Wednesday, July 1, 2015

UTATA NA SHAKA MBALI MBALI KATIKA HADITH ZA MUHAMMAD

Hadithi za Bukhari
Mamia ya maelfu ya hadithi (mapokeo) yanadai kuelezea mafundisho na matendo ya Muhammad na wafuasi wake wa karibu. Waislam wa kale walizichambua hadithi hizi ili kuona ni zipi kati yake ni za kweli. Kuna makundi sita ya hadithi zinazofikiriwa na Wasuni kuwa "sahihi" au halisi na zenye mamlaka ya kidini. Hadithi hizi huchukuliwa kuwa ni muhimu karibu sawa na Kurani yenyewe. Kundi refu zaidi ni Sahih al-Bukhari lenye juzuu tisa na hadithi 7,275. Mambo yafuatayo yana mvuto mkubwa kwa wasomaji wote Waislam na wasio Waislam toka kwenye hadithi za kundi la Bukhari. Dondoo hizi zimetolewa toka kwenye kitabu kiitwacho Tafsiri za Kiarabu na Kiingereza za Maana za Sahih Al-Bukhari kilichoandikwa na Dr. Muhammad Mushin Khan wa Chuo Kikuu cha Kiislam cha Medina Al-Munawwara, Saudi Arabia.

Muhammad Haabudiwi
"Baada ya hapo Abu Bakr alisema Tashah-hud (yaani hakuna mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wake)... Abu Bakr alisema, ‘Amma ba’du, yoyote miongoni mwenu aliyemwabudu Muhammad, basi Muhammad amekufa, lakini yoyote aliyemwabudu Mungu, Mungu yu hai na hatakufa kamwe. Mungu alisema: ‘Muhammad ni Mtume tu’" Bukhari juzuu ya 2 kitabu cha 23 (Kitabu cha Misiba) sura ya 3 na. 333 uk.188-189.
Hata hivyo Waislam wanamthamini sana Muhammad. "Kwa [msaada wa] Allah, Mtume wa Allah alipotema mate, mate yaliangukia kwenye mkono wa mmoja wa (yaani washiriki wa nabii) ambaye alifuta uso na ngozi vyake; alipowaamuru, washiriki wake walitimiza" maagizo yake mara moja; aliponawa walipigania kuchukua maji yaliyobakia; na walipoongea naye, walipunguza sauti zao na hawakumwangalia usoni mara kwa mara kwa ajili ya heshima." Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 50 (Masharti, ‘Conditions’) sura ya 13 na. 891 uk.564-565.

Marufuku Vinywaji Vikali
"‘Aisha [mke wa Muhammad] Nabii alisimulia akisema, ‘Vinywaji vyote vyenye kuleta ulevi ni Haram (vimezuiliwa) kunywa." Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 4 (Kitabu cha Kujitakasa) sura ya 75 na. 243 uk.153.
"Abu Huraira alisimulia: ‘Nabii alisema, ‘Mzinzi, wakati anafanya tendo la ndoa lisiloruhusiwa si muumini; na mtu yeyote, wakati anapokunywa kinywaji chenye kulevya, si muumini; na mwizi, wakati anapoiba si muumini" Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 69 (Kitabu cha Vinywaji) sura ya 1 na. 484 uk.339.

Waislam pia wamezuiliwa kuuza mvinyo, sanamu na nyama ya nguruwe. Muislam Sahih juzuu ya 3 kitabu cha 9 (Kitabu cha Biashara) sura ya 621-622 na.3835-3840 uk.828-830. Hawaruhusiwi kununua, kuuza au kubeba mvinyo. Ibn-i-Majah juzuu ya 4 kitabu cha 30 (Kitabu cha Vinywaji) namba 3380-3381 uk.493-494; juzuu ya 4 kitabu cha 30 na.3382 uk.494. Kuuza pombe kumezuliwa kwenye Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 8 (Kitabu cha Maombi) sura ya 73 na. 449 uk.267.

Je Muhammad Aliona Mwezi Ukigawanyika Vipande Viwili?
"Ombi la wapagani kwa Nabii kuwa awaonyeshe muujiza. Nabii aliwaonyesha kugawanyika kwa mwezi. ‘Abdullah bin Massud alisimulia: Wakati wa uhai wa Nabii mwezi uligawanyika vipande viwili na Nabii alisema, ‘Shuhudia (jambo hili).’" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 56 (Wema na Uadilifu wa Nabii na Washiriki Wake) sura ya 26 na. 830 uk. 533.
"Anas alisimulia kuwa watu wa Maka walimwomba Mtume wa Mwenyezi Mungu awaonyeshe muujiza, na kwa ajili hiyo aliwaonyesha kugawanyika kwa mwezi." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 56 (Wema na Uadilifu wa Nabii na Washiriki Wake) sura ya 26 na. 831 uk.533.
"Ibn ‘Abbas alisimulia: Mwezi uligawanyika vipande viwili wakati wa uhai wa Nabii." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 56 (Wema na uadilifu wa Nabii na Washiriki Wake) sura ya 26 na. 832 uk.534.

Nyota Zinapaswa Kuyapiga Mashetani?
"Uumbaji wa nyota ulikuwa na malengo matatu, yaani kuwa mapambo ya mawingu, kupiga mashetani, na ishara za kuongozea wasafiri. Kwa hiyo, mtu yoyote anapojaribu kutafuta tafsiri tofauti, amekosea na anapoteza nguvu zake..." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 (Mwanzo wa Uumbaji) sura ya 3 maelezo ya mwenye kutafsiri kabla ya na. 421 uk.282.


Kumbukumbu ya Abu Huraira
"Abu Huraira alisimulia: Nilisema, ‘Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nasikia masimulizi mengi toka kwako lakini nayasahau.’ Alisema, ‘Tandaza shuka lako.’ Nilitandaza shuka langu na alitembeza mikono yake miwili kana kwamba anachota kitu na akamimina kwenye shuka na kusema, ‘Jifunge.’ Nilijifunga mwilini mwangu na toka wakati ule sijasahau Hadithi hata moja." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 56 (Wema na Uadilifu wa Nabii na Washiriki Wake) sura ya 27 na.841 uk.538. Pia Bukhari juzuu ya 9 kitabu cha 92 (Kuizingatia Kurani na Mapokeo ya Nabii) sura ya 22 na.452 uk.332; juzuu ya 1 kitabu cha 3 (Kitabu cha Maarifa) sura ya 43 na.119 uk.89.

Shetani Puani Mwako
"Abu Huraira alisimulia: Nabii alisema, ‘Kama mtu yeyote kati yenu akiamka toka usingizini na kutawadha [kaida ya kujitakasa], anapaswa kuosha pua yake mara tatu kwa kuingiza maji na kuyatoa kwa kuhema kwa sababu Shetani alikuwa kwenye sehemu ya juu ya pua yake usiku mzima."(1) Maelezo ya mwenye kutafsiri (1) yanasema, "Tunapaswa kuamini kuwa ni kweli kwamba Shetani anakaa kwenye sehemu ya juu ya pua ya mtu hata kama hatuwezi kuelewa kwa sasa, kwani jambo hili linahusika na ulimwengu usioonekana ambao hatujui lolote kuhusiana nao isipokuwa yale ambayo Mwenyezi Mungu ametuambia kupitia Mtume wake." Bukhari sura ya 4 kitabu cha 54 (Mwanzo wa Uumbaji) sura ya 10 na.516 uk.328.

Kumwamini Muhammad Wakati Nzi Wanakuwepo
"Abu Huraira alisimulia: Nabii alisema, ‘Kama nzi ameangukia kwenye kinywaji cha mtu yoyote kati yenu, na amchovye (kwenye kinywaji), kwani bawa lake moja lina ugonjwa na lingine lina tiba ya huo ugonjwa." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 (Mwanzo wa Uumbaji) sura ya 16 na.537 uk.338. Tazama pia Abu Dawud juzuu ya 3 kitabu cha 21 (Kitabu cha Vyakula) na.3835 uk.1080.

"Abu Huraira alisimulia: Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema, ‘Kama nzi ameangukia kwenye chombo cha yoyote kati yenu, mtu huyo na amchovye huyo nzi (kwenye chombo) kisha amtupe, kwani kwenye bawa lake moja kuna ugonjwa na kwenye lingine kuna uponyaji (1) (kiuasumu), yaani tiba ya ule ugonjwa." Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 71 (Kitabu cha Dawa) sura ya 58 na.673 uk.452-453.

Maelezo ya mwenye kutafsiri (1) yanasema, "Katika taaluma ya uganga inafahamika sana siku hizi kwamba nzi hubeba vijidudu vinavyosababisha magonjwa [pathogens] kwenye baadhi ya sehemu za mwili wake kama alivyosema Nabii (karibu miaka 1400 iliyopita wakati ambapo binadamu walikuwa na ufahamu mdogo sana wa uganga wa kisasa.) Vivyo hivyo, Mungu aliumba vumbe na namna za utendaji vinavyoua hivi vijidudu vyenye kusababisha magonjwa mf. Kuvu ya penicillin (penicillin Fungus) huua vijidudu kama Staphalococci na vinginevyo. Hivi karibuni majaribio yaliyofanywa chini ya usimamizi yameonyesha kuwa nzi hubeba ugonjwa (pathagens) pamoja na viuasumu vya vijidudu hivyo. Kwa kawaida nzi anapogusa chakula kinachomiminika huathiri kimiminika kwa vijidudu vyake, hivyo ni lazima kumchovya ili aweze kutoa viuasumu vya vijidudu hivyo kwa lengo la kusawazisha vijidudu hivyo. Kuhusiana na somo hili pia niliandika kwa rafiki yangu kupitia kwa Dr. Muhammad M. El-SAMAHY, mkuu wa idara ya hadithi ya Chuo Kikuu cha Al-Azhar CAIRO (Misri) ambaye ameandika makala kuhusu Hadithi hii na kuhusiana na taaluma ya uganga amesema kuwa wataalamu wa vijidudu vidogo (microbiologists) wamethibitisha kuwa kuna chembe chachu zenye kukata kwa urefu zinazoishi kama vimelea ndani ya tumbo la nzi na chembe hizi chachu hujichomoza kupitia mishipa ya kupumulia ya nzi na kama mtu akimchovya nzi kwenye kimiminika, chembe hizi hupasuka kwenye kimiminika na vitu vilivyomo kwenye chembe hizi ni viuasumu vya vijidudu ambavyo nzi huvibeba."

Karibu madaktari wote, kama si Waislam, hudhihaki wakisika kuhusu kumchovya nzi kwa makusudi kwenye kinyaji chako.

Muhammed Alikuwa na Dhambi
"Abu Huraira alisimulia: ... Unasemaje katika kituo kati ya Takbir na masimulizi? Nabii alisema, ... O Mola! Niepushe na dhambi (makosa) zangu kama mashariki na magharibi zilivyotengwa na nioshe dhambi ili niwe mweupe kama vazi lililooshwa uchafu (baada ya kusafishwa kikamilifu). O Mola! Nioshe dhambi zangu kwa maji, theluji na mvua ya mawe." Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 12 (Tabia za Maombi) sura ya 8 na.711 uk.398. Tazama pia Sura 40:55; 48:1-2, na Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 2 (Imani) sura ya 13 na.19 uk.23; juzuu ya 1 kitabu cha 12 (Tabia za Maombi) sura ya 57 na.781 uk.434; juzuu ya 6 kitabu cha 60 (Kitabu cha Maoni) sura ya 3 na.3 uk.4; juzuu ya 8 kitabu cha 75 (Maombi) sura ya 3 na.319 uk.213.

Muhammad Aliwahi Kulogwa (Kwa Apizo, ‘Under a Spell’)
" ‘Aisha anasimulia: Nabii alifanyiwa uchawi hata akaanza kudhani kuwa anafanya kitu fulani wakati hakuwa anafanya. Siku moja alimwomba (Mungu) kwa muda mrefu sana kisha akasema, ‘Naona kuwa Mungu amenipa mwongozo wa namna ya kujitibu mwenyewe.’..." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 (Mwanzo wa Uumbaji) sura ya 10 na.490 uk.317. Tazama pia juzuu ya 4 kitabu cha 53 (Wajibu wa Khumus) sura ya 34 na.400 uk.267, juzuu ya 8 kitabu cha 73 (Mienendo Myema) sura ya 56 na.89 uk.56-57, juzuu ya 8 kitabu cha 75 (Kitabu cha Maombi ‘Book of Invocations’) sura ya 59 na.400 uk.266-267. Juzuu ya 7 na.658-660 uk.441-443. Pia tazama Muislam Sahihi juzuu ya 2 kitabu cha 4 (Kitabu cha Sala) sura ya 309 na.1888 uk.411

Muhammad alilogwa. Alisimulia ‘Aisha: Nabii aliendelea kwa kipindi fulani akidhania kuwa anafanya tendo la ndoa na mke wake, lakini haikuwa hivyo. Siku moja alisema kwangu, "O ‘Aisha! Mungu ameniagiza kuhusiana na suala nililomuuliza. Watu wawili walikuja, mmoja alikaa karibu na miguu yangu na mwingine karibu na kichwa changu. Yule aliyekuwa karibu na miguu yangu alimuuliza yule wa karibu na kichwa changu (akininyooshea kidole), ‘Mtu huyu ana shida gani? Yule mwingine akamjibu, ‘Ameathirika na uchawi. Yule wa kwanza akauliza, ‘Ni nani aliyemfanyia uchawi?’ Yule mwingine akajibu, ‘Lubaid bin A’sam." Yule wa kwanza akauliza, ‘(Alitumia) nyenzo gani?.’ Yule mwingine alijibu ‘Ngozi ya chavua ya mtende wa kiume na chanio lililowekwa nywele, na kuwekwa chini ya jiwe kwenye bwawa la Dharwan.’" Kisha Nabii alikwenda kwenye bwawa lile na kusema, "Hili ndilo bwawa lilelile nililoonyeshwa kwenye ndoto. Ncha za mitende yake inaonekana kama vichwa vya mashetani, na maji yake yanaonekana kama mchanganyiko wa hina."… ‘Aisha aliongeza, "(Mchawi) Lubaid bin A’sam alikuwa anatokea Bani Zuraiq, mshirika wa Wayahudi." Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 73 (Mienendo Myema) sura ya 56 na.89 uk.57. Tazama pia Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 75 (Kitabu cha Maombi ‘Book of Invocations’) sura ya 59 na.400 uk.266

Mabinti wa Allah
Uarabuni kabla ya Muhammad, kabila la Muhammad, Quaraysh, lilimwamini Mungu aitwaye Allah (au Al’Ilah) aliyekuwa na mabinti watatu walioitwa Al-Lat, Al-Uzza, na Manat.

" ‘Urwa alisema, ... kuhusiana na Ansar aliyezoea kumdhania Ihram kuwa anaabudu sanamu anayeitwa ‘Manat’ ambaye walizoea kumwabudu kwenye sehemu iliyoitwa Al-Mushallal..." Bukhari juzuu ya 2 kitabu cha 26 (Hija) sura ya 78 na.706 uk.413.

"Mstari huu ulifunuliwa kwa kuhusiana na Ansar aliyekuwa anamdhania Ihram kuwa sanamu Manat ambaye aliwekwa karibu na sehemu iliyoitwa Qudaid..."Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 27 (‘Hija ya Umra) sura ya 10 na.18 uk.11. Al-Lat, Al-Uzza wameelezewa Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 74 (Kitabu cha Kuomba Ruhusa ya Kuingia) sura ya 52 na.314 uk.209; juzuu ya 5 na.375 uk.259

Mistari Iliyofutwa Kwenye Kurani
"Baada ya hapo, Mungu alitufunulia mstari uliokuwa miongoni mwa ile iliyofutwa baadaye." Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 59 (Kitabu cha Safari za Kijeshi) sura ya 27 na.416 uk.288.

"Anas bin Malik alisimulia: ... Walifunuliwa wale waliouawa Bi’r-Ma’una, mstari wa Kurani tuliozoea kuukariri, lakini badaye ulifutwa. Mstari wenyewe ulikuwa: ‘Wafahamishe watu wetu kuwa tumekutana na Bwana wetu. Amefurahishwa nasi na ametufurahisha.’" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52 (Kitabu cha Jihad) sura ya 19 na.69 uk.53. Tazama pia Historia ya al-Tabari juzuu ya 7 uk.156.
Kumbukumbu nyingine za mistari iliyofutwa ni Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52 (Kitabu cha Jihad) sura ya 8 na.57 uk.45, Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 52 (Kitabu cha Jihad) sura ya 184 na.299 uk.191, naBukhari juzuu ya 5 kitabu cha 59 (Kitabu cha Safari za Kijeshi) sura ya 27 na.421 uk.293 zote zinarudia kitu hicho hicho kuhusu mstari huo huo.

Wakati fulani Muhammad aliafikiana na kusema kuwa kuhusiana na mabinti wa Allah kwenye Sura 53:19 "sala ya ya kuombea ilipaswa kutumainiwa." Muhammad alisema tunapaswa kutegemea msaada wa sanamu hizi tatu.
Wafuasi wa Muhammad walishangazwa kuwa amesema hivi. Baadaye, Muhammad alibadilisha msimamo wake na kusema kuwa Shetani alimdanganya. Mistari hii ilibatilishwa au kutolewa. Wanazuoni wa Kiislam wanaiita mistari hii "aya za Shetani." Inafurahisha kusoma maelezo ya Waislam kuhusu namna ambayo nabii wa kweli angeweza kusema hivi.

Tofauti na Yesu
Jambo moja ambalo Wakristo na wengi wa Waislam wanakubaliana ni kuwa Yesu hakuwa na dhambi. Kwa ulinganisho, soma kuhusu maisha ya Yesu kwenye Injili.

Muhammad na Kuuza Watumwa
"Anas bin Malik alisimulia: Mtume wa Mungu alikuwa safarini na alikuwa na mtumwa Mwafrika aitwaye Anjasha, na alikuwa akiendesha ngamia..." Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 73 (Mienendo Myema) sura ya 95 na.182 uk.117.

"Anas alisimulia: ... Na Anjashah, mtumwa wa Nabii [Muhammad], alikuwa akiendesha ngamia..." Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 73 (Mienendo Myema) sura ya 111 na.221 uk.142.

"Jabir bin ‘Abdullah alisimulia: Mtu mmoja miongoni mwetu alitanganza kuwa mtumwa wake angepewa uhuru baada ya kifo chake. Nabii alimwita yule mtumwa na akamuuza (1) Mtumwa yule alikufa mwaka uleule." Rejeo chini ya ukurasa (1) inasema "Mtoaji uhuru alikuwa na shida, kwa hiyo Nabii alimuuza mtumwa kwa niaba yake na kumruhusu kuiondoa ahadi yake ya kumpa mtumwa uhuru baada ya kifo chake." Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 45 (Kitabu cha Rehani kwenye Sehemu Zinazomilikiwa na Wakazi wa Kudumu ‘The Book of Mortgaging in Places Occupied by Settled Population’) sura ya 9 na.711 uk.427.

"Kisha mtu aitwaye Rifa’a bin Zaid ... alimleta mtumwa aitwaye Mid’am kwa Mtume wa Allah" Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 78 (Kitabu cha Viapo na Nadhiri) sura ya 33 na.698 uk.455.

"Kuuzwa kwa Mudabbar (yaani mtumwa aliyeahidiwa na bwana wake kuachiwa huru baada ya kifo cha bwanawe." (433) Jabir alisimulia: Nabii alimuuza Mudabbar (kwa niaba ya bwana wake aliyekuwa bado hai na anahitaji hela)." Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 34 (Kitabu cha Mauzo yaani Kujadiliana Juu ya Bei) sura ya112 juzuu ya 433 na kabla ya uk.238.

"Mtu wa Ansari alimfanya mtumwa wake Mudabbar na hakuwa na mali nyingine yoyote isipokuwa yeye. Nabii aliposikia hilo, alisema (kwa washiriki wake), ‘Nani anataka kumnunua (yaani mtumwa) kwa ajili yangu?’ Nu’aim bin An-Nahham alimnunua kwa Dirham mia nane." Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 79 (Kitabu cha Fidia za Viapo Visivyotimizwa) sura ya 7 na.707 uk.464.
"‘Ammar alisimulia: Nilimwona Mtume wa Mungu na mahali pale hapakuwa na mtu yoyote isipokuwa watumwa watano, wanawake wawili, na Abu Bakr (yaani hao ndio waliokuwa watu pekee waliobadili dini na kuwa Waislam kwa wakati huo)." Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 57 (Washiriki wa Nabii) sura ya 6 na.12 uk.8.

" [Ibn Az-Zubair] alimtumia [‘Aisha] watumwa kumi ambao aliwaacha huru kama fidia kwa (kutotimiza) nadhiri yake. ‘Aisha aliwaacha huru watumwa zaidi kwa lengo hilohilo mpaka aliwaachia watumwa arobaini. Alisema, ‘Ningejua ningeeleza bayana jambo la kufanya iwapo nitashindwa kutimiza nadhiri yangu nilipokuwa naiweka ili kwamba niweze kuitimiza kirahisi.’"(1)
Rejeo la chini ya ukurasa (1) linasema, "‘Aisha hakueleza bayana nini angefanya endapo angeshindwa kutimiza ahadi yake, hii ndio sababu aliwaachia huru watumwa wengi sana ili aweze kujirahisishia utoshelevu wa kiapo chake." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 56 (Maadili na Matendo Mema ya Nabii na Washiriki Wake) sura ya 2 na.708 uk.465.
"Na ‘Ata hakupenda kuwaangalia hao wajakazi waliokuwa wakiuzwa Maka isipokuwa alipokuwa anataka kuwanunua." Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 74 (Kitabu cha Kuomba Ruhusa) sura ya 2 na.246 uk.162.

Tendo la Ndoa na Watumwa na Mateka
"Je mtu anaweza kusafiri na mjakazi bila kujua kama ni mjamzito au la? Al-Hasan hakuona shida kwa mwenye mtumwa kumbusu au kumpapasa kwa mahaba mjakazi.

Ibn ‘Umar alisema, ‘Kama mjakazi afaaye kuhusiana naye kimwili ametolewa kuwa zawadi kwa mtu mwingine, au ameuzwa, au ameachwa huru, bwana wake hatakiwi kufanya naye tendo la ndoa kabla hajapata hedhi moja ili kupata uhakika wa kutokuwepo kwa mimba, na hakuna haja hiyo kwa bikira.’
‘Ata alisema, ‘Hakuna madhara yoyote kumpapasa kimahaba (1) kijakazi mjamzito bila kufanya naye tendo la ndoa. Allah alisema: ‘Isipokuwa kuwapapasa kimahaba wake zao na (mateka wanawake) ambao mikono yao ya kuume inawamiliki (kwani katika hali hii hawastahili kulaumiwa).’" Rejeo chini ya ukrasa (1) linasema, "Mjamzito na mtu mwingine, siyo bwana wake wa sasa." Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 34 (Kitabu cha Mauzo yaani Majadiliano ya Bei) sura ya 113 baada ya na.436 uk.239-240. (Sehemu hiyo hiyo ‘Ata kama hapo awali.)

"Abu Sai’id Al-Khudri alisema kuwa wakati alipokuwa amekaa na Nabii wa Allah alimwambia, ‘Oh Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tunapata mateka wanawake kama sehemu yetu ya nyara, na tunapendezwa na bei zao, una maoni gani kuhusu [tendo la ndoa la] kukatiza kujamihiana na kumwaga nje?’ Nabii alisema, ‘Je unafanya hivyo kweli? Ni vema kwako kutokufanya, Hakuna nafsi ambayo Allah ameifanya kuishi isipokuwa itakuja kuishi." Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 34 (Kitabu cha Mauzo, yaani Majadiliano ya Bei) sura ya 111 na.432 uk.237.

"Ibn Muhairiz alisimulia: Niliingia msikitini na nikamwona Abu Sa’id Al-Khudri na kukaa pembeni yake na nikamuuliza kuhusu Al-’Azl (yaani kukatiza kujaminiana). Abu Sai’id alisema, ‘Tulitoka na Mtume wa Allah kuelekea Ghazwa [vita] ya Banu Al-Mustaliq na tulipata mateka miongoni mwa mateka Waarabu na tuliwatamani wanawake na useja ukawa mgumu kwetu na tulipenda kufanya ngono ya kukatiza kujamihiana. Basi tulipokusudia kufanya ngono ya kukatiza kujamihiana, tulisema, ‘Tunawezaje kufanya ngono ya kukatiza kujamihiana kabla ya kumuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu aliyepo miongoni mwetu?’ Tulimuuliza kuhusu jambo hili na akasema, ‘Ni vema kutokufanya hivyo, kwa sababu nafsi yoyote kama iliandikwa kuishi itaishi mpaka Siku ya Kiama." Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 59 (Kitabu cha Safari za Kijeshi) sura ya 31 na.459 uk.317. Sehemu hii inasema sawa na Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 77 (Kitabu cha al-Qadr) sura ya 3 na.600 uk.391. Kwa maneno mengine, chochote kitakachokuwa kitakuwa, hivyo usizuie kwa namna isiyokuwa kawaida. Muhammad hakuwahi kukosoa kuwasumbua kingono mateka au watumwa ambao mtu anawamiliki.

‘Aisha na Zainab bint Jahsh
"Baba ya Hisham alisimulia: Khadija miaka mitatu kabla Nabii hajaondoka kwenda Madina. Alikaa huko miaka miwili hivi na kisha alimuoa ‘Aisha alipokuwa binti wa miaka sita, na aliikamilisha ndoa hiyo kwa ngono binti alipokuwa na miaka tisa." Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 58 (Matendo Mema ya Ansar) sura ya 43 na.236 uk.153. Tazama juzuu ya 5 kitabu cha 58 (Matendo Mema ya Ansar) sura ya 43 na.234 uk.152.
Zainab binti Jahsh aliolewa na mtoto wa kuasiliwa wa Muhammad, mpaka Muhammad alipotamka Sura kwamba alitakiwa kuaachana na mtoto wake na kuolewa na Muhammad. Zainab "alikuwa anajivuna kwa wake wengine wa Nabii na alikuwa akisema kuwa, ‘Allah ameniozesha (kwa Nabii) Mbinguni.’" Bukhari juzuu ya 9 kitabu cha 93 (Imani kuwa Kuna Mungu Mmoja Tu, ‘Monotheism’) sura ya 22 na.517 uk.382; pia tazama kitabu cha 93 (Imani kuwa Kuna Mungu Mmoja Tu) sura ya 22 na.516,518 uk.381-383. Kwa maneno mengine, Kurani ya kimbingu, isiyoumbwa na iishiyo milele imeelezea ndoa ya Zainab.
Uislam na Wanawake
"‘Inakuwaje mtu miongoni mwenu anampiga mke wake kama anavyopiga farasi dume halafu anamkumbatia mke huyo huyo (analala) naye?’ Na Hisham alisema, ‘Kana kwamba anampiga mtumwa wake.’"Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 73 (Kitabu cha Mienendo Myema) sura ya 43 na.68 uk.42.
"Abu Huraira alisimulia: Mtume wa Mungu alisema, ‘Watendee wanawake mema kwa sababu mwanamke aliumbwa toka kwenye ubavu, na sehemu ya mbavu iliyojikunja zaidi ni ile ya juu kwa hiyo, kama utajaribu kuinyosha itavunjika; lakini kama ukiiacha jinsi ilivyo itabaki imepinda. Kwa hiyo watendee mema wanawake.’" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 55 (Kitabu cha Manabii) sura ya 1 na.548 uk.346.

"‘Abdullah bin Qais Al-Ash’ari alisimulia: Nabii alisema, ‘Hema (huko Peponi) ni kama lulu tupu yenye kimo cha maili thelathini na kwenye kila pembe ya hilo hema muumini atakuwa na familia ambayo haionekani kwa watu wengine.’" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 (Kitabu cha Mwanzo wa Uumbaji) sura ya 7 na.466 uk.306.

Wanawake Machoni pa Sheria ya Kiislam
"Abu Sai’id Al-Khudri alisimulia: Nabii alisema, ‘Je ushahidi wa mwanamke si sawa na nusu ya ule wa mwanaume?’ Wanawake walisema, ‘Ndio.’ Alisema, ‘Hii ni kwa sababu ya upungufu wa akili za mwanamke." Bukhari juzuu ya 3 kitabu cha 48 (Kitabu cha Shahidi) sura ya 12 na.826 uk.502.
" [Muhammad] alisema, ‘Taifa linalomfanya mwanamke kuwa mtawala wake halitafanikiwa.’" Bukhari juzuu ya 9 kitabu cha 88 (Kitabu cha Mateso) sura ya 18 na.219 uk.171.
Ndoa ya Muda (Mut’a)
"‘Ali bin Abi Talib alisimulia: Siku moja ya Khaibar, Mtume wa Allah alizuia Mut’a (yaani ndoa ya muda) na kula nyama ya punda." Bukhari juzuu ya 5 kitabu cha 59 (Kitabu cha Safari za Kijeshi) sura ya 37 na.527 uk.372. Bukhari juzuu ya 7 kitabu cha 62 (Ndoa) sura ya 32 na.50, 52 uk.36, 37 pia zinajadili jambo hili. Waislam wengi isipokuwa baadhi ya Wasuni hawawi na ndoa za muda, wakati ambapo wengi wa Washia wanafundisha kuwa ni sahihi kufanya hivyo.

Mahusiano ya Kimbari (Race Relations) na Muhammud Kumiliki Watumwa Waafrika

"Anas alisimulia: Mtume alisema, ‘Msikilize na kumtii (chifu wako) hata kama ni Muethiopia ambaye kichwa chake ni kama zabibu kavu akifanywa kuwa chifu wako." Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 11 (Kitabu cha Wito wa Maombi) sura ya 54 na.662 uk.375 (pia Ibn-i-Majah juzuu ya 4 kitabu cha 24 (Kitabu cha Jihad) sura ya 39 na. 2860 uk.196) Bukhari juzuu ya 1 kitabu cha 11 (Kitabu cha Wito wa Maombi) sura ya 55 na.664 uk.376 husema vivyo hivyo.

Kama ilivyosemwa mwanzoni, Muhammad alikuwa mmiliki wa watumwa aliyekuwa na mtumwa Mwafrika angalau mmoja. (Bukhari juzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 316 na.435 uk.407, juzuu ya 9 kitabu cha 91 (Kitabu cha Habari Zilizotolewa na Mtu Mkweli) sura ya 3 na.368 uk.275) Muhammad aliuza watumwa wake Waafriaka wawili ili aweze kumwacha huru mtumwa mwingine ambaye alibadilika kuwa MuislamIbn-i-Majah juzuu ya 4 kitabu cha 24 (Kitabu cha Jihad) sura ya 41 na.2869 uk.202. Zifuatazo ni dondoo.

"Kisha nilivaa nguo zangu na kwenda nyumbani kwa Mtume wa Mungu, na tazama, alikuwa anakaa kwenye chumba chake cha juu ambako mtumwa wake Mwafrika alikuwa (anakaa) kwenye kituo cha kwanza." (Bukhari juzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 316 na.435 uk.407)

"Umar alisimulia, "Nilikuja na tazama, Mtume wa Allah alikuwa anaishi kwenye Mashroba (chumba cha barazani) na mtumwa Mwafrika wa Mtume wa Allah alikuwa juu ya ngazi zake." (Bukhari juzuu ya 9 kitabu cha 91 sura ya 3 na.368 uk.275)

Jambo hili linafurahisha kwani Muhammad alimnunua mtumwa ambaye alikuwa amebadilika kuwa Muislam (labda kwa lengo la kumfanya kuwa huru.) Badala ya kumlipa mwenye kummiliki hela taslimu, Muhammad aliwauza watumwa wake wawili Waafrika. Mbari ya mtumwa wa kwanza haijaelezwa ila kwa sababu moja au nyingine ilionekana kuwa muhimu kuandika kuwa watumwa wawili ambao Muhammad aliwauza walikuwa Waafrika, na ilibidi wawe wawili ili aweze kumnunua mtumwa mmoja.

"Jabir (Allah apendezwe naye) aliripotiwa kusema kwamba kuna mtumwa aliyekuja na kutoa kiapo cha utii kwa Nabii Mtakatifu (amani na baraka za Mungu ziwe naye) kwani uhamaji (Hijra) na Nabii Mtakatifu (amani na baraka za Mungu ziwe juu yake) hakujua kwamba alikuwa mtumwa. Kisha mmiliki wake alikuja kumtafuta na Nabii Mtakatifu (amani na baraka za Mungu ziwe juu yake) alisema, ‘Muuze kwangu.’ Hivyo alimbadilisha na watumwa wawili Waafrika. Kisha Muhammad hakupokea kiapo cha utiifu toka kwa mtu yoyote baada ya hapo, mpaka hapo mtu atakapomuuliza: Je huyu ni mtumwa?" (Ibn-i-Majahjuzuu ya 4 kitabu cha 24 (Kitabu cha Jihad) sura ya 41 na.2869 uk.202)
Hadithi za Bukhari zinapatikana kwenye mtandao wa kumpyuta katika tovuti:


Maoni kwa Wakristo

Japokuwa unaweza kujiona kuwa umebarikiwa sana kwamba huhitaji kuamini na kufanya mambo haya, usijivune. Isingekuwa neema ya Mungu, ungeweza kunaswa kwenye utumwa wa aina hiyo ambao ungekufanya ufikiri kuwa unapaswa kufanya mambo haya ili uweze kumpendeza Mungu. Marafiki Waislam wa Suni unaoweza kuwa nao wanaweza wasijue sana vitabu vyao wenyewe na wasielewe mambo haya. Waonyeshe, na waulize kama kweli wanataka kushiriki kwenye mambo haya.


Mungu anapenda tumpende; anataka mioyo yetu na akili zetu pamoja na mwenendo wetu na matendo yetu. Hapendi tuamini tiba zisizo safi za kutumia nzi, au matendo yasiyo safi kwa mateka na wajakazi. Mungu anapenda tufuate mambo aliyotufundisha katika Neno lake, Biblia, na Yesu, ambaye alikuwa zaidi ya nabii, bali Isaya alimwita Emmanuel (Mungu pamoja nasi).

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW