Wednesday, July 1, 2015

Unajimu na Kurani

 Baadhi ya Waislam wanasema Kurani ina ukweli wa kisayansi kuhusu mizunguko ya jua, mwezi, (na nyakati nyingine sayari). Ninapenda kuchunguza jambo hili, na tutazunguka pande tofauti tofauti kabla ya kufikia uamuzi. Lakini jambo la msingi ni kuwa: isipokuwa Muislam awe ameziona hizi aya kama misemo ya kufananisha, aya hizi hazitakubali, hazithibitishi usahihi wa kisayansi wa Kurani. 
 
Sura 36:37-40 inasema, "Na ishara yao ni usiku: Tulijitoa pale toka mchana, na tazama wakazamishwa kwenye giza; 38 na jua linafuata mkondo wake wa kawaida kwa muda liliopangiwa; hii ni amri yake (yeye), aliyeinuliwa kwenye nguvu, yeye ajuaye vyote. 39 Na mwezi-tumeupimia majumba makubwa (kupita toka upande mmoja hadi mwingine) hadi unabadilika kuwa kama sehemu ya chini ya kikonyo cha mtende kilichozeeka (na kunyauka). 40 Jua haliruhusiwi kuukuta mwezi na usiku hauwezi kwenda haraka hata kuupita mchana: Kila kimoja huelea tu kwenye mkondo wake wenyewe (kwa mujibu wa sheria)." (Tafsiri ya Yusuf Ali, toleo la kwanza) [Maneno yaliyo kwenye mabano yamo katika mabano kwenye tafsiri.]
 
Baadhi ya Waislam wanasema kuwa "jua hufuata njia yake kwa muda ambao limepangiwa" na neno "mkondo" likiwa limewekwa mwishoni. Hata hivyo, hatuwezi kusema vitu vingi sana kuhusu "mkondo" wa jua kwa sababu tafsiri ya Yusuf Ali ina rejeo (la 17) chini ya ukurasa linalohusiana na neno hili likisema "mzunguko, njia." Pia, toleo la Yusuf Ali lililofanyiwa marekebisho linasema "mahali pa kupumzika" badala ya "kipindi."
 
Ni kwa Jinsi Gani Baadhi ya Waislam Huitafsiri Kurani kwa Uhuru?
Tovuti ya Wasufi http://www.sufi.co.za/modern_science_and_islam.htm hupita kiwango ikisema
"Vitu hivi vyote dunia, mwezi na sayari zote na wakati wote hutembea kwenye mikondo (au mihimili) yake ni matufe yaeleayo" (Ansari)
Inaongeza maneno "(vyote hivi ni sayari)" na "(au mihimili yake)" kwenye mabano, kwa sababu hayamo kabisa kwenye Kiarabu. Hebu tuliache hili kwa kuwa ni tafsiri isiyo sahihi, na tujiulize "Sura 36:37-40 inafundisha nini hasa?" Inaweza kuwa moja ya vitu hivi vitatu:
  
Mikondo ya jua na mwezi:
 Kurani inafundisha kuwa jua na mwezi vilienda bila kupumzika kwenye njia/mikondo vikiizunguka dunia kwa kipindi maalum kilichopangwa.
  
Kuogelea kuelekea sehemu linaposimama:
 Jua huogelea kwenye mawingu wakati wa mchana, na huelekea sehemu linapopumzika usiku, na kurudi mahali pake lilipokuwa asubuhi iliyotangulia. Vivyo hivyo mwezi huogelea kwenye njia yake.
  
Misemo ya kufananisha:
 Kama sehemu iliyotangulia, ila hili limekusudiwa kama maelezo ya jinsi vitu vinavyoonekana kuwa, si jinsi vilivyo hasa. 

 

Hebu Turudi kwenye Kiarabu
Njia/Mkondo: Yusuf Ali anaelezea neno la Kiarabu linalojadiliwa kwenye rejeo la 3983 chini ya uk.1326. Ali anasema, "Mustaqarr linaweza kumaanisha: (1) kikomo cha muda, kipindi kilichopangwa kabla, kama kwenye vi. 67, au (2) mahali pa kupumzikia au utulivu; au (3) mahali pa kuishi, kama kwenye ii. 36. Nafikiri maana ya kwanza ndio yenye kufaa zaidi hapa; lakini wafafanuzi wengine wanapendelea maana ya pili. Katika hali hiyo ulinganisho utakuwa kati ya jua linaloshindana mbio wakati linaonekana kwetu, na kupumzika wakati wa usiku ili kujiandaa kuanza upya mbio zake siku inayofuata. Kukaa kwake pamoja na upande wa pili wa dunia kunaonekana kwetu kama kipindi cha mapumziko."
  
Kutembea/kuogelea/kuzunguka: 
yasbahuna inaweza kumaanisha kuharakisha, ingawa maana yake ya moja kwa moja zaidi ni kuogelea.
  
Ogelea/zunguka:
 Mtoa maoni maarufu wa Kiislam Ibn Taymiyah (aliyekufa mwaka 1328 BK) aliandika, "jua, nyota na sayari zina umbo la duara (istidaaratul-aflaak) – kama ulivyo usemi wa wanajimu na wataalam wa hesabu (ahlul-hay’ah wal-hisab)..... [Neno] falak [kwenye lugha ya Kiarabu] linamaanisha kitu cha duara" (Majmu’ul-Fatawa juzuu ya 6, uk. 566-567).
 
Si "muujiza wa kisayansi" kwamba jua na mwezi ni "falak" kwa sababu
a) Neno ‘dunia kulizungika jua’ kwa Kiarabu si falak bali mahrek.
b) Neno falak halikutoka kwenye Kurani; lilikuwa ni neno lililochukuliwa toka lugha ya kigeni.
 
Mtu mmoja alichangia yafuatayo: "Asili [ya Kiarabu -- falaka] … toka kwenye chanzo kimoja cha kale cha Kisemiti tunapata [Kiakadia -- pilakku]; [Kiebrania -- pelek]; [Kiarabu -- falkatun], yote yakimaanisha mduara wenye kwenda kwa haraka, na chimbuko lingine la tofauti [la Kiarabu -- falakun]; [Kiethiopia -- falaka] likimaanisha nusu nyingine ya mbingu. Kwa hiyo wataalam wa maneno wamekuwa na desturi ya kutafuta kuhusisha [neno la Kiarabu -- falkun] na chanzo hiki, wakifikiri kuwa limeitwa hivyo tokana na umbo lake la duara."
 
Pia, neno falak lilitumiwa na Waarabu, kabla ya Muhammad kuzaliwa likimaanisha kuelea kwa jua, nyota na sayari kwenye "dari la anga la duara (kuba)." Watu walioishi kabla, na wakati wa Muhammad waliamini kuwa ulimwengu una mfano wa Kiaristote/Kiptolem ambamo dunia ipo katikati ikiwa imezungukwa na dari 7 za duara (kuba). Na jua, nyota na sayari ziliaminiwa kuwa zinazunguka kwenye miduara, au midura yenyewe iliaminiwa kuwa inazunguka kwenye njia moja. Kwa kuwa Kurani inasema kuwa kuna mbingu saba inaonyesha mtazamo wa Muhammad kuhusu "mfumo wa unajimu" unafanana na mfano wa Ptolem na Aristote, ambayo iliaminiwa kuwa ni kweli katika kipindi hicho cha historia.
  
Maoni yangu (kwa sasa):
 Ingawa neno la Kiarabu haliko bayana kabisa, maneno haya hayaelezi kitu chochote ambacho watu wa kale kabla ya Muhammad kuzaliwa hawakuwa wameishasema.
 
Hata hivyo, kama tukidhani kuwa Muhammad na wafuasi wake wa kwanza hawakuielewa Kurani (wazo salama kabisa), na kwamba maoni ya kisayansi ya Kurani ni thabiti, tuna njia mbili za kufika kwenye uamuzi unaofaa. Kwanza, Waislam wa mwanzo walisema nini kuhusiana na jambo hili, na pili, sehemu iliyobaki ya Kurani inasema nini.
 
Muhammad na Waislam wa Mwanzo Walisema Nini kuhusu Jua?
Utakwenda wapi kutafuta maana sahihi ya Kurani? Zamakhshari? al-Tabari? Baidawi? Kama ungekuwa Muislam wa mwanzo ungeweza kwenda kwa Muhammad mwenyewe! Sikia jinsi Muhammad alivyoeleza, kwa mujibu wa Bukhari na al-Tabari. 
  

"Abu Dhar alisimulia: Nabii aliniuliza wakati wa machweo ya jua, ‘Unafahamu mahali ambako jua linakwenda (wakati wa kuchwa)?’ Nilijibu, ‘Allah na Mtume wake wanafahamu vizuri zaidi.’ Alisema, ‘Linakwenda (yaani linasafiri) hadi linasujudu chini ya kiti cha enzi, na linapata kibali cha kusimama tena, na linaruhusiwa na kisha (muda utakuja ambapo) litakuwa linakaribia kusujudu lakini kusujudu kwake hakutakubaliwa …’" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 4 na.441 uk.283. 
  

Tafsiri nyingine ya kifungu hicho hicho cha al-Bukhari inasema:

"Abzur Ghifari (ra) alisimulia: siku moja Nabii Muhammad (amani na iwe juu yake) aliniuliza, ‘Abzar unafahamu jua linakwenda wapi baada ya kuzama?’ Nilimjibu, ‘Sifahamu, Mtume wa Allah ndiye yeye tu anayeweza kusema vizuri zaidi.’ Kish Nabii (SA) alinijibu, ‘Baada ya kuzama, jua hubaki likisujudu chini ya Aro’sh (kiti cha enzi cha Allah) na linasubiri amri ya Allah ili lichomoze tena upande wa mashariki. Siku itakuja wakati ambapo jua halitapata ruhusa zaidi toka kwa Allah ya kuchomoza tena na Qeyamot (Siku ya Kiyama) itakuja duniani.’"
  
al-Tabari
 juzuu ya 1 uk.231 inasema, "Nilimuuliza Mjumbe wa Mungu [Muhammad] ‘[Jua] linazama wapi?’ Alinijibu: ‘Linazama mbinguni na kisha linachomoza kutoka mbingu kwenda mbingu nyingine hadi linachomoza kwenye mbingu ya juu zaidi, mbingu ya saba. Hatimaye, linapokuwa chini ya kiti cha enzi, linaanguka chini na kusujudu, na malaika wanaolisimamia wanasujudu pamoja nalo. Kisha jua linasema, Bwana wangu, ni wapi unakoniamuru nichomozee, ni upande ule nilikozamia au nilikochomozea?’ Aliendelea. Jambo hili ndilo (linalokusudiwa na) neno la Mungu: ‘Na jua: Hukimbilia mahali linapotakiwa kuwepo (usiku)’ linaposhikiliwa chini ya kiti cha enzi – ‘Jambo hilo limeamriwa na Yeye Mwenye Nguvu na Mwenye Kujua’ Bwana kwa mamlaka yake ya kifalme, Bwana ambaye ‘anavijua’ viumbe vyake. Aliendelea, Gabriel alileta kwenye jua vazi lenye kung’aa tokana na mwanga utokao kwenye kiti cha enzi, kwa kufuata vipimo vya saa na siku. Ni refu zaidi wakati wa majira ya joto na fupi zaidi wakati wa majira ya baridi, na lenye urefu wa wastani wakati wa majira ya kupukutisha majani na wakati wa majira ya kuchipua majani. [Mitindo ya majira ya kuchipua majani, kupukutisha majani na majira ya baridi!] Aliendelea. Jua huvaa vazi hio, kama mmoja wenu anavyovaa zavi lake. Kisha, huwa huru kuzunguka kwenye anga la mbinguni mpaka linapochomoza kutokea upande linaochomozea. … Njia hiyo hiyo hufuatwa na mwezi wakati wa kuchomoza kwake … Lakini Gabriel huuletea vazi kutoka kwenye mwanga wa miguunil. Hivi ndivyo neno la Mungu (linavyomaanisha) ‘Amelifanya jua kuwa angavu na mwezi kuwa mwanga.’"
 
Jua na mwezi ni alama za Allah. Abu Dawud juzuu ya 1 kitabu cha 2 na.1173 uk.304; 
Sunan Nasa’i
 juzuu ya 2 na.1462,1464 uk.272; juzuu ya 2 na.1465, 1466 uk.273; juzuu ya 2 na.1475 uk.278; juzuu ya 2 na.1477 uk.280; juzuu ya 2 na.1481 uk.283; juzuu ya 2 na.1485-1486 uk.286-287; juzuu ya 2 na.1488-1489 uk.287,289; juzuu ya 2 na.1500 uk.297; juzuu ya 2 na.1502 uk.299; juzuu ya 2 na.1505 uk.300; juzuu ya 2 na.1506 uk.301.
 
Dhu al-Qarnaiyn [Zul Qarnain] "alishuhudia kuzama kwa jua kwenye sehemu yake ya kupumzikia kwenye bwawa lenye ute mweusi na wenye harufu mbaya sana." al-Tabari juzuu ya 5 uk.173-174 (Tazama Sura 18:82-97).
  
al-Tabari
 juzuu ya 1 uk.234 pia inasema kuwa jua huzama kwenye chemchemi yenye matope. Msemo "yenye matope" ni hami’ah, unaomaanisha udongo mweusi wa mfinyanzi, lakini hamiyah ni neno lenye kufanana nalo linaloweza kumaanisha kitu cha moto. (Tazama rejeo la 442 chini ya uk.234).
 
" [Muhammad] Aliendelea. Wakati jua linachomoza, linainuka juu ya kibandawazi (kinachokokotwa na farasi) toka kwenye moja ya chemchemi hizo likiwa pamoja na malaika 360 …. Wakati Mungu anataka kuvijaribu jua na mwezi, ili kuwaonyesha watumishi wake ishara na kwa njia hiyo kuwataka waache kutokumtii Yeye na kuanza kutii, jua huporomoka ghafla toka kwenye kibandawazi na kuanguka kwenye kina cha bahari, ambacho ni cha mduara. Wakati Mungu anataka kuongeza umuhimu wa ishara kuwatisha zaidi watumishi wake, jua lote hunguka, na hapawi na sehemu yake yoyote inayobaki kwenye kibandawazi. Huko ndiko kupatwa kukamilifu kwa jua, wakati ambapo mchana hujiwa na giza na nyota hutokeza." al-Tabari juzuu ya1 uk.236.
 
Je Muhammad na Waislam wa Mwanzo Wanatuambia Nini kuhusu Mbingu?
Nabii [Muhammad] alijibu: ‘Ali, kuna nyota tano: Jupiter (al-birjis), Saturn (zuhal), Zebaki (utarid), Mars (Bahram), na Venus (al-zuhrah). Nyota hizi tano huinuka na kukimbia kama jua na mwezi na hushindana nazo pamoja. Nyota nyingine zote zimening’inizwa toka mbinguni kama taa zilivyoning’inizwa toka kwenye misikiti…" al-Tabari juzuu ya 1 uk.235-236.
 
"Mungu aliiumba bahari fasrakh tatu (kilomita 18) kutoka mbinguni. Mawimbi yamedhibitiwa, yanasimama angani kwa amri ya Mungu. Hakuna tone hata moja linalomwagika. Bahari zote hazitembei, lakini bahari hutiririka kwa kiwango cha mwendokasi wa mshale. Imeachwa kutembea angani kwa ulinganifu, kana kwamba ni kamba ilinayotokeza kwenye eneo kati ya mashariki na magharibi. Jua, mwezi, na nyota zenye kurudi nyuma [sayari 5] huzunguka kwenye kina cha mawimbi ya bahari. Hivi ndivyo neno la Mungu (linavyomaanisha): ‘Kila moja huogelea kwenye mduara.’ ‘Mduara’ ni mzunguko wa kibandawazi kwenye kina cha mawimbi ya ile bahari." al-Tabari juzuu ya 1 uk.235.
  
Maoni kutoka kwa Waislam wa mwanzo:
 Jua huenda hasa kwenye sehemu ya kupumzika wakati wa usiku, na kwamba jua na mwezi "huelea" hasa kwenye bahari yenye maji angani.
 
Sehemu Nyingine za Kurani Zinasema Nini?
Elewa kuwa namba za aya zinatofautiana kwenye matoleo tofauti ya Kurani. Namba hizi za aya zifuatazo zimetolewa kwenye (toloe lililorekebishwa la) Yusuf ‘Ali. Nimesahihisha matumizi ya herufi kubwa.
  
Sura 20:53
 "Yeye aliyeiumba dunia kwa ajili yako kama zulia ameisambaza"
  
Sura 50:7
 "Na dunia – tumeisambaza4946, na tumeweka milima juu yake …"
Rejeo la Yusuf ‘Ali la 4946 chini ya ukurasa linasema, "Linganisha xiii. 3; na xv. 19 na rejeo la 1955. Dunia ni ya mviringo, lakini inaonekana kuwa imenyooka kama eneo kubwa la wazi, kama zulia lililoshikiliwa imara na uzito wa milima." Hivyo ikiwa unaamini kuwa jambo hili linadai kuwa dunia ni tambarare au la, Yusuf ‘Ali anasema kuwa aya hii inasema kuwa dunia inaonekana kuwa kama zulia tambarare.
  
Sura 67:15
 "Ni Yeye aliyeifanya dunia iweze kuthibitiwa5571…" Tafsiri nyingine zinatumia neno "usawa." Rejeo la 5571 la Yusuf Ali chini ya ukurasa linasema, "Zalul inatumiwa kwenye ii.71 kwa mnyama aliyefunzwa na anayeweza kuthibitiwa: hapa linatumika kuielezea dunia, na nimelitafsiri kama ‘inayoweza kuthibitiwa’…."
  
Sura 71:15
 "‘Je hamuoni jinsi Allah alivyoumba mbingu saba moja juu ya nyingine ‘Na aliumba mwezi uwe mwanga kati yao, na aliumba jua liwe taa ing’aayo?" Hata kama ikichuliwa kuwa hii ni lugha ya kufananisha, hakuna kitu chochote chenye kuashiria mafundisho ya kisasa ya unajimu.
  
Sura 71:19
 "‘Na Allah aliiumba dunia kwa ajili yako kama zulia (lililosambazwa),5718…" Rejeo la 5718 la Yusuf ‘Ali chini ya ukurasa linasema, "linganisha xx 53.
  
Sura 78:6-7
 "Sisi [Allah] je hatujaumba dunia pana kama eneo kubwa wazi5890, na milima kama vigingi?" Rejeo la 5890 la Yusuf ‘Ali chini ya ukurasa linasema, Tazama rejeo la 2038 hadi xvi. 15. Linganisha pia xiii. 3 na xv. 19. Eneo kubwa wazi lenye nafasi pana linaweza kulinganishwa na zulia, ambalo milima ni kama vigingi …."
 
Zul-Karnain kwenye Sura ya 18 na Sayansi ya Unajimu
Sura 18:85-86 "Njia (mojawapo) ambayo [Zul-qarnain] aliifuata, hadi, wakati alipofika machweo ya jua, alikuta linazama kwenye chemchemi ya maji meusi na machafu: karibu na sehemu hiyo aliwakuta watu: Sisi [Allah] alisema: ‘Oh Zul-qarnain! (Wewe unayo mamlaka) ama kuwaadhibu ama kuwatendea wema." Neno "Murky" limetafsiriwa pia kama chemchemi ya maji "nyeusi" na yenye "udongo." Msemo "chemchemi ya . . . maji" pia imetafsiriwa kama "chemchemi.". M. H. Skahir ameitafsiri kuwa "bahari nyeusi."
  
Sura 18:89-90
 "Kisha [Zul-qarnain] aliifuata njia (nyingine), hadi alipofika kwenye mawio ya jua, alilikuta likichomoza juu ya watu ambao hatukuwapa kitu chochote cha kujikinga dhidi ya jua."
 
Watoa maelezo wa Kiislam wanatofautiana juu ya Zul-qarnain (mtu wa pembe mbili) kuwa ni nani hasa. Wengine wanafikiri kuwa ni Alexander Mkuu, wengine wanafikiri ni Cyrus wa Uajemi, na wengine wanafikiri kuwa ni mfalme wa Yemeni. Hata hivyo haijalishi. Vyovyote itakavyokuwa, Zul-qarnain aliweza kwenda mahali halisi ambako jua linachomozea. Jambo hili linathibitisha maoni ya Kurani kuwa dunia ina umbo bapa. Kitu muhimu zaidi ni kuwa alikwenda mahali jua linapozamia, na akakuta kuwa linazama kwenye chemchemi nyeusi na yenye matope.
 
Ukiwauliza wanajimu endapo jua linazama kwenye chemchemi yenye matope watakwambia "hapana.’
  
Hitimisho:
 Kurani inafundisha mambo yafuatayo:
Dunia ina umbo bapa, imeenea kama zulia na imefungwa kuwa bapa kwa vigingi ambavyo ni milima
Dunia ina njia yake ambayo imewekewa mipaka wakati wa mchana, kisha huzama kwenye chemchemi nyeusi na yenye matope wakati wa usiku na huenda kwenye kiti cha enzi cha Allah.
Baadaye jua huchomoza kutoka kwenye sehemu moja maalum
Ukiachia nyota (sayari) tano "zenye kwenda nyuma", nyota zimening’inizwa kama taa
Muhammad aliwafundisha Waislam wa mwanzo jambo hili kama ukweli halisi, siyo sitiari au mlinganisho.
 
Madhumuni ya Nyota na Vimondo
"Mbingu za chini kabisa zina taa [nyota], na ‘Tumeziumba (taa) hizi kama makombora ya kuwafukuzia waovu, na tumetayarisha Adhabu ya Moto Uwakao kwa ajili yao.’" Sura 67:5.
 
"Kuumbwa kwa nyota hizi kuna madhumuni matatu, yaani, kulipamba anga, makombora ya kuyapiga mashetani,na alama za kuwaongoza wasafiri. Kwa hiyo kama mtu yoyote anajaribu kupata tafsiri nyingine amekosea na anapoteza nguvu zake tu..." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 3 kabla na.421, uk.282.
 
Wakati mwingine vimondo hurushwa kwa mashetani ambao wanajaribu kusikiliza siri za mbinguni. Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 4 na.902 na rejeo la 674 chini ya uk.243.
 
Vimondo vinapaswa kuwapiga malaika [wabaya] kabla hawajaeneza mambo walyoyasikia. Wakati mwingine malaika wabaya huwaambia watabiri kabla ya kuwapiga. Ibn-i-Majah juzuu ya 1 kitabu cha 1 na.194, uk.110.
 
Vimondo huyashambulia majini (genies) Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 24 na.5538, uk.1210.
 
Nyota hulinda dhidi ya shetani. al-Tabari juzuu ya 1, uk.223.
 
Muhammad Anaupasua Mwezi Vipande Viwili
"Hitaji la wapagani kwa Nabii kuwa awaonyeshe miujiza. Nabii aliwaonyesha kupasuka kwa mwezi. ‘Abdullah bin Massud alisimulia: Wakati wa maisha ya Nabii mwezi ulipasuliwa vipande viwili na Nabii alisema kuhusiana na hilo, ‘Shuhudia (jambo hili).’" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 56 sura ya 26 na juzuu ya 4 kitabu cha 56 sura ya 26 na.830, uk.533.
 
"Anas alisimulia kwamba watu wa Maka walimwomba Mtume wa Allah awaonyeshe muujiza, na kwa ajili hiyo aliwaonyesha mwezi unaopasuka." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 56 sura ya 26 na.831, uk.533.
 
"Ibn ‘Abbas alisimulia: Mwezi ulipasuliwa vipande viwili wakti wa uhai wa Nabii." Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 56 sura ya 26 na.832, uk.534.
 
Mwezi unaopasuka. Bukhari juzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 225 na.290, uk.273 na rejeo la 1 chini ya uk.273; juzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 287 na.387-391, uk.365-366; juzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 261 na.345, 349, uk.331; Bukharijuzuu ya 6 kitabu cha 60 sura ya 265 na.368-370, uk.331, 336.
 
Kuupasua mwezi Sahih Muslim juzuu ya 4 kitabu cha 37 na.6721, 6724-6730, uk.1467-1468.
 
Sura 54:1 inasema, "Saa (ya hukumu) imekaribia, na mwezi ulipasuliwa vipande viwili. (toleo lililorekebishwa la Yusuf ‘Ali).
 
Tambua kuwa kupasuliwa vipande viwili kunamaanisha kuwa mwezi uligawanywa nusu kwa nusu, na kitenzi kilichotumika hapa ni cha wakati uliopita. Hatuna kumbukumbu za watu wengine wowote ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na jirani zao wa Misri, Syria, au Uajemi ambao waliuona mwezi uliopasuliwa vipande viwili. Kurani na hadithi hazisemi ni jinsi gani mwezi uliweza kurudi kuwa kitu kimoja tena.
 
Yusuf ‘Ali, kwenye rejeo la 5128 chini ya ukurasa, anasema, "Maelezo matatu yametolewa kwenye Mufradat, na pengine yote matatu yanahusika hapa: (1) kwamba mwezi ulionekana ukiwa umepasuka vipande viwili kwenye bonde la Maka machoni pa Nabii, washirika wake, na baadhi ya watu wasiokuwa waumini; (2) kwamba wakati uliopita wa kinabii huonyesha wakati ujao, kupasuka kwa mwezi vipande viwili ikiwa ni Ishara ya Hukumu inayokuja; na (3) kwamba msemo huu ni sitiari, ukimaanisha kuwa jambo hili liko wazi kama mwezi. Kwamba kupasuka kwa mara ya kwanza kulionekana na watu wasiokuwa waumini ni dhahiri kwenye aya ya 2. Kupasuka kwa mara ya pili litakuwa ni kuvunjwa kwa mfumo wa jua kwenye Uumbaji Mpya: Linganisha lxxv. 8-9."
Mifano Inayoenda Kinyume kwenye Kurani?
Hebu na tuziache aya zilizotangulia na tuangalie aya nyingine kwenye Kurani ambazo baadhi ya Waislam wanaamini kuwa zinaunga mkono kanuni za kisasa za unajimu. Ili kuwatendea haki, zifuatazo ni aya ambazo wanazitumia, pamoja na maitikio yake.
  
Sura 7:54
 "…Huuvuta usiku kama mtandio juu ya mchana, kila mmoja akiwa anamtafuta mwingine kwa mfuatano wa haraka..." 
Itikio:
 ni kweli kwamba usiku na mchana vinafuatana, lakini jambo hili halisemi kitu chochote kuhusu sayansi au unajimu ambacho watu wa zamani hawakukifahamu.
  
Sura 13:2
a na Sura 31:10 zinasema kuwa Allah aliziinua mbingu bila nguzo zozote unazoweza kuziona." 
Itikio:
 Ingawa si watu wote wa kale walioamini kuwa mbingu zilikuwa zimeshikiliwa na nguzo, jambo hilo linaeleza tu kuwa Mungu hakuwa na nguzo zozote zenye kuonekana zinazoweza kuonekana.
  
Sura 13:2b
 "…Amevitiisha jua na mwezi! Kila kimojawacho kutembea (kwenye njia yake) kwa muhula kilichopangiwa" 
Itikio:
 Kwamba jua na mwezi vina utaratibu ni jambo lililojulikana hata kwa watu wa kale.
  
Sura 21:30
 "Je watu wasioamini hawaoni kuwa mbingu na nchi ziliungwa pamoja (kama Kitu Kimoja Kilichoumbwa) kabla sisi [Allah] hatujavigawa vipande viwili?" Waislam wanaona jambo hili kuwa ni matarajio ya Kurani ya nadharia ya mlipuko mkubwa uliyoifanya dunia iumbwe, yaani, ‘the big bang theory.’ 
Itikio:
 Wamisri wa kale, Wahindu wa Arya, na watu wengine waliamini kuwa mbingu na dunia vilikuwa pamoja hazijagawanywa. Kusema tu kuwa mbingu na dunia ziliungwa pamoja (kwa maana ya kuwa nusu mbili) ni kama hadithi za kubuniwa za kale na si nadharia ya mlipuko mkubwa ulioifanya dunia iumbwe.
  
Sura 21:33
 "Vyote (jua, mwezi, nyota na sayari) huelea juu ya, kila kimoja kwenye mkondo wake2695 wa duara. Rejeo la 2695 la Yusuf Ali lililo chini ya ukurasa lina maelezo mazuri hapa. Linasema, "Nimeonyesha, tofauti na wengi wa wafasiri, sitiari ya kuogelea iliyodokezwa kwenye maneno ya asili…"
Tafsiri ya Malik inasema, "vyote (jua, mwezi, nyota na sayari) hutembea kwa haraka sana kwenye mihimili yao yenyewe." 
Itikio:
 Neno la Kiarabu lilifahamika kuwa "kuogelea" kama Yusuf Ali alivyolitafsiri kiusahihi, kama ilivyoonyeshwa na al-Tabari juzuu ya 1, uk.235; al-Tabari juzuu ya 1, uk.236. Aya hizi pia zinazungumzia jua na mwezi, siyo sayari na nyota, kwa hiyo si sahihi kabisa kuviweka (jua, mwezi, nyota na sayari) kwenye mabano kwenye tafsiri. Kurani haisemi kuwa kitu chochote hutembea kwenye njia/mhimili wake angani isipokuwa jua, mwezi na sayari zenye kurudi nyuma (sayari).
  
Sura 21:104
 "Siku ambayo tunaziviringisha mbingu kama hati ya kukunja." 
Itikio:
 Haieleweki kwangu ni kwa jinsi gani jambo hili linadhaniwa kuwa linatarajia unajimu wa kisasa, lakini mke wa kwanza wa Muhammad alielewa kuwa alisikia injili toka kwa mkristo mmoja, na Biblia, kwenye Ufunuo 6:14 na Agano la Kale kwenye Isaya 34:4. Hata hivyo, Wakristo, kwa jumla, hawafanyi juhudi ya kujaribu kuufanya unajimu wa kisasa ufanane na Ufunuo 6:14.
  
Sura 22:65
 "…Hulishikilia anga2847 lisianguke duniani isipokuwa kwa jani lake …" Rejeo la Yusuf ‘Ali la 2847 chini ya ukurasa linasema kuwa neno hili samaa linaweza kumaanisha (1) kitu kilicho juu, (2) mzizi, dari, (3) anga, mbingu, (4) mawingu au mvua. Anasema kuwa anaelewa maana ya mwisho hapa, ingawa mamlaka nyingi zinaelekea kulitafsiri kwa maneno kama "anga." 
Itikio:
 Hivyo basi kwa mamlaka nyingi neno litakuwa "anga" ambalo linaendana sawa na maoni kuwa dunia ni tambarare. Kwa hiyo ingawa hatuwezi kusema kuwa aya hii inathibitisha kabisa maoni ya Kurani ya dunia tambarare, tokana na maana ya Kiarabu kutokuwa bayana kabisa, aya hii haiwezi kutumika kuthibitisha maoni ya Kurani ya sayansi ya kisasa.
  
Sura 25:61-62
 "Amebarikiwa Yeye aliyeumba makundi ya nyota angani, na kuyaweka kwenye taa na mwezi ili yatoe mwanga. Na ni yeye aliyevifanya usiku na mchana vifuatane…" 
Itikio:
 Kuliita jua taa hakusaidii kuthibitisha kuwa Kurani ina maoni ya kisayansi ya kisasa. Kwamba mchana na usiku vinafuatana ni kweli, lakini hili ni jambo lililojulikana hata na watu wa kale.
  
Sura 27:88
 "…milima hii unayoiona na kudhani kuwa imejishikilia imara, itapita kama mawingu …" (Malik) Mtetezi mmojawapo wa Kiislam ametokea kuamini kuwa jambo hili linadokeza mzunguko wa dunia. 
Itikio:
 Aya inayotangulia inalitaja tarumbeta la mwisho, kwa hiyo muktadha huu ni wa nyakati za mwisho, siyo leo.
  
Sura 29:44
 inasema kuwa kuumbwa kwa mbingu na dunia ni ishara ya kwa wanaoamini. 
Itikio:
 Kuumbwa kwa mbingu na dunia kunaonyesha ukuu wa enzi wa Mungu kwa mujibu wa Zaburi 8:1, 3, 5; Zaburi 19:1-6. Muahammad alizijua Zaburi (zubur) za Daudi, hivyo hakuna jambo jipya hapa.
  
Sura 31:29,
 Sura 35:13Sura 36:37, na Sura 39:5 zote zinasema kuwa Allah aliuunganisha usiku kuwa mchana na mchana kuwa usiku. Pia zinasema kuwa jua na mwezi kila kimoja huzunguka kwenye njia zao zilizoamriwa. Sura 55:5 pia inasema kuwa jua na mwezi huzunguka kwenye njia zao zilizoamriwa. 
Itikio:
 Hakuna kitu chenye kuonysha kuwa hii siyo njia ya jua na mwezi angani. Mambo haya yalifahamika na kuchunguzwa na watu wa kale, hata watu wasiojua vitu vingi. Kuusema ukweli ambao hata wapagani waliisha kuuamini haithibitishi kuwa kitabu si sahihi. Hata hivyo, kurudia mambo ambayo yanajulikana na watu wote hakuthibitshi kuwa Kurani ilitabiri ufahamu wa sayansi ya kisasa.
  
Sura 51:47,48
 "Tumejenga mbingu kwa uwezo: na hakika tunazo nguvu kubwa. Na tumeitandaza dunia (pana sana): Ni kwa uzuri gani tunaenea!" (Yusuf ‘Ali). Tafsiri nyingine zinasema "kama zulia." 
Itikio:
 Kuitandaza dunia, jambo ambalo wengine wanaliona kama kufundisha kuwa dunia ni tambarare, hakusaidii kuthibitisha kuwa Kurani inafundisha kanuni za kisayansi za kisasa. Kama mtu asiyekuwa Muislam, niko tayari kukiri kuwa jambo hili linaweza kuwa halifundishi uongo kuwa dunia ni tambarare, lakini ni njia ya kueleza kishairi. Waislam wamelitumia jambo hili kusema kuwa Kurani imefundisha nadhaaria ya mlipuko mkubwa ulioleta kupanuka kwa ulimwengu. Ukweli kuwa Mungu alizitandaza mbingu hauongelei kidhahiri nadharia ya mlipuko mkubwa ulioifanya dunia iumbwe, na kwamba Mungu alizitandaza mbingu imo kwenye Biblia, Isaya 42:5. Lakini Wakristo hawatumii maelezo hayo yasiyokuwa bayana kuthibitisha kutarajiwa kwa nadharia ya mlipuko mkubwa ulioleta kuumbwa kwa dunia.
  
Sura 55:33
 inazitaja kanda za dunia ambazo watu na majini [genies] hawawezi kuingia bila kibali. 
Itikio:
 Kanda za dunia hazitufundishi jiografia ya kisasa, ingawa inaonekana kama jinamizi la baharini au vizuizi vingine vinavyowazuia watu kusafiri kwenda baadhi ya sehemu za dunia. Kwa jinsi hiyohiyo, kanda za mbinguni hazina umuhimu mkubwa sana, isipokuwa kwamba Muhammad na tamaduni za Kiyahudi zinaongelea kuhusu mbingu ya saba.
  
Sura 71:15-16
 "Je huoni jinsi Mungu alivyoumba mbingu saba moja juu ya nyingine, Na ameuumba mwezi uwe mwanga katikati yake, na amelifanya jua kuwa (Ng’aavu) kama taa?" Inadaiwa na baadhi ya Waislam kwamba safu saba za anga la dunia (troposphere, stratosphere, n.k.) ndizo mbingu saba. 
Itikio:
 Licha ya mbingu saba kufanana katika na tamaduni ya Kiyahhudi, kuuita mwezi kuwa mwanga na jua taa hakuonyeshi maoni ya sayansi ya kisasa, ingawa jambo hili haliwezi kuthibitishwa kuwa uongo endapo litachukuliwa kuwa ni lugha ya kishairi. Pia, kama mbingu saba ndio safu saba za anga la dunia, itakuwa ni makosa kusema kuwa jua, mwezi, na nyota zipo mbinguni.
 
Kama wazo la ziada, ingawa Biblia haijazungumzia mbingu saba, tamaduni kadhaa za Kiyahudi zinazohusiana na Biblia lakini si sehemu ya Maandiko Matakatifu (Apocrypha) zinazungumzia mbinug saba: 2 Enoch 20:1; 20:1; Martyrdom and Ascension of Isaiah 7:8; 9:1,6; 10:17; The Testament of the Twelve Patriarchs sura ya 3.3. Na 3 Baruch 11:1 inazungumzia mbingu tano, ingawa haisemi kuwa hizo ndizo mbingu pekee zilizopo. Kwa hiyo hata kama ungekuwa ni muujiza wa kisayansi kwamba mbingu saba alizozizungumzia Muhammad ndizo safu saba za anga la dunia, ingekuwa ni muujiza mkubwa zaidi kwa vitabu vya kale zaidi kwani navyo vilizungumzia mbingu saba.
  
Sura 86:1-3
 "Kwa mbingu na kwa mgeni mashuhuri wa usiku, na kitu gani kitakuelezea kuwa mgeni mashuhuri wa usiku ni nini? Ni nyota yenye kung’aa kwa ajabu. (Kama ambavyo Allah Mwenye nguvu anavyochunga kila nyota kwenye kundi lao, kwa namna hiyo hiyo) kuna malaika mlinzi aliyewekwa juu ya kila nafsi." (Malik)
Baadhi ya Waislam wanadai kuwa jambo hili linafundisha kuwa jua ni nyota.
  
Itikio:
 Angalia vitu viwili: a) jua halijatajwa hapa, na b) maneno yote yaliyomo kwenye parandeshi yamefanywa kuongezwa kwenye tafsiri ya Kiingereza; hayamo kwenye maandiko ya asili ya Kiarabu!
 
Yusuf ‘Ali (toleo lililorekebishwa) anatoa tafsiri sahihi zaidi hapa. "Kwa anga6067 na mgeni mashuhuri wa usiku6068 (humo); Na kitu gani kitaelezea kwako Mgeni mashuhuri wa usiku ni nini? – (Ni) nyota yenye kung’aa kwa ajabu; - hakuna nafsi isiyokuwa na mlinzi juu yake.6069"
 
Rejeo la Yusuf ‘Ali la 606 chini ya ukurasa linasema, "…‘Nyota yenye mng’aro wa ajabu’ inaeleweka na baadhi ya watu kuwa ni sayari ya Saturn, kwa wengine tena ni nyota ya Sirius, au Pleids [Pleiades] au vimondo. Nadhani ni vema zaidi kuielewa ‘Nyota’ kwa mtazamo wa jumla, kwani nyota hung’aa kila usiku katika mwaka, na mng’ao wao wa ajabu unaonekana zaidi kwenye usiku wenye giza nene zaidi." 
Baadhi ya Tafsiri Hazifanani na Ulimwengu Huu!
Hapa kuna maoni mengine ya Kiislam yaliyorekodiwa kwenye http://debate.org.uk/topics/history/interprt.htm. Tovuti hii ina habari nyingine pia nzuri.
 
"Chukulia kwa mfano Muhammad Hanafi al-Banna aliyegundua vidokezo vya ndege (Sura 17:1), setilaiti za bandia (Sura 41:53), safari baina ya sayari (Sura 55:33), na bomu la haidrojeni (Sura 74:33-38) (Jansen 1980:48).
 
Hivyo, haikushangaza wakati watu kama Muhammad Kamil Daww aliandika kuwa muujiza wa mambo ya "kisayansi" yaliyomo kwenye Kurani ulikuwa mkubwa kuliko muujiza wa uzungumzaji usiokuwa na kifani. Jambo hili limemshuhudia Muhammad kuwa ni mkweli, na kwa ajili hiyo usahihi wa maelezo yote ya kwenye Kurani.
 
Leo hii mtu anayefahamika zaidi kwa kuueneza ufafanuzi wa kisayansi ni daktari wa Kifaransa Maurice Bucaille. Kwenye kitabu chake, The Bible, The Qur’an and Science, amejaribu kuonyesha jinsi Biblia isivyokuwa ya kisayansi na wakati huohuo akiiinua hadhi ya Kurani kwa kutumia kigezo hicho hicho."
 
Lakini Baadhi ya Waislam Walikuwa Wanaeleweka Zaidi
Inafaa kusema kwamba Waislam wengine hawaamini tafsiri zilizotangulia. Baadhi yao wanaziona aya hizi kuwa zinazungumzia mambo ambayo yanaweza kuonekana kiurahisi kabisa angani.
 
Muhammad alisema: "Jiepusheni kuniongelea isipokuwa kwa mambo ambayo mnayajua. Mtu yoyote anayezulia uongo kwa makusudi na aandae sehemu yake kwenye jehanamu ya moto. Na yoyote anayeitafsiri Kurani kwa kufuata maoni yake mwenyewe na aandae sehemu yake kwenye jehanamu ya moto." Tirmiz EE, Tefsir 1, (2951) (amechangia).
 
 
"Ndiyo, Tunautupa Ukweli kwa nguvu dhidi ya Uongo, na unaugonga ubongo wake, na tazama, Uongo unaangamia! Ah! Ole wenu kwa ajili ya mambo ya uongo mnayotuzulia." Sura 21:19.
 
Ikiwa mtu yoyote atamzulia uongo Muhammad kwa makusudi, mahali pake patakuwa ni jehanamu. Abu Dawud juzuu ya 3 sura ya 1372 kitabu cha 19 na.3643, uk.1036. Pia Bukhari juzuu ya 2 kitabu cha 23 sura ya 33 na.378, uk.212-213.
 
"...Na yeyote atakayesema kwa makusudi kitu chochote cha uongo dhidi yangu [Muhammad], hakika atapata mahali pake kwenye (jehanamu) ya moto." Bukhari juzuu ya 8 kitabu cha 73 sura ya 109 na.217, uk.139-140.
 
Ushahidi wa uongo ni sawa na kudai kuwa Allah anao wenza. Ibn-i-Majah juzuu ya 3 kitabu cha 13 na.2372, uk.414.
 
Maoni ya Waislam na Maitikio Yake
1. Kurani iliitarajia sayansi ya kisasa: Jua na mwezi ziko kwenye mkondo na huzunguka kwenye mhimili wao (Sura 21:33; 36:27-40). Kurani pia inafundusha nadharia ya mlipuko mkubwa uliosababisha kuumbwa kwa dunia (Sura 21:30; Sura 51:47,48). Neno la Kiarabu falak linamaanisha "mkondo." Wanajimu wanatuambia kuwa jua huzunguka kwenye kitovu cha kundi la nyota kila baada ya miaka karibu milioni 250. Neno la Kiarabu yasbahuna (linatokana na sabaha)linamaanisha kuzunguka mkondo wake.
  
1 Itikio:
 Jambo hili ni ndoto za mchana kwa sababu mbili. 
1) Maneno hayako bayana: 
falak ni neno la Kiarabu lenye kumaanisha njia, kuendelea kwenye mkondo, na yasbahuna inaweza kumaanisha kuharakisha, ingawa maana yake ya moja kwa moja zaidi ni kuogelea. 
2) Muhammad alituambia
 wazi kabisa maana yake, na inamaanisha kuwa jua na mwezi vinasafiri juu ya dunia, vikiwa vimepanda kibandawazi kwenye anga la dunia.
 
Tena, kuna vyanzo viwili vya maneno aliyosema Muhammad.
 
"Mungu aliumba bahari iliyo fasrakh tatu (kilomita 18) toka mbingni. Mawingu yamethibitiwa, inasimama angani kwa amri ya Mungu. Hakuna tone lake lolote linalomwagika. Bahari zote hazitembei, lakini bahari hutembea kwa mwendokasi wa mshale. Inao uhuru wa kutembea angani kwa uwiano sawa, kana kwamba ni kamba iliyovutwa kwenye eneo kati ya mashariki na magharibi. Jua, mwezi, na nyota zinazorudi nyuma [sayari 5] zinakimbia kwenye kilindi cha tumbo lake. Hivi ndivyo neno la Mungu (linavyomaanisha): ‘KIla kimojawapo huogelea angani.’ ‘Anga’ ni mzunguko wa magari yanayokokotwa na farasi kwenye kilindi cha tumbo la hiyo bahari." al-Tabari juzuu ya 1, uk.235.

Abu Dhar alisimulia: Nabii aliniuliza jioni moja, ‘Unajua mahali jua linakokwenda (wakati linapozama)?" Nilimjibu, "Allah na Mtume wake wanafahamu hilo vizuri zaidi." Aliniambia, "Linakwenda (yaani linasafiri) hadi linasujudu chini ya kiti cha enzi, na linapata ruhusa ya kuchomoza tena, na linaruhusiwa na kisha (muda utakuja wakati ambapo) litakuwa linataka kusujudu lakini kusujudu kwake hakutakubaliwa…" Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 4 na.441, uk.283. Sahih Muslim juzuu ya 1 kitabu cha 1 sura ya 73 na.297-300, uk.95-96 pia lina maelezo ya kina ya maongezi ya Muhammad na Abu Dharr.
 
2. Kurani inauelezea mhimili wa jua karibu na kitovu cha kundi letu la nyota
2 Itikio: Jua halina mhimili wake peke yake kwenye kundi letu la nyota. Kama Kurani ilikuwa inajaribu kufundisha sayansi ya kisasa, ingepaswa kusema kuwa jua, mwezi, dunia, na nyota zinazorudi nyuma (sayari) zinazunguka pamoja kwenye mhimili mmoja.
 
Tena, tunafahamu kabisa kitu ambacho Muhammad alikimaanisha, kwa sababu alituambia, kama Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 4 na.441, uk.283 na al-Tabari juzuu ya 1, uk.235 ilivyorekodi.

3. Sehemu ya kupumzikia jua inamaanisha kuwa linaangaza kwenye upande mwingine wa dunia

 
Tena, tunafahamu kabisa kitu ambacho Muhammad alimaanisha, kwa sababu alituambia kama Bukhari juzuu ya 4 kitabu cha 54 sura ya 4 na.441, uk.283 na al-Tabari juzuu ya 1, uk.235 ilivyorekodi.
  
4. Sehemu ya jua kupumzikia inamaanisha uharibifu mkamilifu wa jua

  
4 Itiko:
 Mtu wa kawaida anayesoma hili, kwenye lugha yoyote ile, anaweza kufikiri kuwa inaongelea mzunguko wa vipindi, sio uharibifu mkamilifu.
  
5. Lugha ya ufananisho:
 Jua, mwezi, na sayari huweka alama ya njia angani. Aya hizi hazikuwa na lengo la kuunga mkono au kupinga sayansi ya kisasa, bali zilikuwa ni maelezo ya kishairi zikisema tu kwamba Allah alihusika na vitu ambavyo watu walikuwa wakiviona.
  
5 Itikio:
 Mtazamo huu ungeweza kuwa sahihi isingekuwa maneno ambayo Bukhari na al-Tabari wameandika kuwa Muhammad aliyasema. Kama Bukhari na al-Tabari walikosea kuhusiana na hili, basi kuna kigezo gani cha kusema kuwa walikuwa sahihi kwa jambo lolote.
 
Hitimisho
Baadhi ya Waislam (si wote) wanajaribu kuzitumia aya hizi kuthibitisha usahihi wa kisayansi wa Kurani. Isipokuwa tu kama umeona makosa kwenye uchambuzi huu, haitakuwa sahihi kiakili kujaribu kudai kuwa jambo hili linathibitisha usahihi wa kisayansi wa Kurani. Ukweli ni kwamba baadhi ya hizi aya zinapingana na yale tunayoyajua kupitia sayansi ya kisasa, labda kama utazielewa kuwa ni ushairi na lugha ya ufananisho. Hata hivyo, Bukharina al-Tabari wanaonyesha kuwa aya hizi zilieleweka kama zilivyo. Jua na mwezi zinaogelea angani juu ya dunia.
 
Hata hivyo, kitu cha muhimu zaidi ulimwenguni si vitu unayovijua bali Nani unayemjua. Jambo la maana si kanuni za watu ambazo unaziamini, bali ni kama unafuata kile ambacho Mungu wa kweli amekifunua. Kila mitazamo wa unajimu hadi kufukia karne ya kumi na tisa ulikuwa na makosa ndani yake. Ni nani atakayesema kuwa siku zijazo watu hawatasema maneno hayohayo kuhusu mtiazamo yetu wa kisayansi? Njia pekee tunayoweza kujua kweli ni kupitia kwa yale ambayo Mungu ametufunulia. Tunatumaini kuwa Mungu atatufunulia yale ambayo tunahitaji kuyajua, na kwamba ataitunza maana ya ufunuo Wake.
 
Bibliografia: Tafsiri za Kurani
1. Arberry, Arthur J. The Koran Interpreted. Macmillian Publishing Co., Inc. 1955.
 
2. Dawood, N.J. The Koran. Penguin Books. 1956-1999.
 
3. Malik, Farooq-i-Azam. English Translation of the Meaning of AL-QUR’AN : The Guidance for Mankind. The Institute of Islamic Knowledge 1997.
 
4. Pickthall, Mohammed Marmaduke. The Meaning of the Glorious Koran. Dar al-Islamiyya (Kuwait) (tarehe haijaonyeshwa).
 
5. Rodwell, J.M. The Koran. First Edition. Ivy Books, Published by Ballantine Books. 1993.
 
6. Shakir, M.H. The Qur’an. Tahrike Tarsile Qur’an, Inc. 12th U.S. Edition 2001.
 
7. Sher Ali, Maulawi. The Holy Qur’an. Islam International Publications Limited (Ahmadiyya) 1997.
 
8. Yusuf ‘Ali, Abdullah. The Holy Qur-an : English translation of the meanings and Commentary. Revised & Edited by The Presidency of Islamic Researches, IFTA. King Fahd Holy Qur-an Printing Complex. (Al Madina Saudi Arabia) 1410 BH.
 
Marejeo Mengine
Campbell, Dr. William. The Qur’an and the Bible in the Light of History and Science (2nd edition). Arab World Ministries 2002.
  
The Translation of the Meanings of Sahih Al-Bukhari Arabic-English
 Vol.1 by Dr. Muhammad Muhsin Khan. Islamic University, Al-Medina Al-Munawwara AL MAKTABAT AL SALAFIAT AL MADINATO AL MONAWART
Tarehe haijaonyeshwa, hakina haki miliki.
 
The History of al-Tabari : An Annotated Translation. Ehsan Yar-Shater, General Editor. State University of New York Press, 1989.
 
http://debate.org.uk/topics/history/interprt.htm
 
Kiambatanisho – Tafsiri ya Sura 36:38-40

"Na jua huzunguka kwa kufuata masharti lililopewa; hiyo ni amri ya Mwenyezi, Mwenye kujua vyote. (39) Na (kwa upande wa) mwezi, Tumeuamuria hatua hadi hapo utakapokuwa tena kama tawi kavu na lilillozeeka la mtende. (40) Jua halijaruhusiwa kuupita mwezi wala usiku kutembea haraka kuliko mchana; na vyote vinaelea angani."Tafsiri ya M.H. Shakir.
 
Tafsiri ya Pickthall ina aya zilizo namba moja nyuma.
"(37) Na jua huzunguka kuelekea kwenye sehemu ambayo linapumzikia. Hiki ndicho kipimo cha Mwenyezi, Mwenye busara. (38) Na mwezi Tumeteua kwa ajili yake majumba makubwa hadi hapo utakaporudi kama tawi la mtende la zamani lililojikunja." (39) Jua halipaswi kuupita mwezi, wala usiku kwenda haraka kuliko mchana. Vyote hivi vinaelea kimoja juu ya kingine kwenye mkondo." (Tafsiri ya M.M. Pickthall)
 
(38) Na ishara kwao ni usiku ambao kutoka humo tunachomoa mchana, na tazama! Wamo gizani. (39) Na jua linatembea kwenye njia iliyoamriwa kwa ajili yake. Hii ni amri ya Mwenyezi, Mungu Anayejua vyote."
Tafsiri ya Maulawi Sher Ali (Ahmadiyya)
 
(36:37-40) Ishara yao nyingine ni mwanga; Tunapouondoa mwangaza wa mchana kutoka kwake, na tazama! Wamo gizani. Jua hutembea kwenye njia yake, njia hii imekadiriwa kabla kwa ajili yake na Mwenyezi, Anayejua vyote. Kwa upande wa mwezi, tumeunda awamu kwa ajili yake hadi utakapokuwa tena kama tawi kavu la zamani la mtende. Jua haliwezi kuupita mwezi, wala usiku kwenda haraka kuliko mchana; kila kimoja huelea kwenye mhimili wake wenyewe." Tafsiri yaMuhammad Farooq-i-Azam Malik.
 
(37) Na Ishara kwao Ni Usiku: Tuliuondoa Mchana, na tazama! Walidumbukia kwenye giza; (38) Na Jua Hutembea kwenda kwenye sehemu ya kupumzikia, kwake Yeye: hii ni amri ya (Yeye) Aliyetukuka katika Nguvu, Anayejua vyote. (39) Na mwezi, - Tumepima vituo vyake (vya kupita unaposafiri) Hadi unaporudi kama sehemu ya chini iliyozeeka (na kunyauka) ya kikonyo cha mtende. (40) Jua haliruhusiwi kuukuta Mwezi, wala Usiku kwenda haraka kuliko Mchana: Kila kimoja kinaogelea (tu) kwenye mhimili wake (kwa mujibu wa sheria).
(Tafsiri ya Yusuf Ali ya Kurani (uk.1326-1327) Iliyorekebishwa na Kuhaririwa na Presidency of Islamic Researches, IFTA. King Fahd Holy Qur-an Printing Complex.)
 
(37) Na Ishara yao ni Usiku; Tunauondoa Mchana, na tazama! Wametumbukizwa kwenye giza; (38) Na jua hutembea kwenye njia yake kwa kipindi kilichoamriwa kwake: hii ni amri ya (Yeye), aliyetukuka kwa Nguvu, Ajuaye yote. (39) Na mwezi – Tumepima majumba yake makubwa13 (ya kupita unaposafiri) hadi utakaporudi kama sehemu ya chini ya kikonyo cha mtende iliyozeeka (na kunyauka)." (40) Jua haliruhusiwi kuukuta mwezi, wala Usiku kwenda kwa haraka kuliko Mchana: kila kimoja huogelea (tu) kwenye mhimili17 (wake wenyewe) (kwa mujibu wa Sheira).
Rejeo la 17 chini ya ukurasa linasema "Mzunguko, njia"
Abdullah Yusuf Ali imechapishwa na MILLAT Book Centre
 
Hii inatofautiana na Yusuf Ali ya awali (iliyorekebishwa) kwenye "kwa kipindi kilichoamriwa kwa ajili yake" dhidi ya "kwenye sehemu ya kupumzika, kwa ajili yake" na "vituo" dhidi ya "majumba makubwa."
 
"Na ishara kwao ni usiku; Tunachomoa mchana toka kwake na, tazama! Wamo gizani. na jua – linaenda kwenye sehemu maalum ya kupumzikia; hii ni amri ya Mwenyezi, Yeye Ajuaye yote. Na mwezi- Tumepanga kwa vituo vyake, hadi utakaporudi kama mtende wa kununua uliozeeka. Jua linao wajibu wa kutokuupita mwezi, wala usiku kwenda haraka kuliko mchana, kila kimoja kinaogelea angani." Tafsiri ya A.J. Arberry.
 
"Ishara kwao ni usiku. Tunaondoa mchana kutoka kwake, na tazama! Wametumbukia kwenye giza; Na jua liliharakisha kwenda kwenye sehemu yake ya kupumzikia. Hii, amri ya Mwenyezi, Ajuaye vyote! Na kwa upande wa mwezi, tumeamuru vituo kwa ajili yake, hadi utakapobadilika kama tawi la zamani la mtende lililopinda. Jua halijaruhusiwa kuupita mwezi, wala usiku kwenda haraka kuliko mchana; bali kila kimoja kusafiri kwenye anga lake lenyewe."
Tafsiri ya J.M. Rodwell ya Kurani.
 
"Usiku ni ishara nyingine kwa watu. Kutoka kwenye usiku Tunauondoa mchana – na wanatumbukizwa kwenye giza. Jua huharakisha kuelekea kwenye sehemu yake ya kupumzikia; njia yake imewekwa kwa ajili yake na Mwenyezi, Yeye Ajuaye yote. Tumeamuru nyakati za mwezi, ambao huingia ndani na mwishowe huonekana kama kijiti cha zamani kilichojikunja. Jua haliruhusiwi kuupita mwezi, wala usiku kwenda kwa haraka kuliko mchana. Kila kimoja huogelea kwenye mhimili wake wenyewe."
Tafsiri ya N.J. Dawood ya Kurani. 

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW