunduliwa ya kwamba ni magimba makubwa sana katika anga la nje yanayong'aa kwa sababu yanatoa mwanga, joto na aina mbalimbali za mnururisho kutokana na myeyungano ya kinyukilia ndani yao. Lakini ziko mbali sana na kwa hiyo tunaziona kama nukta ndogo za nuru. Kwa jumla nyota zinaonekana kwenye anga kwa mpangilio usiobadilika na kila nyota huwa na mahali pake pasipobadilika kati ya nyota nyingine hata kama nyota kwa jumla zinazunguka angani juu yetu kila siku.

Baada ya kusoma maana ya Nyota, mtu anaweza jiuliza, kivipi Allah anapigana na Mashetani kwa kutumia Nyota?
Mbona Allah hajawai tuletea aya ambayo inasema jinsi alivyo pigana na Mashetani kwa kutumia Nyota?
Ni vita zipi ambazo Allah anatumia Nyota kupigana na Mashetani?
Kama Allah ni AKBAR kama wanavyo dai, Waislam, kwanini anshindwa kutumia nguvu yake kuyapiga mshetani mpaka atumie Nyota?
JIFUNZE ZAIDI KUHUS NYOTA:
Fizikia na astronomia zimegundua ya kwamba nyota hazidumu milele bali zina mwanzo na pia mwisho. Kutokana na tabia hii wataalamu mara nyingi huongea juu ya "maisha", "kuzaliwa" na "kufa" kwa nyota ingawa si viumbehai.

Nyota zinaanzishwa katika nebula au katika mawingu makubwa ya gesi kwenye anga la ulimwengu. Kama wingu ambalo sehemu kuwa yake ni hidrojeni ni kubwa sana inaanza kujikaza kutokana na graviti yake. Katika muda wa miaka mioni 10-15 wingu linajikaza kuwa tufe kadhaa kubwa na ndani ya tufe hizi halijoto inazidi kupanda. Kadiri jinsi gesi inajikaza nguvu ya graviti ndani yake inaongezeka na atomi zake zinaanza kugusana. Halijoto inazidi hadi kufikia kiwango ambako mmenyuko mfululizo wa kinyuklia unaanza kutokea hadi kufikia mmeyungano nyuklia wa hidrojeni kugeukia heli.
Kipindi cha mmeyungano nyuklia wa hidrojeni kinaendelea kwa miaka mabilioni hadi sehemu kubwa ya hidrojeni imekwisha. Hapa sehemu za nje ya nyota hupoa na kupanuka; halii hii huitwa pandikizi nyekundu (red giant) kwa sababu ya ukubwa na rangi yake. Mapandikizi mekundu kadhaa huonekana kwa macho tu angani yaking'aa kwa nuru nyekundu. Kama masi ya nyota bado ni kubwa mmeyungano nyuklia unaendelea kuzaa elementi nzito zaidi kwa sababu sehemu ya heli inaendelea kujibadilisha kuwa elementi za juu zaidi. Inaaminmiwa ya kwamba elementi zote ulimwenguni zilianzishwa ndani ya nyota.
Mwishowe kama masi haitoshi tena kuendeleza mmeyungano masi inaweza kujikaza; kutegemeana na ukubwa wa masi nyota inaweza kupasuka. Mabaki ya mlipuko huu yanakaa angani tu na mara nyingi huingia tena katika mwendo wa kuzaa nyota mpya; sehemu ndogo za masi hii huwa sayari.
Kama masi imejikaza sana shimo nyeusi (Kiing.: black hole) inatokea. Katika hali hii nguvu ya graviti ni kubwa mno inashika hata nuru yenyewe ambayo haiwezi kuoka nje tena.
Nategemea leo umesha gundua kuwa Allah hakuumba Nyota na wala Allah hazielewi Nyota.
Karibuni kwa Yesu Mungu Mkuu.
Mungu awabariki sana,
Max Shimba Ministries Org.
No comments:
Post a Comment