Wednesday, December 9, 2015

JINSI YA KUENENDA KWA ROHO

Wagalatia 5:16 “Basi, nasema enendeni kwa Roho, wala hamtatimiza kamwe tamaa za mwili”Hapa tunaona Paulo anawaagiza wagalatia kwamba waenende kwa Roho na lengo kubwa ni ili wasizitimize tama za mwili.
Lengo la waraka huu mfupi ni kukueleza namna unavyoweza kuenenda kwa Roho, na hii ni kwa sababu Yesu mwenyewe alisema ni heri mimi niondokeili aje mwingine msaidizi huyo Roho wa kweli. Na 
kama tunaye Roho mtakatifu ni lazima tujue ni kwa namna gani tutaenenda kwa roho?Neno la Mungu/ Mungu anaposema, enendeni kwa Roho ana maana hii:-
(a) Kila unalolizungumza, lizungumze chini ya uongozi wa Roho mtakatifu. Yohana 12:49-50. Yesu mwenyewe hakunena neno lolote kwa shauri lake, bali kila ambalo baba alimwambia kupitia Roho mtakatifu. Hivyo hata wewe
kama unafundisha, unahubiri, unaonya hakikisha unachokisema Roho mtakatifu ndiye amekuruhusu ukiseme. Usiseme kitu cha kwako halafu ukasema Roho mtakatifu amekuongoza.
(b) Tii uongozi wake .Yohana 16:13 “ lakini atakapokuja huyo Roho wa kweli; atawaongoza awatie kwenye kweli yote…….” Moja ya kazi za Roho mtakatifu ni kutuongoza na kututia kwenye kweli yote. Hivyo kuenenda kwa Roho maana yake ni kutii katika yale anayotuambia maana hata yeye haneni kwa ridhaa yake isipokuwa yale anayoyasikia kutoka kwa Mungu.

(c) Jifunze kuyafikiri mambo ya Roho wa Mungu. Warumi 8:5b “
Bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho”Kuenenda kwa roho kunajumuisha kukaa chini na kuanza kutafakari mambo/kazi za Roho mtakatifu. Vile jinsi utendaji wake ulivyo, karama zake, vipawa, tunda la Roho na vile jinsi anavyofanyika msaidizi katika maisha yako.
(d) Kuliishi tunda la Roho.Wagalatia 5:22 “lakini tunda la Roho ni upendo, Furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi………”Sikiliza ukijifunza au kadri unavyoishi maisha yaliyojaa upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi ndivyo unavyokuwa umejiweka kwenye mkao wa kuongozwa na Roho au ndiko kunaitwa kuenenda kwa Roho.
(e) Kwa kuyakataa na kuyafisha/vunja matendo ya mwili katika maisha yako. Wagalatia 4:28-31 ule mstari wa 30 unasema” Lakini lasemaje andiko? Mfukuze mjakazi na mwanawe kwa maana mwana wa mjakazi hatarithi kabisa pamoja na mwana wa muungwana”Biblia inapozungumzia kumfukuza mjakazi pamoja na mwanawe ina maana ya kuyafukuza, kuyapinga, kuyaondoa, kuyafisha, kuyaharibu matendo ya mwili katika maisha yako ambayo yametajwa katika. Wagalatia 5:19-21 ikiwa ni pamoja na uasherati, ulevi, husuda, uadui, ugomvi, uchafu, ufisadi nk.Naamini baada ya ujumbe huu utaanza kuenenda kwa Roho na kuomba msaada wa Mungu katika maisha yako kwenye eneo hili..
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nawe.
Patrick akifundisha
Na; Patrick Samson Sanga

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW