Wednesday, July 29, 2015

YESU YUPO NA ANAKUJUA HATA JINA LAKO

Yesu ni wa kweli, anajua jina lako na kila kitu kinacho kuhusu, pia anakupenda. Hayuko mbali nawe, yuko karibu nawe, anataka ujue kuwa yupo, anaishi, na anataka kukusaidia ikiwa utapenda. Na kama utapenda kumfahamu, unaweza kumfahamu. Ikiwa utahitaji msaada, atakusaidia, kama utaongea nae atakusilikiza, naye ataongea nawe pia.

Yesu ndiye aliyekufanya usome maandishi haya, kwa sababu ametuambia tukuandikie, na amehakikisha kuwa yamekufikia. Anajua kila kitu kinachokuhusu tangu mwanzo wa maisha yako hadi sasa hivi, amejumuika nawe katika huzuni, madhaifu na hata matatizo yako, atakusaidia mara tu utakapo muhitaji. Hakutaka uwe peke yako, mara nyingi ametaka umjue yeye. Ndiyo maana amekufanya kuwa rafiki kwa makusudi hayo. Mwamini yesu, kwani kwa Yesu urafiki ni mzuri tena wa kweli, isitoshe ni wa upendo ule wa ndani. Hatokuacha kamwe, unachotakiwa kufanya ni kumwamini na uongee nae yeye Yesu, naye atakujibu, atakusaidia, na ndipo utakapomfahamu Yesu. Anakutazama sasa unaposoma maandishi haya na amejaa upendo juu yako.

Imeandikwa kuwa, Yesu alikuja duniani, akafa, akatoa uhai wake kwa ajili yetu. Hii inaonyesha kuwa kifo kilikuwa ni cha lazima, ili kulipa deni la dhambi zetu. Kwa nini alichagua kulipa deni la dhambi kwa njia ya kifo? Ni kwa sababu anakupenda sana!

KAFARA: BABA KAMA MTOTO
Hakuna mtu mwingine katika historia ya dunia hii bali Yesu tu. Hakuwa mdhambi, dhambi ilikuwa kwa wengine. Dhambi zote zinakuja zenyewe kwa namna moja ama nyingine alionekana mnyenyekevu. Baba wa mbinguni alituumba ili tupendane sisi kwa sisi, na pia tumpemde yeye, lakini dhambi imekuwa kinyume na upendo huo na imechukua nafasi kubwa katika maisha yetu, hata kusababisha kifo. Hata hivyo, kifo ndio kimekuwa malipo makuu ya dhambi. Dhambi inatembea kutoka kwa mtu mmoja. Kwenda kwa mwingine, nchi moja kwenda nyingine, na inaleta maumivu kwa kila mtu, na ndiyo maana inawatenganisha wanadamu wote na Mungu, na inawapeleka kuzimu. Mungu hatokubali dhambi iingie Mbinguni, na mbingu ziwe kama dunia ilivyo hivi sasa, imejaa maovu na kujiona zaidi. Kwa miaka mingi Mungu aliruhusu wanyama wafe. Kwa njia hiyo wanadamu walikuwa na mahusiano ya karibu zaidi na Mungu wao mpendwa na waliongea nae. Aliwapenda na kuongea nao pia, kwa mfano, Abrahamu, Ayubu, Adamu na wengine wengi. Mungu anataka uhusiano huo leo kwako, lakini hutaki kujitolea kafara wanyama ili kuwa nae.

HEKIMA ZA MWANADAMU
Mwanadamu amejaribu kuwa na ukaribu na Mungu kwa kupitia njia mbali mbali, lakini si kwa njia ile ambayo Mungu alitegemea kutoka kwao. Kaini mtoto wa Adamu alitoa kafara ya mazao yake badala ya mnyama. Hata hivyo, Mungu hakupokea kafara ya Kaini kwa sababu haikuwa na thamani sawa na dhambi iliyokuwa ndani yake. Haijarishi Kaini alikuwa na mawazo mazuri au mabaya juu ya Mungu, bali kafar yake haikuwa na thamani ya kulipa deni la dhambi.

Ukweli ni kwamba watu bado hawajajua dhambi. Kwetu dhambi imekuwa ni neno la kidini. Wengi hawajajua kwa nini jambo lifanyike kwa ajili ya dhambi. Lakini Mungu ameona ni jinsi imekuwa ya kuume na ya kipekee tena yenye nguvu. Na jinsi ambavyo inaleta shida na masumbufu ndani yetu. Huko mbinguni kama siyo dhambi, tungeweza kuonana na Yesu uso kwa uso, tungekuwa huru kutoka dhambini na kuwa huru wenye nguvu zaidi na zaidi, pia tungekuwa mahali ambapo kila mtu awaye binadamu, au
malaika, au kiroho, angependa kuwepo. Wote tungependana na Mungu angeishi maisha ya upendo kwa wengine na siyo ya kibinafsi.

HEKIMA ZA MUNGU

Mungu ni mwerevu na kwa sababu ya hekima zake, amekuwa mkweli katika kile asemacho na afanyacho. Ikiwa hatutomficha, na kuiendea njia ile aliyotuandalia, kwa sababu ya dhambi, Bwana atajitoa na kwenda mbali nasi. Yeye ni Mungu mwenye upendo, asiye na ubinafsi, na wala hajihusishi na dhambi. Kama utaing’ang’ania dhambi na bila kinga yoyote, utajitenga mwenyewe na Mungu. Nawe hawezi kuja karibu yako ili umfahamu. Hata hivyo kumfahamu Mungu. Ni lazima uwe na kinga ya dhambi.

KUMJUA MUNGU
Kwa karne nyingi wema wa mwanadamu umekuwa ukitolewa kafara ya wanyama kwa Mungu. Wengi walidhani kuwa Mungu yuko mbali nao, lakini wachache walitambuwa kuwa Mungu yu pamoja nao. Hata hivyo, watu wengi wamekuwa wakiangalia zaidi dini, kwa matumaini kuwa wema zaidi mbele zake. Kwa kuwa hivyo, kunawafanya watu wajisikie vizuri , lakini kuna haja ya kusaidiana sisi kwa sisi. Kwa sababu sisi sote ni viumbe vya Mungu, isipokuwa kumjua Mungu kwa kupitia dini, ndicho kitutenganishacho. Tumeumbwa kwa mfano wa Mungu, naye yu kama sisi. Isipokuwa yeye si mdhambi, ni mwingi wa upendo na rehema. Ni wa upendo kwa amfikiriaye, amhisiye, ampendaye na kwa yule anayemjali, alituumba ili tuweze kumfahamu. Adamu, Ibrahimu, Musa, Paulo na wengine wengi walimpenda Mungu. Na aliwachukulia kila mmoja kuwa ni marafiki zake. Kila mmoja wao ni mzima na ana mjua Mungu. Wako pamoja nae sasa huko Mbinguni, kama alivyoahidi kuwa ikiwa utamjua yeye, nawe utakuwa nae kule Mbinguni.

Baba wa mbinguni alijua kuwa kafara ya mnyama haitoshi. Mwanadamu akaanza kupoteza hamu ya kumjua Mungu na kuridhika na mambo ya dini. Cha ajabu, Mungu akaamua kuja duniani kwa ajili ya kila mmoja wetu. Akaja, akaishi kama Mwanadamu, ili aweze kulipa deni la dhambi zetu. Kwa mara moja hiyo, watu waweze kuwa marafiki zake (Mungu). Fidia ya dhambi imekuwa kama tumekuwa nae kwa undani zaidi, kwa maumivu aliyoyapata, kwa maana huo wema wa Mwanadamu hauwezi ukalipwa kwa damu ya mnyaa kamwe.

YESU
Huyu ndiye Yesu, na ndiyo sababu alikuja duniani, yeye ni Mungu. Alikuja duniani kutoa kafara ya ndani kwa ajili ya dhambi zetu kila mmoja, ili kwamba yeyote atakaye mwamini Baba kupitia kifo chake, damu yake iliyomwagika msalabani kwa ajli ya dhambi zetu. Yesu hakuwa mdhambi. Hata sadaka aliyoitoa kwa kwa Mungu ilikubalika. Kifo chake kilikuwa kafara yakutosha. Alikufa na dhambi zetu. Kafara yake ilikuwa ya upendo na njia kwa kuweka daraja kati ya Mungu na mwanadamu kwamba tuweze kwenda na kumjua Mungu tena.

Yesu ni mwenye ushirikiano, ni mzuri, mwema na mwenye upendo. Matokeo ya dhambi zet ingekuwa uharibifu, kama ambavyo dunia yote ingeharibiwa kama kipindi cha nuhu. Mungu angeweka huruma yake ili tuendelee kuwepo, kafara aliyoitoa ilituepusha na uharibifu wowote na kutufanya wake. Ilikuwa ni upendo wa kujitolea mno! Yesu ni Mungu, ni Mungu mwenye uhuru. Nani awezaye kumzuia katika kutuangamiza sisi? Nani awezaye kulazimisha aweze kuja kutufilia sisi hapa duniani na dhambi zetu? Watu walidhani kuwa ni kazi ya Mungu kuokoa maisha yetu. Hapana, haikuwa kazi, bali upendo tu. Tunaweza kujiuliza ni upendo wa namna gani aliyokuwa nao hata kujitoa kwa ajili yetu? Hata tukiishi miaka milioni, hatustahili kile Yesu alichotenda. Yesu ni mwanaume na mwenye nguvu. Ana mamlaka yote juu ya kifo, na hii inathibitishwa pale Yesu aliporudi katika maisha yake baada ya kuwa amekwisha uawa.

IMEKWISHA
Sasa kwa kuwa maisha ya Yesu yametoweka, Mungu hayupo tayari kuona mwanadamu anapotea, hata kwa damu ya wanyama, dini nyingine hata kwa imani. Nyumba ya Mungu ibaki kuwa takatifu, na kwa ajilki ya Mungu tu. Nyumba ya Mungu imetobolewa kutoka Mbinguni hadi duniani na mkono wa Mungu, wakati Yesu yuko msalabani, anafungua njia kwa ajili ya uwepo wa Mungu. Yesu alisema kuwa “imekwisha” . kifo kilihitajika kam jibu pekee la dhambi. Na ilikuwa kwa kumtoa mwana wake wa pekee afe kwa ajili ya dhambi zetu. Na baba yake alihakiki na kumpokea kwa ajili yetu.

UTAONA UWEPO WAKE
Habari njema ni kwamba, hautokuwa mbali na Mungu, bali utakuja kwa Baba wa Mbinguni. Kwa unyenyekevu, mwombe atoe kafara ya mwana wake Yesu kwa ajili ya dhambi zako, na kwa furaha atafanya. Halafu utaongea nae, na ataongea nawe na kufanya urafiki na wewe ambao hautokwisha milele. Atakuwa karibu nawe, haijarishi nini kitakukuta katika maisha yako binafsi, au katika ulimwengu. Atakupenda, na atakusaidia.

Atakufanya umjue kupitia roho mtkatifu. Atahisi uwepo wake, naye atajibu maombi yako. Utaanza kumfahamu Yesu ambaye ni mwingi wa upendo, rehema na utu wema. Kuhusu maisha yake na dunia kwa ujumla, kama utakavyoongea nae, atakusikia, atakuja karibu yako.

Sio tu ataongea nawe kuhusu maisha yako, bali atakuonyesha na mawazo yake juu yako kutoka moyoni jmwake, kama jinsi ambavyo unajua mawazo ya rafiki, kipenzi chako yalivyo moyoni mwake. Pia atakuonyesha mahali pazuri (Mbingini) ambako utakuwa naye milele. Lakini sasa unaweza kumfahamu Mungu kwa uzuri zaidi. Kumjua Mungu siyo kwenda kanisani kwa sababu wanaompenda Kristo na kumjua, ndio walioko kwenye kanisa lake.

Mwamini Mungu, naye atakuonyesha nini cha kufanya. Biblia iliandikwa kwa uwezo wa roho mtakatifu kwa niaba yetu. Lakini haikumaanisha kuchukua nafasi ya kumjua yeye. Biblia ni neno la Mungu, na inatuelekeza kwa Yesu akupendaye na aliyekufa kwa ajili yako, na yupo kwako sasa hivi, anatak umjue! Wasiliana nasi kwa picha nzuri na za bure za Yesu.

By Permission: JESUS IS ALIVE

For Max Shimba Ministries Org.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW