Tuesday, July 21, 2015

QURAN IMEJAA SHAKA NA MASWALI YA KUTATANISHA



Waislamu wamekuwa na kawaida ya kufanya kila juhudi kuonyesha kwamba Biblia imepotoshwa, ingawaje jambo hilo si kweli hata kidogo.
Na juhudi hizi zote zinafanywa ili kutaka kuonyesha kwamba Quran ni neno la Mungu la kweli ambalo halijapotoshwa hata kidogo. Basi mimi naomba mnisaidie majibu ya maswali haya machache kati ya mengi:
1. Sura 54:19 inasema kuwa mji wa Aad uliharibiwa kwa siku moja na sura 69:6,7 inasema kuwa uliharibiwa kwa 'usiku' sita na siku nane (seven nights and eight days). Hapo kuna mkanganyiko au la?
2. Sura 19:17 inaonyesha kuwa malaika alimtokea Mariamu lakini sura 3:42 inasema walikuwa malaika wengi.
3. Sura 28:40 inasema kuwa farao alizama na kufia kwenye maji lakini sura 10:92 inasema kuwa farao huyo alipona.
4. Sura 18:86 inasema kuwa jua huzama kwenye chemchemi ya maji yenye tope. Unadhani hii ni sahihi. Jua lina joto la zaidi ya nyuzijoto 6000 kwenye uso wake. Lakini maji yakifika nyuzijoto 100 yanageuka mvuke. Je, maji yanayotajwa kwenye sura hii ni maji gani? Unadhani ni Mungu aliyeumba jua na maji ndiye anayesema haya?
5. Sura 15:19 inasema kuwa dunia ni bapa kama meza (flat). Kama Mungu ndiye aliumba dunia na ndiye alileta Quran, anaweza kusema jambo kama hili?
6. Sura 86:6,7 inasema kuwa manii ya mwanamume hutokea kati ya uti wa mgongo na mbavu. Hii ni sayansi ya wapi? Ni kutoka kwa Mungu aliyeumba wa mbingu na nchi na uti wa mgongo na mbavu kweli? Kama haitoki kwa Mungu basi hata kitabu chenyewe nacho hakitoki kwa Mungu, au siyo?
7. Sura 19:27,28 inasema kuwa Mariamu alikuwa ni dada wa Haruni. Lakini tangu Haruni aishi ilipita miaka 1300 ndipo alipozaliwa Mariamu. Ni Mungu gani basi anayeweza kusema maneno kama haya?
8. Sura 28:8 inasema kuwa farao na Hamani waliishi wakati mmoja na mahali pamoja. Lakini historia iko wazi kwamba kuna tofauti ya miaka takribani 1000 kati ya watu hawa. Vilevile, farao aliishi Misri wakati Hamani aliishi Uajemi kwenye ngome iliyoitwa Shushani.
Huu ni Msiba Mkubwa sana katika Uislam
Max Shimba Ministries Org

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW