Friday, January 8, 2016

ALLAH ANAKIRI KATIKA QURAN KUWA BIBLIA YOTE NI MANENO YA MUNGU

KAMA KUNA MUISLAM ANABISHA, ANILETEE AYA KUTOKA QURAN INAYOSEMA KUWA BIBLIA SIO MANENO YA MUNGU.


Ndugu msomaji,

Bila ya kupoteza muda, tutaanza moja kwa moja kwa kusoma Surat Al Maida aya ya 46 iliyo teremka Madina. Na hii ni katika Sura zilizo shuka karibu na mwisho. Humu umebainishwa waajibu wa kutimiza maagano, sawa yakiwa baina ya mja na Mola wake Mlezi, au baina ya watu wenyewe kwa wenyewe.


ALLAH ANATEREMSHA AYA NA KUSEMA KUWA INJIL NI NURU NA INASADIKISHA TAURAT.
Surat Al Maida 46. Na tukawafuatishia hao Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake uwongofu, na NURU NA INAYO SADIKISHA yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachamungu.47. Na wahukumu Watu wa Injili kwa yale aliyo teremsha Mwenyezi Mungu ndani yake. Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio wapotofu. Maelezo

Katika aya hapo juu, tunajifunza kuwa Injili ni NURU, na Biblia inasema kuwa YESU NI NURU YA ULIMWENGU. Allah anakiri kwa mdomo wake kuwa Injili ni Nuru na HAKUWAI SEMA KUWA Quran ni Nuru. ALLAH AMESHA ANZA KUKIRI KUWA BIBLIA NI NURU na haina shaka ndani yake.

KAMA KUNA MUISLAM ANABISHA, ANILETEE AYA KUTOKA QURAN INAYOSEMA KUWA BIBLIA SIO MANENO YA MUNGU.

Endelea kusoma


ALLAH ANATHIBITISHA KUWA BIBLIA HAINA SHAKA NA NI NENO LA MUNGU.
Surat Al Maida 48. Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hichi kinacho sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Vitabu na kuyalinda. Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia. Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka ange kufanyeni nyote umma mmoja, lakini ni kukujaribuni kwa aliyo kupeni. Basi shindaneni kwa mambo ya kheri. Kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo yenu nyote, na atakuja kuwaambieni yale mliyo kuwa mkikhitalifiana.

ALLAH katika Surat Al Maida aya ya 48 anaendelea kukiri kuwa KITABU-BIBLIA ni maneno ya Mungu na haina shaka ndani yake.


ALLAH ANAMWAMBIA MUHAMMAD katika Surat Yunus 94 KUWA, KAMA ANA SHAKA NAYE KUWA BIBLIA SIO MANENO YA MUNGU, BASI AWAULIZE WAKRISTO AMBAO WANASOMA "KITABU-BIBLIA".

HAPA ALLAH ANAHAKIKISHA NA KUTHIBITISHA KWA MUHAMMAD KUWA BIBLIA NI MANENO YA MUNGU.

Surat Yunus 94. Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu kabla yako. Kwa yakini imekwisha kujia Haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe miongoni mwa wenye shaka

Ndugu msomaji, unaona jinsi Allah anavyo KIRI KUWA BIBLIA NI MANENO YA MUNGU? Sasa kwanini Waislam wanabishana na Allah wao na Mtume wake kipenzi Muhammad kuwa Biblia sio maneo ya Mungu?

KAMA KUNA MUISLAM ANABISHA, ANILETEE AYA KUTOKA QURAN INAYOSEMA KUWA BIBLIA SIO MANENO YA MUNGU.


MTUME MUHAMMAD SASA ANAKIRI KUWA BIBLIA NI MANENO YA MUNGU NA ANAIAMINI.
Surat Ash Shuura 15. Basi kwa haya waite! Nawe simama sawa sawa kama ulivyo amrishwa, wala usiyafuate matamanio yao. Na sema: NAAMINI ALIYO TEREMSHA MWENYEZI MUNGU KATIKA VITABU. Na nimeamrishwa nifanye uadilifu baina yenu. Mwenyezi Mungu ni Mola wetu Mlezi, na Mola wenu Mlezi. Sisi tuna jukumu kwa vitendo vyetu, na nyinyi mna jukumu kwa vitendo vyenu. Hapana kuhojiana baina yetu na nyinyi. Na Mwenyezi Mungu atatukusanya pamoja, na marejeo ni kwake

Mtume Muhammad sasa anasadiki katika Biblia iliyo kuwepo kabla ya Quran na ansema hivi, nukuu: NAAMINI ALIYO TEREMSHA MWENYEZI MUNGU KATIKA VITABU

MASWALI:
1. Sasa kama Muhammad anaiamini Biblia, wewe Muislam, ni nani aliye kuroga na kusema kuwa Biblia imetiwa Mkono na sio maneno ya Mungu?

2. Kama Biblia imetiwa mkono, basi, NILETEE NAKALA YA BIBLIA ambayo haikutiwa MKONO ILI NA MIMI NISADIKI KAMA MUHAMMAD?


ALLAH NA MUHAMMAD WANAKIRI KUWA INJIL NI UWONGOFU NA NI NURU NA INAYO SADIKISHA
Surat Al Maida 46. Na tukawafuatishia hao Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake uwongofu, na nuru na inayo sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachamngu.

Waislam wengi wanadai kuwa Injil iliyo ndani ya Biblia imetiwa Mkono, INGAWA AHAWANA aya kusaidia hayo maneno zaidi ya hadith dhaif dhaif ambazo sio maneno ya Allah.

SASA BASI, kama kweli Injili ilitiwa MKONO, naomba mnijibu maswali yafuatayo.

1. Nileteeni Injili ambayo haijatiwa mkono iliyo teremshwa kabla ya Quran. Kumbuka mimi sina muda na aya za Quran kwasababu Quran sio BIBLIA - Mkusanyiko wa vitabu. Ipo wapi Injili iliyo teremshwa kabla ya Quran na inayo thibitisha Taurat?

2. Nileteeni Taurat ambayo haijatiwa mkono iliyo teremshwa kabla ya Quran. Kumbuka mimi sina muda na aya za Quran kwasababu Quran sio BIBLIA - Mkusanyiko wa vitabu. Ipo wapi Taurat iliyo teremshwa kabla ya Quran na inayo thibitishwa na Injili?

3. Nileteeni Zaburi ambayo haijatiwa mkono iliyo teremshwa kabla ya Quran. Kumbuka mimi sina muda na aya za Quran kwasababu Quran sio BIBLIA - Mkusanyiko wa vitabu. Ipo wapi Zaburi iliyo teremshwa kabla ya Quran na inayo thibitishwa na Injili?

WAISLAM, MKISHINDWA KUNIONYESHA WAPI ZILIPO INJILI, ZABURI, NA TAURAT zilizo teremshwa kabla ya Quran, basi kushindwa kwenu ni jibu tosha kuwa BIBLIA NI MANENO YA MUNGU NA IMEKAMILKA NA UWONGOFU KWA WALIO ONGOKA.

KAMA KUNA MUISLAM ANABISHA, BASI ANILETEE AYA KUTOKA QURAN INAYOSEMA KUWA BIBLIA SIO MANENO YA MUNGU.

Leo tumejifunza kutoka Quran na Allah na Muhammad kuwa BIBLIA NI MANENO YA MUNGU.

Max Shimba Ministries

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW