UFUNUO WA YOHANA 1:1-7
Kitabu hiki kinaelezea jinsi itakavyokua baadaye kwa watendao maovu pamoja na wasiowaminifu, na pia watakatifu pamoja na waminifu. Lakini uzuri wa haya yote, ni jinsi kinavyotuelezea. Yesu ni nani hasa. Na kwa thibitisho sahihi na pasipo shaka kimeelezea kuwa Yesu ni Mungu.
Ni hoja ya uzima na mauti kumjua Yesu ni nani - Yohana 8:24,26 Yesu alisema, "Kwa hivyo naliwambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu, kwa sababu msiposadiki ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu"
Mathayo 22:36-38, Mariko 12:26-29 ...Yesu aliulizwa katika amri zote ni ipi ilio ya kwanza, na kwa upezi akakalili kumbukumbu la torati 6:4 "sikia ee israeli Bwana Mungu wetu bwana ni mmoja..." Yesu akiwa Mungu alijua hakuna kabisa Mungu mwingine ila yeye mwenyewe. Kijitabu hiki kimeandikwa ili kiweze kuthibitisha umoja wa Mungu.
THIBITISHO SABA ZINAZO AMINIKA
Kitabu hiki cha ufunuo wa Yohana kimetupatia thibitisho saba ambazo haziwezi kukataliwa ya kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu na Mungu.
Yohana aliamini jambo hili kabla ya kuandika kitabu hiki cha Ufunuo. Yohana wa kwanza 5:20 "...nasi twajua kwamba mwana wa Mungu amekwisha kuja naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake, yeye aliye wa kweli yaani ndani ya mwanawe Yesu Kristo huyu ndiye Mungu wa kweli na uzima wa milele."
1. THIBITISHO LA KWANZA
Ufunuo wa Yohana 1:8 Yesu akasema, "Mimi ni Alpha na Omega, mwanzo na mwisho, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja Mwenyezi."
Ufunuo wa Yohana 1:17-18 "...mimi ni wa kwanza, na wa mwisho, na aliye hai nami nilikuwa nimekufa; ...na tazama, ni hai hata milele na milele."
Yesu alisema yeye ndiye wa kwanza na wa mwisho, hakika hili lamthibitisha yeye ni Mungu, kwa maana Mungu wa Israeli alisema katika kitabu cha Nabii Isaia 44:6 "...Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu."
Je ni thibitisho lingine lipi tunahitaji litufahamishe Yesu ni Mungu?
Kuelewa jambo hili vizuri utapaswa uelewe hali mbili za asili ya Mungu (dual nature). Mungu ambaye ni Roho alichukua mwili wa nyama kwa muda wa miaka thelathini na nusu "Emmanuel" .
Yohana 1:1 "Hapo mwanzo kulikuwako na Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu."
Yohana 1:14 "...Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu ---“ (Mungu) alifanya jambo hili aweze kutoa uhai wake na kumwaga damu kwa ondoleo la dhambi zetu.
2.THIBITISHO LA PILI
YOHANA 4:2 "...Na mara nalikuwa katika roho, na tazama kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na Mmoja ameketi juu ya kile kiti."
UFUNUO 4:6-8-- "Na kwa kile kiti kulikuwa na makundi yaliokuwa yakimwabudu aliyekalia kiti hicho."
Mstari wa 8, unatuelezea vizuri ni nani aliyekuwa amekikalia kiti hicho. "Wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu Bwana Mungu mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja.
UFUNUO 1:8 Yesu akasema ya kwamba yeye ndiye aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja, Mungu mwenyenzi. Kuna Mungu Mwenyenzi mmoja tu.
UFUNUO 4:11 "Umestahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kupokea utukufu na heshima na uweza; kwa kuwa wewe ndiwe uliyeviumba vitu vyote,--"
YOHANA 1:3 na (10)...yazungumza juu ya Yesu ya kwamba vitu vyote viliumbwa naye, na ulimwengu haukumwelewa.
WAKOLOSAI 1:16-17 Mtume Paulo alisema,"kwa kuwa katika vitu vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake," Na kwa thibitisho zaidi ya kuwa Yesu Kristo ndiye Bwana Mungu Mwenyezi, tunasoma kwenye kitabu cha Isaya 44:24...Mungu mwenyenzi kwa agano la kale akisema..."Mimi ni Bwana, nifanyaye vitu vyote, nizitandaye mbingu peke yangu; nienezaye nchi; ni nani aliyekuwa pamoja nami;
UFUNUO 5:9....Nao waimba wimbo mpya kwa Mwana kondoo wakisema, "Wewe ....ulitukomboa ukamnunulia Mungu kwa damu yako..." Damu ya nani?
MATENDO YA MITUME 20:28...Kanisa la Mungu lilinunuliwa kwa damu yake (Mungu) mwenyewe.
YOHANA WA KWANZA 3:16--"Katika hili tumelifahamu pendo la Mungu, kwa kuwa Yeye (Mungu) aliutoa uhai wake kwa ajili yetu."
3. THIBITISHO LA TATUUFUNUO 11:16-17
Na wale wazee ishirini na wanne waketio mbele za Mungu .... wakaanguka kifudifudi wakamsujudia Mungu, wakisema, Tunakushukuru wewe, Bwana Mungu
(Mstari wa 17)... Mwenyezi uliyeko na uliyekuweko na utakayekuja. (Read English King James version).
(Mstari wa 15)...Kwa sababu umeutwaa uweza wako ulio mkuu, na kumiliki. Huu mstari unaelezea kuwa Yesu atamiliki milele na milele! Na kuthibitisha zaidi. Soma Ufunuo 1:8...Yesu akasema mimi ndimi (mmoja) aliyeko, aliyekuweko na atakayekuja, Mwenyezi.
4. THIBITISHO LA NNE
UFUNUO 15:3….”Nao wauimba wimbo wa Musa, …na wa Mwana - kondoo, wakisema, Ni makuu na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu mwenyezi. Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa watakatifu.
Yeye sio tu Mfalme wa watakatifu pia ni Mfalme wa wafalme! Hii ni mara ya nne katika kitabu hiki kinachotufahamisha Yesu mfalme wa watakatifu kuwa ni yeye Bwana Mungu Mwenyezi…na mengi inafuatilia!
5. THIBITISHO LA TANO
UFUNUO 19:13-16…”Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu; na jina lake aitwa, Neno la Mungu…..Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyanga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi. Naye ana jina limeandikwa katika vazi lake na paja lake, MFALME WA WAFALME, NA BWANA WA MABWANA.
6. THIBITISHO LA SITA
UFUNUO 21:22-23….”Nami sikuona Hekalu ndani yake kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana kondoo, ndio hekalu lake.
(mstari wa 23) Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana-kondoo.
SIRI ama (FUMBO)
Mungu Mwenyezi na Mwana kondoo ni wamoja. Yohana wa kwanza 10:30…Yesu akasema, “Mimi na Baba tu Umoja.”
Timotheo wa kwanza 3:16…Paulo akaandika, “Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu…Mungu alidhihirishwa katika mwili,( Mwana-kondoo) akajulika kuwa na haki katika roho. Akaonekana na malaika akahubiriwa katika mataifa, akaaminiwa katika ulimwengu. Akachukuliwa juu katika utukufu.
Yesu alijua ilikuwa siri ( ama fumbo) Yohana 16:25-26
“Na hayo nimesema nanyi kwa mithali saa yaja ambapo sitasema nanyi kwa mithali. Lakini nitawapa wazi wazi habari ya Baba.”
UFUNUO 22:3….Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-kondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumwa wake…”sio watumwa wao ni wake” Nao watamuona uso wake (sio nyuzo zao..ni wake na jina lake-sio majina yao ni lake) litakuwa katika vipaji vya nyuso zao.
Tafadhali mpendwa ...elewa vizuri sio wao wala zao bali “yeye na ake.”
UFUNUO 4:2 Kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi “umoja wa Mungu ni kibibilia na iko wazi na sawa kabisa.
THIBITISHO LILILO LA MWISHO "SABA"
Thibitisho la mwisho na la kutokataliwa ni ya kwamba Baba na Mwana ni wamoja hiyo inamaanisha ya kuwa Yesu Kristo na Baba ni Wamoja.
UFUNUO 22:16 ”...Mimi Yesu, nimemtuma malaika wangu
kushuhudia mambo haya kwa ajili ya makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile Nyota ya asubuhi ing'aayo.. Hizi ni asili mbili za Yesu Kristo. Asili ya uungu na uuwana-damu, Nabii Isaya 9:6 ... afunua ukweli huu mkuu “...Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; ... Jina lake ataitwa... . Mungu mkuu, Baba wa milele...” Je,ni kweli, mwana ndiye Mungu mkuu na ndiye Baba?
kushuhudia mambo haya kwa ajili ya makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daudi, ile Nyota ya asubuhi ing'aayo.. Hizi ni asili mbili za Yesu Kristo. Asili ya uungu na uuwana-damu, Nabii Isaya 9:6 ... afunua ukweli huu mkuu “...Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; ... Jina lake ataitwa... . Mungu mkuu, Baba wa milele...” Je,ni kweli, mwana ndiye Mungu mkuu na ndiye Baba?
Yohana 16: 5 Vyote alivyo navyo Baba ni vyangu. Ndiyo maana nimesema Roho atachukua yaliyo Yangu na kuwajulisha ninyi.
Yote niliyotaka kuandika kwenye kijitabu hiki ni ukweli wote na sio lingine ila ukweli mtupu, lazima tumwabudu Mungu katika Roho na katika kweli.
Ukweli utakuweka huru kabisa.
Max Shimba Ministries Org
No comments:
Post a Comment