Wednesday, July 1, 2015

Zul-Qarnain na Kutua kwa Jua katika Sura 18:85-86

Je, ni kweli kuwa jua linazama katika chemichemi za maji zenye tope au giza, au Koran ina makosa, au kuna maelezo mengine? Kwanza tutaangalia maana ya wazi Sura ya 18:85-86, na kisha tutaangalia maelezo na majibu ya baadhi ya Waislam kuhusu jambo hili.
Unajimu Kidogo
Inawezekana kuwa haijulikani kwa mapana kwamba watawala wa kislam wa Abbasid, Waarabu na Waajemi waliendelea sana katika unajimu, wakizipa majina nyota nyingi, hata walinukuru na kusahihisha baadhi ya orodha za hesabu za watawala wa Misri (Ptolemy’s tables). Hata hivyo jua ni kubwa mara nyingi zaidi ya dunia nzima, na dunia husafiri ikilizunguka jua. Jua halizami katika chemichemi za maji zenye tope.
Zul-Qarnain ni Nani?
Hatuna ushahidi kama Muhammad alimwambia mtu yeyote kuwa Zul-Qarnain alikuwa nani hasa. Waislam wana mitazamo minne tofauti.
  
Alexander Mkuu
 (wa Makedoni) ni mtazamo wa Waislam wengi zaidi. Zul-Qarnain humaanisha kuwa ni "mtu mwenye pembe mbili." Kuna hadithi ya kubuniwa isemayo kuwa Alexander Mkuu alikuwa mungu na alikuwa na pembe mbili za kondoo dume zilizokuwa zinakua pembeni mwa kichwa chake. Licha ya ukweli kwamba hii haikuwa kweli (na ni tatizo kupata kofia ya vita—helimeti inayoweza kutosha), hadithi hii ilijulikana, na waislam wengi hudhani kuwa Allah katika sura ya 18 Alexander alitajwa kwa jina hili, mungu.
  
Koreshi I Muajemi 
ni mtizamo mwingine. Ufalme wake hasa ulikuwa ufalme uliohusisha makundi mawili: Wamedi na Waajemi, lakini zaidi ya hayo hakuna uthibitisho kuwa pembe mbili zinamhusu yeye.
  
Mfalme wa Yemeni
 ambaye alivaa kofia ya vita yenye pembe mbili za kondoo dume, ni mtazamo walionao baadhi ya Waislam.
  
Mtu asiyejulikana 
ni mtizamo wa nne. Hata hivyo inaonekana si vema sana kutoa maelezo juu ya watu ambao msemaji hajawahi kuyasikia.
  
Hitimisho:
 Haijalishi kuwa Zul-Qarnain alikuwa nani hasa. Kama aligundua kuwa jua hutua kwenye chemichemi za maji zenye tope, na huwa halizami kwenye chemichemi za maji zenye tope, kwa hiyo huu ni ubatili, bila kujali mtu ambaye Muhammad alimzungumzia.
Sura 18 Mawazo na Majibu

 

Wazo la I: Jua huzama kwenye chemichemi za maji zenye tope!
Kwa Waislam wa awali, Koran iliwafundisha kuwa jambo hili linatokea hasa. Mwanahistoria wa kiislamu wa awali al-Tabari juzuu ya 1 uk.234 anaonesha hili. Kama mfano wa pili, "[Dhu al-Qarnaiyn] alishuhudia kuzama kwa jua katika sehemu yake ya kupumzika ndani ya bwawa jeusi na tope la kunuka." Kwa mujibu wa al-Tabari juzuu ya 5 uk.173-174. Dul Qarnain [Zul Qarnain] anapatikana pia kwenye al-Tabari juzuu ya 1 uk.371.
Jambo jingine linaloingiliana na hili, dunia hukaa juu ya samaki mkubwa kwa mujibu wa al-Tabari juzuu ya 1 uk.220 (839-923 K.K.).
Wazo la 2: Jua lilionekana kwa Alexander likitua katika ziwa la Ithaca Makedonia
 
Wazo hili hubashiri kuwa Zul-Qarnain alikuwa Alexander, na kwamba Alexander alikuwa Muislam mzuri. Wazo hili haliendani na ukweli kwamba Alexander alikuwa na hekalu lililotengenezwa kwa ajili yake. Pia Alexander alikwenda kuteka kaskazini na magharibi mwa Ithaca ambayo ni Albania ya sasa.
 
Kibaya zaidi katika wazo hili, Wayunani walifanya makazi mamia ya maili magharibi mwa Ithaca ambayo ni Hispania, Sicily, n.k. za asa, miaka mia tano kabla ya Alexander. Kitu gani kingemfanya Myunani mwenye akili sana afikiri kuwa jua lilizama katika ziwa la Makedonia wakati meli za kiyunani zilikuwa zinaenda mbali zaidi magharibi mwa nchi ya Alexander? Kwa nyongeza, Tertullian katika Hoja Juu ya Nafsi [A Treatise on the Soul] sura 49 uk.227 anasema kwamba Aristotle, aliyeishi wakati ule ule, anataja shujaa kutoka kisiwa cha Sardinia mbali magharibi mwa Makedoni lakini ni kama kwenye latitudi ile ile.
Wazo la 3: "Chemichemi ya maji yenye tope" ni Bahari ya Atlantic
Bahari ya Atlantic haina tope na si nyeusi, bali ni bluu-kijani. Pia si chemichemi bali ni bahari. Jua huwa halizami katika bahari. Cha muhimu zaidi, Alexander, Koreshi I wa Uajemi na wafalme wa Yemeni hawakuwahi kwenda kwenye Bahari ya Atlantic na Sura ya 18:85-86 inasema kuwa Zul Qarnain aliona au alishuhudia hili.
Sababu yoyote kati ya hizi nne inatosha kulindoa wazo hili, hivyo basi kwa Waislam wanapendekeze hili? Hiki ndicho kiwango ambacho wanajaribu kwenda ili kuonyesha kuwa Sura ya 18:1-2 sio potofu. Ikiwa Allah [Mungu] wa uislam alikuwa na wazo hili katika Koran, na Allah alijua kuwa hili ni wazo potofu, hivyo jambo hili litakuwa uongo. Kama Allah wa uislam hakujua ukweli huu, wasingelikuwa na ufahamu na hakika wasingekuwa na uwezo wa kujua kila kitu. Kama mistari hii isingetoka kwa Allah [Mungu] wa uislam, basi Koran ingekuwa na makosa dhahiri, kwa sababu inathibitisha upotofu huu kutoka kwa Allah wakati sivyo hivyo. Bila shaka, ikiwa kweli si Allah wa uislam, na Mungu wa kweli si mwandikishi wa Koran, basi Allah wa uislamu hakusema uongo kwa sababu hayupo.
Wazo la 4: "Chemichemi ya maji yenye tope" ni Koreshi I alikoangalia Bahari Nyeusi (Black Sea)
Hata kama Koreshi I alikwenda magharibi mwa ufuko wa mashariki mwa Bahari Nyeusi (Black Sea), na jua lingeonekana vipi likitua katika Bahari Nyeusi, ikiwa alikuwa ameshaupita ufuko wa mashariki kuelekea kusini na mashariki? Hatuna ushahidi kuwa Koreshi aliwahi kusafiri kwenda ukanda unaojumuisha Georgia, Amernia, Azerbaijan, n.k. za sasa, zilizo mashariki mwa Bahari Nyeusi. Muislam angekuwa na hoja yenye udhaifu kidogo kama angesema kuwa Koreshi aliliona jua likichomoza kutoka kwenye Bahari Nyeusi, kwa sababu alivuka hadi Uyunani, lakini Koran inaongelea kuzama kwa jua. Hata hivyo Bahari Nyeusi sio chemichemi, kila mtu kuanzia wamisri na wengineo kaskazini ya mbali, walijua kuwa jua halikuzama kwenye Bahari Nyeusi.
Wazo la 5: "Chemichemi ya maji yenye tope" ni Koreshi I alikoangalia Bahari ya Aegean

Lakini Waajemi walikuwa wakiwafahamu vema Waatene, Waspartani, (asili ya Wayunani), na Wayunani wengine. Waajemi wangelijua kuwa Wayunani hawakuwa upande mwingine wa jua.
Wazo la 6: Hakika "Chemichemi ya maji yenye tope" ni mfalme wa alikoangalia Bahari Nyekundu
Wayemeni (Wasaba/Waseba) wakati wote waliwafahamu Waabisinia (Waethiopia) ng’ambo ya mto. Ikiwa walifikiri kuwa jua lilizama katika Bahari Nyekundu (Red Sea) basi Waabisinia wangelikuwa watu waliokuwa upande mwingine jua lilikokuwa.
Wazo la 7: "Chemichemi ya maji yenye tope" ni usemi wa kufananisha na kitu kingine
Ikiwa kitu hiki hakikuwa halisi, bali ni kifananishi cha kitu au vitu vingine, basi Koran imeshindwa kuelezea kuwa hakikuwa kweli, na wazo hili lilikuwa la kupotosha. Zaidi ya yote, hakuna mtu anayeweza kusema kwa hakika kuwa kitu hiki kilifananishwa ni nini hasa.
 
Hakuna kitu chochote kwenye Koran kinachoonyesha kuwa kitu hiki si halisi, na Waislam wengi wa awali walikichukulia kuwa kitu halisi, yaani ukweli halisi. Kwa kuzingatia kuwa walijua maana hasa ya jambo hili kutoka kwa wafuasi wa Muhammad, kwa hiyo walipotoshwa na Sura ya 18. 
Wazo la 8: Muhammad alikuwa akisimulia juu ya ndoto yake
Wazo hili halimfahamu Zul-Qarnain kuwa ni nani hasa. Ikiwa Muhammad alikuwa anasimulia juu ya ndoto yake, jua lingeweza kutua popote alipotaka litue. Hata kama haifahamiki ni muhusika gani dhahania aonaye kitu kilicho potofu kabisa, na watu wanaoamini kuwa ni kitu cha kweli, atatufundishaje sisi juu ya kuiamini kweli.
Hata hivyo, ikiwa mtu atasema kuwa walimwona mtu fulani aitwaye ‘Ali akifanya kitu cha ajabu ajabu, na mamilioni ya watu wakamwamini kwa karne nyingi. Je, mtu huyo ataweza kuwa mwongo ikiwa alisahau kuwaambia watu kwamba, "ilikuwa ndoto yangu tu na sikumwona Ali akifanya hivyo kwa macho yangu."?
Hitimisho
Bila kujali kama Zul-Qarnain alikuwa Alexander Mkuu au mtu mwingine, Korani yaeleza jambo hili kama ukweli kuwa jua huzama katika chemichemi za maji yenye tope. Hata watu wa zamani miaka 1,000 kabla ya Muhammad walijua kuwa jua halikuzama upande huu wa Hispania. Wazo hili halikuwa kifananishi cha kitu kingine kwa sababu hakuna Muislam wa zamani aliyepatikana kuwa hakulichukua jambo hili kuwa halisi au kutoa maana yake kama usemi wa kufananisha na kitu kingine, na Waislam wote wa zamani waliamini kuwa Koran haikutolewa kwa ajili ya kudanganya.
Orodha ya Vitabu vya Tafsiri ya Korani
1. Arberry, Arthur J. The Koran Interpreted. Macmillian Publishing Co., Inc. 1955.
2. Dawood, N.J. The Koran. Penguin Books. 1956-1999.
3. Malik, Farooq-i-Azam. English Translation of the Meaning of AL-QUR’AN : The
Guidance for Mankind
. The Institute of Islamic Knowledge. 1997
4. Pickthall, Mohammed Marmaduke. The Meaning of the Glorious Koran. Dar al-
Islamiyya (Kuwait) (no date given)
5. Rodwell, J.M. The Koran. First Edition. Ivy Books, Published by Ballantine
Books. 1993.
6. Shakir, M.H. The Qur’an. Tahrike Tarsile Qur’an, Inc. 12th U.S. Edition 2001.
7. Sher Ali, Maulawi. The Holy Qur’an. Islam International Publications Limited
(Ahmadiyya) 1997
8. Yusuf ‘Ali, Abdullah. The Holy Qur-an : English translation of the meanings
and Commentary
. King Fahd Holy Qur-an Printing Complex. (Al Madina
Saudi Arabia) 1410 A.D.
Vitabu Vingine vya Rejea
Encyclopaedia Britannica. Encyclopaedia Britannica, Inc. 1958. 
The History of al-Tabari : An Annotated Translation
. Ehsan Yar-Shater, General Editor. State University of New York Press 1989-. 

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW