Wednesday, January 6, 2016

ALLAH ATEREMSHA AYA NA KUSEMA KUWA MASINAGOGI SIO MISIKITI

Ndugu msomaji,
Leo nataka nimalize NGEBE ZOTE za Waislam ambazo zinalazimisha kuwa eti Masinagogi ni Misikiti.

Katika Suratul Hajj aya ya 40 iliyo teremshwa na Allah huko Madina na kutafsiriwa na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani ( alie fanya tarjuma).
Andiko hili linataja majina ya majengo mbalimbali ya ibada ikiwemo na Sinagogi kwenye tafsiri ya Qur-an ya Kiswahili ya Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani.
Suratul Hajj 40. Wale ambao wametolewa majumbani mwao pasipo haki, ila kwa kuwa wanasema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingeli vunjwa nyumba za wat'awa, na Makanisa, na MASINAGOGI, na misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi. Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu. Maelezo
SASA MADA INAANZIA HAPA:
1. Kama kweli Masinagogi ni Misikiti ya Wayahahudi, kwanini Allah ameyatofautisha hayo majengo kimajina, "Masinagogi na Misikiti" kwenye hii aya?
2. Kama Masinagogi ni Misikiti ya Wayahudi, kwanini Allah asinge sema Nyumba za Watawala za Wayahudi ni Misikiti, LAKINI akaziita Masinagogi.
3. Je Sinagogi laweza kuwa ni Msikiti katika uasili wa lugha?
4. Ikiwa kuingia tu kwenye Sinagogi kulimaanisha Yesu ni Muislam, je Paulo naye kwa tendo hilo lakuingia humo alikuwa Muislam?
5. Je, Paulo kuingia kwenye Sinagogi alikuwa anaingia kwenye Misikiti?
6. Kama Masinagogi ni Misikiti, kwanini kwenye Masinagogi kuna viti na kwenye Misikiti hakuna viti?
7. Kama Masinagogi ni Misikiti, kwanini kwenye Masinagogi hakuna maji ya kutawadha kama kwenye Misikiti?
8. Kama Masinagogi ni Misikiti, kwanini Masinagogi hayaangalii Makka kama Misikiti?

9. Kumbe Misikiti ni Masinagogi ya Waislam.

10. Mwislam ni mtu wa ajabu sana, anakubali kuwa Masinagogi ni Misikiti ya Wayahudi lakini atakataa kuwa Misikiti ni Masinagogi ya Waislam.
Ndugu Waislam, tafadhali jibuni kwa aya. Hoja ujibiwa kwa hoja.
Max Shimba Ministries

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW