Thursday, July 9, 2015

Yesu ni nani?

Yesu wa Nazareti ni nani kwako? Maisha yako hapa duniani na ya milele yanaguswa na jibu lako kwa swali hili?

dove
Nani, kwa maoni yako, ni...
  • Mtu wa ajabu kupita watu wote katika nyakati zote?
  • Nani aliyejitokeza kuwa mtu mashuhuri kwa vipindi vyote?
  • Kiongozi mkuu?
  • Mwalimu mkuu?
  • Mtu aliyefanya matendo mema kwa wanadamu kupita mwingine?
  • Mtu aliyeishi maisha matakatifu kuliko yeyote aliyewahi kuishi?
Tembea sehemu yoyote ulimwenguni. Ongea na watu wa dini yoyote. Haijalishi jinsi walivyoshikilia tabaka za dini zao, kama wanajua chochote kuhusu historia, watakubali kwamba hakujawahi kuwa na mtu kama Yesu wa Nazareti. Yeye ni mtu wa ajabu mno kuliko watu wote wa enzi zote.

Yesu alibadilisha mwenendo wa historia. Hata tarehe kwenye gazeti lako la leo inathibitisha kwamba Yesu wa Nazareti aliishi ulimwenguni karibu miaka 2,000 iliyopita. Maandishi kwa Kiingereza "B.C." yanasimamia nyakati kabla ya kuzaliwa kwa Kristo; vilevile maandishi "A.D." yanasimamia nyakati baada ya kuzaliwa kwa Kristo.
KUJA KWAKE KULITABIRIWA
Mamia ya miaka hata kabla ya Yesu kuzaliwa, maandiko yaonyesha wanabii wa Israeli wakitabiri kuja kwake. Agano la kale, lililoandikwa na watu wengi katika muda wa miaka 1,500, lina unabii zaidi ya 300 kuhusu kuja kwa Yesu. Yote yaliyotabiriwa yalitendeka, pamoja na kuzaliwa kwake kimiujiza, maisha yake matakatifu, kufa na kufufuka kwake.

Maisha aliyoishi Yesu, miujiza aliyotenda, maneno aliyosema, kufa kwake msalabani, kufufuka kwake, kupaa kwake mbinguni - yote yathibitisha kwamba yeye hakuwa mwanadamu peke yake bali alikuwa zaidi ya mwanadamu. Yesu alisema, "Mimi na Baba tu umoja" (Yohana 10:30), "Aliyeniona mimi amemwona Baba" (Yohana 14:9) na, "Mimi ndimi njia, na ukweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi." (Yohana 14:6).
MAISHA  NA UJUMBE WAKE HUSABABISHA MABADILIKO
Tazama maisha na mvuto wa Yesu wa Nazareti, Mesiya, katika historia yote na utaona kwamba yeye na ujumbe wake huleta mabadiliko makubwa katika mataifa na maisha ya wanaume na wanawake.5000Popote mafunzo yake yalipoenea, utakatifu wa ndoa, haki na sauti ya wanawake imetiliwa maanani; shule na vyuo vikuu vimeanzishwa; sheria za kulinda watoto zimeandikwa; utumwa umeachishwa; na mabadiliko mengine mengi yamefanywa kwa manufaa ya wanadamu. Maisha ya watu binafsi yamebadilishwa kiajabu. Kwa mfano, Lew Wallace, jemedari aliyejulikana na mwandishi shupavu, alikana Mungu yupo. Kwa miaka miwili, Bw. Wallace alisoma kwenye maktaba zilizo bora sana kule Ulaya na Merikani, akitafuta habari ambazo zingeangamiza kabisa dini ya Kikristo. Alipokuwa akiandika sura ya pili ya kitabu hicho, alijikuta ghafla ameanguka magotini na kulia kwa Yesu akisema, "Bwana na Mungu wangu."
Kwa sababu ya ushuhuda usioweza kukanwa, hakuweza kuendelea kukana kwamba Yesu Kristo alikuwa mwana wa Mungu. Baadaye, Lew Wallace aliandika kitabu kilichoitwa "Ben Hur", moja wapo ya vitabu shwari vilivyo andikwa katika lugha ya Kiingereza kuhusu nyakati za Kristo.

Vile vile, marehemu C. S. Lewis, profesa wa chuo kikuu cha Oxford, alikana kwamba Kristo alikuwa pia Mungu kwa miaka mingi. Lakini, yeye pia, kwa hekima za ukarimu, alijinyenyekeza mbele za Yesu kama Mungu na Mwokozi baada ya kusoma ushahidi usio na pingamizi kwamba Yesu pia alikuwa Mungu .
BWANA, MWONGO AU MWENDA WAZIMU?

Katika kitabu chake kilichojulikana sana "Mere Christianity", Lewis aliandika, "Mtu ambaye alikuwa mwanadamu peke yake na kusema maneno kama aliyoyasema Yesu hawezi kamwe kuwa mwalimu wa utu wema. Huenda ikawa alikuwa mwenda wazimu - sawasawa na mtu anayesema kwamba yeye ni yai lililochemshwa - au roho chafu kutoka kuzimu. Wewe lazima uchague. Kama yeye alikuwa, na hata sasa ni Mwana wa Mungu, au yeye ni mwenda wazimu au kitu kibaya zaidi. Unaweza kumwita mpumbavu au unaweza kujinyenyekeza chini ya miguu yake na kumwita Bwana na Mungu. Lakini tusije na maneno hohehahe tukisema kwamba yeye alikuwa mwalimu shupavu wakibinadamu tu. Yeye hajaacha hilo chaguo wazi kwetu."

Yesu wa Nazareti ni nani kwako? Maisha yako ya hapa duniani na pia ya uzima wa milele yatategemea jibu lako kwa swali hili.

Dini zote zingine zilianzishwa na wanadamu na zinategemea falsafa za kibinadamu, kanuni na pendekezo za tabia. Ondoa waanzilishi wa dini hizi kutoka idhini na tabaka za kuabudu, na machache sana yatabadilika. Lakini ondoa Yesu Kristo kutoka Ukristo na hakuna chochote kitakachobaki. Ukristo uliopendekezwa kwenye Biblia siyo falsafa ya maisha peke yake, wala siyo tabaka na njia za kimila za kuabudu. Msingi wa Ukristo wa kweli ni uhusiano wa kibinafsi na Mwokozi na Bwana aliyefufuka na anayeishi.
MWANZILISHI ALIYEFUFUKA
Yesu wa Nazareti alisulubiwa, akazikwa kwenye kaburi lililokopwa, na siku ya tatu alifufuka kutoka wafu; Ukristo niwa kipekee kwa ajili ya jambo hili. Ubishi wowote juu ya ukweli wa Ukristo utategemea uthibitisho wa kufufuka kwa Yesu wa Nazareti.

Katika enzi zote, waliohitimu katika masomo na kuchunguza sana mathibitisho ya ufufuo wameamini, na wangali wanaamini kuwa Yesu yuhai. Baada ya kuchunguza mathibitisho ya ufufuo kama yalivyoandikwa na waandishi wa Injili, marehemu Simon Greeleaf, aliyehitimu kwa mambo ya kisheria katika Harvard Law School, alisema; "Haingewezekana kamwe kwao kuendelea kusisitiza ukweli wa mambo walionena, kama Yesu kweli hakufufuka kutoka wafu, na kama hawakujua jambo hili kama walivyojua ukweli wowote mwingine walioujua kwa uhakika.
John Singleton Copley ambaye ni mwanasheria aliyetambulikana sana, alisema: "Najua kiasi kwamba ushahidi ni kitu gani; nakwambia, ushahidi kama ule uliotolewa kuthibitisha ufufuo bado haujawahi kuvunjwa."
SABABU ZA KUAMINI
Ufufuo ni msingi katika imani ya Mkristo. Kuna sababu kadha wa kadha ambazo wale wanaosoma kuhusu ufufuo wanaamini kuwa ufufuo ulitendeka:�
boatKUTABIRIWA: Kwanza, Yesu alitabiri habari za kifo chake na ufufuo na zikatendeka kadri na jinsi alivyotabiri ( Luka 18:31-33).

KABURI LILIYO WAZI: La pili, ufufuo ni kielelezo cha pekee cha kaburi lililo wazi. Ukisoma Biblia kwa makini, utaona kwamba kaburi ambalo walilolaza mwili wa Yesu lililindwa barabara na wanajeshi wa Kirumi na pia lilizibwa na jiwe. Kama Yesu hakuwa amekufa, bali alikuwa amedhoofika - kama wengine walivyosema, walinzi na jiwe pia lingezuia juhudi za kuhepa au kusaidiwa na wafuasi wake. Maadui wa Yesu hawangechukua mwili kwa sababu kukosekana kwa mwili huo pale kaburini ingalitia nguvu imani juu ya kufufuka kwake.
KUONANA KIBINAFSI: La tatu, ufufuo ni kielelezo cha kipekee cha kuonekana kwa Yesu na wafuasi wake. Baada ya kufufuka kwake, Yesu alionekana mara zisizopungua 10 na wale waliomjua na pia kwa watu 500 waliokusanyika pamoja. Bwana aliwathibitishia kwamba kuonekana kwake mara tatu hizikuwa ndoto. Alikula na kuongea nao na walimgusa ( 1 Yohana 1 :1).

KUZALIWA KWA KANISA: La nne, ufufuo ni sababu ya pekee ya kueleza sababu ya kanisa kuanzwa. Kanisa la Kristo ni chama kikubwa kuliko vingine vilivyoko sasa pia vilivyowahi kuwepo katika historia ya ulimwengu. Zaidi ya nusu ya mahubiri ya kwanza yaliyohubiriwa yalikuwa kuhusu ufufuo (Matendo 2:14-36). Hakika kanisa la kwanza lilijua kwamba jambo hili litakuwa msingi wa ujumbe wake. Maadui wa Yesu wangelikomesha wakati wowote kwa kuutoa mwili wa Kristo.

MAISHA YALIYOBADILISHWA:
 La tano, ufufuo ni kielelezo cha kipekee cha maisha yaliyobadilishwa ya wafuasi wake. Walimwacha kabla ya kufufuka kwake; baada ya kifo chake walikufa moyo na kuogopa. Hawakutarajia kwamba Yesu atafufuka kutoka wafu (Luka 24 :1-11).

Lakini baada ya kufufuka kwake na mambo waliyopata wakati wa Pentekote, hawa waliokufa moyo, waliopoteza hamu, wanaume kwa wanawake, walibadilishwa na nguvu za Kristo aliyefufuka. Katika jina lake, walifanya kishindo kikubwa duniani. Wengi walipoteza maisha yao kwa ajili ya imani yao; wengine waliudhiwa vibaya. Matendo yao ya ujasiri hayana kielelezo kamili isipokuwa kwamba waliamini Yesu Kristo kweli alifufuka kutoka wafu - jambo lililowatosha hata kukubali kufa kwa ajili yake.

Katika miaka 40 ya kufanya kazi na wataalamu wa vyuo vikuu ulimwenguni, sijawahi kukutana na mmoja ambaye ameyasoma mathibitisho ya dhati kuonyesha uungu wa Yesu wa Nazareti na pia kufufuka kwake, ambaye hakukubali kwamba yeye ni Mwana wa Mungu, Mesiya aliyeahidiwa. Ijapokuwa wachache hawaamini, wanasema kwa moyo wa kweli, "Sijachukua muda wowote kusoma Biblia au kuangalia mambo katika kihistoria yalitotendeka katika maisha ya Kristo."
jesusandgirlBWANA ANAYEISHI:  Kwa sababu ya ufufuo wa Yesu, wanafuasi wake wa kweli hawafuati tu orodha za mwanzilishi aliyekufa, bali wanauhusiano wa karibu na wakibinafsi na bwana aliyehai. Yesu Kristo yuhai leo na anabariki na kuimarisha maisha ya wote wanaomwamini na kumtii. Katika enzi zote, wengi wamedhihirisha kufa kwake Yesu Kristo, kati yao wakiwa watu waliotenda makuu ulimwenguni.

Mwanafizikia na mwanafalsafa wa Kifaransa Blaise Pascal alisema jinsi mwanadamu anavyomhitaji Yesu aliposema, "Kuna pengo katika moyo wa kila mwanadamu linayoweza kuzibwa na Mungu peke yake kupitia Mwana wake Yesu Kristo."
Je, ungependa kumjua Yesu Kristo kama Mwokozi wako? Unaweza! Yesu anahamu ya kuanza uhusiano wa kibinafsi uliojaa upendo kwako. Ameshafanya matayarisho yote.

SSource: http://www.whoisjesus-really.com/swahili/whois.htm

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW