KUTOKA 20:1 – 6 MUNGU akanaena maneno haya yote akasema, mimi ni Bwana, MUNGU wako niliyekutoa katika nchi ya Misri katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilichopo juu mbinguni, wala kilichopo duniani wala kilichopo majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia, kwa kuwa mimi BWANA MUNGU wako ni MUNGU mwenye wivu, nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukizao. Nami nawarehemu maelfu wanipendao, na kuzishika amri zangu. Ndugu msomaji wa makala haya ya Nabii Hebron, na uliyeumbwa na MUNGU tena umefanana na yeye, ni ili umwabudu yeye na kuzishika amri zake peke yake ili upone na ile siku ya mwisho na wewe ukafurahie pamoja na yeye paradiso ila ukienda kinyume na maagizo yake hakika ujijue 100% wewe hauta kwenda mbinguni hata kama unajifariji angalia matendo yako .
Ukisoma kutoka 20: 4 MUNGU anasema usije ukatengeneza sanamu yeyote halafu ukaitumia wakati wa kuomba, sanamu ya aina yeyote iwe ni ya mnyama, au mwanadamu kwa jinsia yeyote kike / kiume, wala kitu chochote kilichopo juu mbinguni (Nitaelezea hapa kidogo ili mpate kufunguka ufahamu na adui ambaye ndiye huyo miungu ya uongo asikupate tena. Biblia inasema na maneno haya ni MUNGU ndiye aliyeyasema na akatoa amri hii, usiabudu hata kitu kilichopo mbinguni). Sasa kuna watu baadhi yao wanaabudu mwezi,nyota, jua , hivi vipo juu ya nchi . Hii ni makosa na unaposhiriki tu , wewe tayari unakuwa unamwabudu MUNGU mwingine ambaye ni mungu wa uongo. MUNGU huyu ni kweli ndiye aliyeziumba hata hizo nyota, jua na mwezi. Na unapoviabudu au kuvisujudia matokeo yake na wewe unakuwa tayari umesha muasi MUNGU aliyekuumba wewe na ukaiacha njia yake ya kweli , ukaifuata ya uongo. Huyu ndiye MUNGU wa Ibrahimu, Isaka, Yakobo, na Eliya na ndiye aliyewaumba Adamu na Hawa pia ndiye Baba yake YESU KRISTO WA NAZARETI , na kwa jina lingine anaitwa Masihi. Akasema pia wala kilichopo chini ya maji kisiabudiwe yani viumbe vyote na hata vilivyopo duniani. Yeye alishajua kuwa haya yatatokea watu watakuja kudanganyika na shetani kama alivyosema ili mzivunje amri zake mpotee na yeye anasema katika kitabu cha Matendo 7:43 .
Wakati zile kule jangwani walipoabudu sanamu MUNGU akawaambia nanyi mlichukua hema ya Moleki , na nyota za mungu wa rehani, sanamu mlizozifanya ili kuziabudu, nami nitawahamisha mwende mbali kupita Babeli kwa wanaoabudu vitu ambavyo MUNGU alishavikataa, watu hao hawataingia Babeli, Babeli maana yake ni mlango wa kumwona MUNGU alipo, au kwa maana nyingine ni mbinguni. Sasa kama unafanya au kushiriki hayo ujijue wazi wazi tayari wewe umesha fungiwa kwenda mbinguni haijalishi unalitaja jina lake halafu unaviabudu vitu hivyo, huko ndipo kuvitumikisha, unavishika , unavinyenyekea na hata kuvibusu na kuviwekea au kutolea sadaka, hapo tayari unatumikishwa na sanamu, au unatumikishwa na mwezi au jua, nyota vitu ambavyo aliviumba mwenyezi MUNGU . Pia unatakiwa ujiulize swali hivyo vitu ndiyo MUNGU ? Au mwezi, nyota, jua na masanamu ndivyo vilivyokuumba wewe? Na wengine watasema hawa viabudu ila wanavishika tu ! Biblia inasema hata kuvitumikisha ni makosa matupu na ni ubatili mbele zake mwenyezi MUNGU aliye mkuu kuliko vitu vyote alivyoviumba. Jibu utalipata utaona hivi vyote aliviumba peke yake na ni mali yake!! Hata kibinadamu haingii akilini, nitatoa mfano huu ; tajiri na mali zake na ni atakaye heshimiwa, je ni mali za tajiri au tajiri aliyezitengeneza mali.?
Sasa embu angalia jinsi shetani alivyo wapotosha wanadamu wakaacha kumpa MUNGU wa kweli heshima yake na kumtukuza yeye tu kama apendavyo na matokeo yake hawa wanadamu walioumbwa na huyu MUNGU tena kwa sura yake , badala ya kumpatia heshima MUNGU,wanavipatia heshima vitu vyake alivyoviumba yeye na wengine wakaona haifai kumpatia MUNGU heshima yake wakaamua kujitengenezea sanamu kama wana wa Israeli walivyofanya na Haruni kule jangwani mpaka Musa akaja kuivunja hiyo sanamu ya ndama, hii ni picha halisi inayoonyesha jinsi wanadamu walivyopotea na wakijua wao wapo salama au sahihi katika kumfuata MUNGU aliye halisi, Alpha na Omega. Pia ujiulize kama yeye ni Alfa na Omega (yani mwanzo na mwisho) Yaani anaouwezo mkubwa zaidi kuliko vyote, sasa embu funguka akili yako uone ulivyopotea au wanadamu wanavyopotezwa. Mwezi, nyota, jua hivyo siyo MUNGU wa kweli, hivyo ameviumba yeye. Na shetani amewakamata watu fahamu zao waziabudu hizo nyota, mwezi, jua ili mfungiwe kwenda mbinguni. Na wote wanaoabudu vitu hivyo tayari ujijue mlango wa mbinguni umefungwa kwao. Maana mbinguni sipo kwa mungu anayeitwa mwezi, jua na nyota. Mbinguni ni mahali pa MUNGU aliye hai aliyeumba vitu vyote na malaika zake,na serikali yake tu, na wale watakaushinda ulimwengu huu kwa kuacha dhambi na kuwa watakatifu na kumfuata YESU 100% ndio watakaokwenda. Maana yeye ndiye njia ya uzima na pasipo huyo YESU hautaweza kumuona MUNGU ambaye ndiye Baba yake.
(Warumi 10:9 ). Na ili uende mbinguni ni lazima uwe mfuasi wake YESU WA NAZARETI uwe wake, UBATIZWE UBATIZO WA MAJI MENGI, YANAYOTEMBEA KAMA MTO JORDANI NA UDUMU KATIKA UTAKATIFU KATIKA MAISHA YAKO YOTE. NOTE: Natumaini umezidi kufunguka ufahamu wako na usikubali kupotezwa katika ulimwengu huu, mambo yameharibika 98% ni shetani amewakamata wanadamu ili waangamie kama yeye, na wewe usiende mbinguni. WACHA KUSHIRIKI IBADA HIZO, KAMA ULIKUWA HUJUI, TUBU NA UTASAMEHEWA NA UOKOKE. SALA YA TOBA BWANA YESU NATUBU, NAOMBA UNISAMEHE, UNIANDIKE JINA LANGU KWENYE KITABU CHAKO CHA UZIMA WA MILELE UNIONGOZE PALIPO SALAMA MAANA WEWE UNAPAJUA ILI NISIJEANGAMIA TENA, NISHIKE MKONO MIMI NI MALI YAKO KUANZIA SASA. ASANTE YESU WA NAZARETI.
No comments:
Post a Comment