Thiolojia ya msingi ya kiislam inafundisha kwamba kwa vile Allah alimtuma Gabriel akiwa na Kurani kwa Muhammad Mjumbe wa Allah, Muhammad na Kurani vinatimiza na kukamilisha lengo na huduma ya Kristo na Agano Jipya. Muhammad anaelekea kutambua umuhimu wa Biblia (Sura 4:47; 4:136; 4:163; 5:44-48; 5:82-83; 6:92, 154), lakini, ukristo na Agano Jipya vinatakiwa kujinyenyekeza kwa uislam na Kurani, ufunuo mpya na ulio bora zaidi.
Sura 5:15-16 inaeleza mtazamo wa Muhammad kwa kutumia mfano. Kwa muktadha wa upotofu wa Muhammad wa mafundisho ya kikristo ya Yesu kuwa Mwana (v. 17), na katika muktadha wa madai yake kuwa Wayahudi wamelaaniwa (v. 13), kifungu hiki kwenye Kurani (kikiwa kinaviwakilisha vingine) kinasema kwamba Wakristo (na Wayahudi) wamekuwa wakitembea gizani hadi wakati Muhammad alipokuja:
5:15 Watu wa Kitabu [Wayahudi na Wakristo] . . . mwanga umekuja kwenu sasa kutoka kwa Mungu, na Maandiko [Kurani] ikifafanua mambo, 16 ambayo kwayo Mungu huwaongoza wale wafuatao mambo yanayompendeza kwenye njia za amani, akiwatoa kutoka gizani na kuwaleta kwenye mwanga, kwa matakwa yake, na kuwaongoza kwenye njia iliyonyooka. (Haleem) (linganiasha na 4:157).
Mkristo wa leo mwenye ufahamu wa Biblia atatambua mara moja tamathali ya mwanga. Yesu anasema kuwa alitumwa toka mbinguni kama nuru ya ulimwengu, na Wakristo wamevuka kutoka giza kwenda nuruni (John 1:4-5, 8:12, 9:5, 12:46; 1 Petro 2:9). Lakini, sasa, Muhammad anadai kuwa Wakristo wamekuwa wakiishi kwenye giza, na amekuja kufafanua mambo kwao, kana kwamba mambo yalikuwa yamevurugwa. Kurani inatoa maongozi kwenye "njia iliyonyooka", mada ambayo imerudiwa mara kadhaa kwenye Maandiko ya kiislam (k.m. Sura 1) na "inafafanua mambo." Mstari wa 16 ni moja ya mistari ambayo Muislam anaweza kuufikiria wakati anapoonyesha kuwa uislam ni dini ya amani. Lakini je ni kweli?
Mkristo aliyejitoa, na mwenye ufahamu wa Biblia hawezi akaamini kwa vyovyote vile kuwa Uislam ni bora, tunawezaje kuuunja mvutano huu uliokwama? Je tuupuuzie? Kwa kuzingatia matokea ya karibuni kama mashambulizi ya kigaidi ya Marekani (Septemba 11, 9/11), jambo hili haliwezekani tena. Je tunajifanya kuamini kuwa dini zote ni sawa? Lakini jambo hili linatulazimisha kuyakana baadhi ya mafundisho ya msingi yasiyoweza kujadiliwa ambayo dini zote zinakuwa nazo na yale ambayo hayawezi kupatanishwa. Kwa jinsi hiyo basi, je tunabishania mafundhisho haya ya kuwazika tu?
Kujadili mambo ya kuwazika kama vile Umoja wa Utatu wa Mungu, kuna sehemu yake katika mazungumzo ya Waislam na Wakristo, lakini hakuna upande unaoweza kudai kuwa unaweza kuthibitishwa kwa uelekevu rahisi wa kutambua (simple observation). Kurani kila sehemu inatamka kwa dhati Umoja wa Mungu, wakati Agano Jipya linatamka kwa udhati kuwa Yesu ni Mungu na Roho Mtakatifu ni nafsi. Kwa hiyo tumepambanisha kifungu kitakatifu kimoja dhidi ya kingine, na ili kuuvunja mvutano huu usiokwisha ni lazima tutumie njia zingine. (Kwa habari zaidi za kuaminika kwa Agano Jipya, tembelea tovuti hii, site; kwa matatizo asilia ya Kurani, nenda hapa here.)
Kwenye muktadha wa Hotuba ya Mlimani, Kristo aliongea kwa makutano, ama hakuna mtu kati yao aliyekuwa mwana thiolojia ama ni wachache tu, bali walikuwa wakulima wa hali ya chini. Kwenye Mathayo 7:15-20, Kristo anatumia lugha isiyokuwa na utata kuhusu namna ya kuutambua ukweli wa manabii:
7:15 Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa mwitu wakali. 16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? 17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. 18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. 19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. 20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua.
Katika ulimwengu wa magharibi wa leo ambamo mamilioni ya watu hawapendelei kuutikisa uislam bali kuukirimu, kifungu hiki kinaweza kuonekana kukosa uvumilivu. Lakini katika aya hizi Kristo anafahamu hatari yake. Madai ya kweli za kidini yamekuja ulimwenguni kwa idadi kubwa, karibu kila sekunde, na madai haya si ya kuwazika tu; maisha ya watu yamo hatarini. Kwa hiyo gharama ya kuukirimu, hasa kuanzia 9/11, ni kubwa mno.
Pamoja na hayo, ni Muhammad aliyesema kuwa yeye ni mkuu kuliko Kristo na kwamba dini yake mpya ni bora kuliko ukristo. Yeye ndiye aliyeanza kuleta upinzani. Kwa hiyo, miaka zaidi ya 600 kabla ya kuja kwa Muhammad, Kristo alimjibu yeye pamoja na watu wengine wengi wanaojiita manabii walioeneza pande zote za Bahari ya Kati tunda la ukaguzi.
Kuelezea kwa mfano, hebu tuchukulie kuwa ninadai kuwa njia yangu ni bora kuliko yako. Kisha naweza kuthibitisha madai yangu ya maneno kwa vitendo vinanavyoonekana. Mwenendo wangu utakuwa bora kuliko wako, kwa sababu matendo yangu yanazungumza kwa nguvu kuliko maneno yangu. Kwa kuainisha, kama mwanzilishi wa dini anasema kuwa waume kwenye jumuiya yangu wanaruhusiwa kuwapiga wake zao (Sura 4:34), lakini wewe kama mwanzilishi wa unasema kuwa waume kwenye jumuiya yako hawaruhusiwi kuwapiga wake zao, je ukuu wangu ninaodai kuwa nao waweza kusimama kwenye maisha halisi? Ninajenga mfano mbaya kivitendo, lakini wewe haufanyi hivyo.
Nifanyacho ni kuwa sienezi tunda la ukaguzi. Yaani, tunda langu au mwenendo au matendo yangu halisi yameoza. Kwa hiyo, Yesu ni sahihi kabisa kutumia mfano huu rahisi kwa wafuasi wake kuchunguza madai ya manabii watakaokuja baada yake. "Mtawatambua kwa matunda yao" (Mt 7:16).
Tunaweza kukiona kiini cha pingamizi la Muhammad na ukaguzi wa matunda wa Kristo kwa kutumia hoja rahisi ya mantiki ikiwa-basi (sababu/chanzo-matokeo). Njia hii hufahamika kama "modus tollens" au kuyakana matokeo (sehemu ya "basi").(1) Ikiwa A, basi B. Ikiwa uislam haujajiboresha na kuwa mzuri kuliko ukristo, basi mabadiliko haya yangeonekana kwenye njia zinazoonekana na zenye kuhusika na mambo halisi.
(2) Si-B. Lakini haya mabadiliko hayaonekani kwenye njia zinazoonekana na zenye kuhusika na mambo halisi.
(3) Kwa hiyo, si-A. Kwa ajili hiyo, uislam haujajiboresha na kuwa mzuri kuliko ukristo.
Sasa tunaweza kuitetea kila kauli kirahisi.
(1) Ikiwa uislam umejiboresha na kuwa mzuri kuliko ukristo, basi mabadiliko haya yangeonekana kwenye njia zinazoonekana na zenye kuhusika na mambo halisi.
Tumeisha itetea kauli hii kwenye sehemu inayotangulia. Kuchunguza maisha na matendo ya mwanzilishi wa ukristo na mwanzilishi wa uislam ni njia ya kwanza na bora zaidi ya kuuvunja mvutano usiokuwa na mwisho kati ya dini hizi mbili zenye kupingana, kwa sababu tunaweza kuona mienendo na matendo yao hapa hapa duniani. Mtawatambua kwa matunda yao.
(2) Lakini haya mabadiliko hayaonekani kwenye njia zinazoonekana na zenye kuhusika na mambo halisi.
Kuitetea kauli hii kwa kutumia ushahidi unaoshikika kunajibu kiwazi kabisa pingamizi ambalo Muhammad ameweka dhidi ya Kristo na inadhihirisha bila shaka yoyote kuwa tunda la Muhammad ni baya, wakati tunda la Kristo lina afya nzuri na limeiva.
Orodha ifuatayo imekwishatengenezwa kwenye makala ya kwenye tovuti hii, this article, ambayo ni msingi wa makala hii. Kama msomaji anaamini kuwa matendo halisi ya kwenye maisha ya Muhammad na aya zinazofuata kwenye Kurani yamechukuliwa nje ya muktadha wake au katika hali ya kutokuonekana, basi, hapo tena, aende kwenye tovuti nyingine zilizotolewa kwenye maelezo husika. Matendo haya yenye kutiliwa mashaka kimaadili yalitokea kabisa kwenye jumuiya ya Muhammad, na Muhammad, kwenye Kurani yake, anaamuru ukatili huu. Pia, ili kuona aya za Kurani kwenye tafsiri nyingi, msomaji anatakiwa kwenda hapa here na kupiga taipu kwenye marejeo, kama 24:2 (24 ni sura, na 2 ni aya). Achana na ombi la vichwa vya sura za Kiarabu vilivyonukuriwa kwa mfumo tafauti, na piga taipu namba tu.
*Muhammad anatoa majina ya utani kwa silaha zake, na anajipa jina la utani "mhalifu."Kristo hakuwahi kumiliki silaha kwa sababu hakuwahi kupigana vita na watu.
*Muhammad kwenye Kurani yake aliamuru kuwa wazinzi wapigwe mijeledi mia moja (Sura 24:2). Hadithi zenye kuaminika (maneno na matendo ya Muhammad nje ya Kurani) zinaamuru kuwapiga mawe.
Kristo alimsamehe mwanamke aliyekutwa akizini. Watu waliokusanyika ili kumpiga walitupa mawe yao na kuondoka. Alibaki, akilia hadi Yesu alipomwambia nenda na usitende dhambi tena (John 8:1-11).
*Muhammad kwenye Kurani yake aliwaruhusu wanaume kuwapiga wake zao (Sura 4:34).
Si Kristo wala waandishi wa Agano Jipya walioruhusu jambo hili au kulitenda.
*Muhammad kwenye Kurani yake anaamuru kuwa mikono ya mwizi, mwanamke au mwanaume, ikatwe (Sura 5:38).
Kristo hakuwahi kusema kufanya hivi. Mtume Paulo alisema kuwa wezi na wafanye kazi kwa mikono yao, siyo kuikata, ili waweze kupata kitu cha kuwagawia watu wengine wenye uhitaji (Waefeso 4:28). Katika jambo hili (na mengine mengi) Paulo anamzidi Muhammad.
*Muhammad aliwaua watunga mashairi na maadui wa kisiasa.
Kristo hakuwahi kuwaua maadui zake wowote wala hata watunga mashairi (hata walio wabaya).
*Muhammad kwenye Kurani yake aliamuru ahabu ya kifo au kukatwa mikono na miguu kwa watu wanaopigana au kuichafua nchi (Sura 5:33).
Kristo, Mfalme wa Amani, alikufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, ili kwamba "uharibifu" na "kupigana" vimalizike.
*Muhammad alimuoa Aisha, msichana aliye bado kuvunja ungo, na kuikamilisha ndoa yake na yeye wakati Aisha akiwa msichana mdogo tu. Kwa ushahidi kamili kuhusu tendo hili la kifamilia la Muhammad ambalo ni la ajabu sana hata kwa Arabia ya karne ya saba, wasomaji wanapaswa kuangalia makala hiyo this article. Kurani yenyewe inaruhusu ndoa kama hizi zisizokuwa halali kwa Waislam wengine pia (Sura 65:4).
*Muhammad kwenye Kurani yake anaahidi bustani yenye kutamanisha "iliyojaa mabikira" kwa wafia dini watakaopoteza maisha yao kwenye vita vitakatifu (Sura 44:51-56, 52:17-29, 55:46-78, 61:10, 4:74, 9:111).
"Ufia dini" wa Kristo msalabani unamaanisha kuwa Wakristo hawapaswi kufa kwenye vita vitakatifu ili kuweza kupata uhakika wa kuingia mbinguni. Kitu pekee wanachotakiwa kukifanya ni kumwamini Yesu.
Kristo alikuwa Myahudi na aliwapenda watu wake. Pamoja na hayo, anawapenda watu wote wa duniani-hata wale wanaoabudu miungu mingi ambao Muhammad aliwaua-na anawakomboa kwa njia ya kufa, kuzikwa, na Kufufuka kwake. Hakutumwa kuua watu.
*Muhammad alinzisha vita yake mwenyewe vya kidini (Crusade) mwaka 630 BK akiwa na wapiganaji 30,000 dhidi ya Wabezantini-ambao hawakutokea (Sura 9:29). Kristo hakuwahi kufanya hivi. Kitu ambacho wazungu wa zama za kati (Medieval Europeans) walikfanya kwa jina lake si msingi wa ukristo. Ni Yesu na Agano Jipya tu ndivyo vilivyo msingi, na havikuidhinisha vita vitakatifu. Muhammad, kwa upande mwingine, ni msingi wa uislam, na alianzisha vita vitakatifu dhidi ya Wakristo wa kibenzantini, na aliidhinisha na kwenda kwenye vita nyingi sana takatifu.
Sura 5:16, iliyonukuliwa kwenye utangulizi wa makala haya, inasema kwa msisitizo kabisa kuwa uislam ni dini ya amani. Orodha hii, hata hivyo, inapingana kiwazi moja kwa moja na maneno haya ya msisitizo. Matendo husema kwa nguvu kuliko maneno. Kwa hiyo, uislam siyo dini ya amani, tazama tovuti hii not the religion of peace.
Kwa kurudia, kama msomaji anaamini kuwa hoja hizi zimetolewa nje ya muktadha wake, anaweza kubpnyeza kwenye tovuti hiyo hapo juu kisha kwenye tovuti nyingine zilizotolewa kwenye kila hoja.Wakristo watawatambua manabii kwa matunda yao. Kwa kusema wazi, Muhammad, mjumbe na nabii aliyejitangaza mwenyewe (Sura 3:144), ameshindwa kabisa ukaguzi wa kihalisi wa tunda. Kwa upande wingne, Kristo Mwana wa Mungu (Matt. 3:16-17) amefaulu kwa ushindi mkamilifu.
(3) Kwa hiyo, uislam haujajiboresha na kuwa mzuri kuliko ukristo
Hitimiso hili linakuja moja kwa moja na kwa mantiki.
Kwa watu wasiopendelea upande wowote na walio tayari kusikia hoja, mambo yahusuyo maisha halisi kama kumpiga mke na kuwapiga mijeledi wazinzi na kuoa wasihana ambao bado hawajavunja ungo yanatosha kufanya uamuzi. Matendo na sera za kihalisi haviwezi kupuuzwa, isipokuwa watu wawe wamechagua kufumba macho na kukataa kuona ni jinsi gani mambo yalivyo makosa dhahiri, au ladba kama nabii atakuwa na jeshi kubwa la kumsaidia kulazimisha matendo yake kwa wafuasi "wanyonge" wa dini "isiyokamilika" iliyotangulia.
Na jambo hili linaturudisha kwenye mafundusho kuwazika, tena kwa kujitumia mimi mwenyewe na msomaji kama kielelezo. Kabla ya kujadili mafundisho yanayotegemea nadharia kama asili ya Mungu, kama mfuasi wa dini lazima nifaulu tunda la ukaguzi. Hebu tufikiri kuwa ni mazoea yangu kuua watu wanaoamini miungu mingi kwenye vita vyenye kupoteza maisha ya watu wengi sana, badala ya kuwaongoa kwa kuwahubiria tu au badala ya kuwaacha waishi kama wamekataa kuongoka (Sura 9:4-5). Kwa upande mwingine, si mazoea yako kuwaua watu wanaoabudu miungu mingi, lakini kuwaongoa kwa kuwahubiria tu na kuwaacha waishi kama wamekataa kuongoka. Katika hali hizi, nashindwa tunda la ukaguzi lililo halisi na linaloweza kuonekana, lakini wewe umefaulu. Kwa hiyo, napoteza haki yangu ya kuaminika kwenye madai mengine kuhusu asili ya Mungu na mafundusho mengine ya kuwazika ambayo hayawezi kuonekana. Ni dhahiri kuwa ama najitumikia mimi mwenyewe au, mbaya zaidi—namtumikia mungu mnyonge. Wewe, kwa upande mwingine, una mawazo sahihi yanayoweza kufanyiwa kazi, kwa hiyo unastahili kupewa haki ya kusikilizwa.
Kwa namna hiyohiyo, kushindwa kwa Muhammad kwenye pingamizi lake kwa Kristo kunaweza kuelezwa kwa hoja nyingine ya kama-basi, safari hii kwenye kanuni ya mantiki iitwayo modus ponens au kuthibitisha sehemu ya maneno inayotangulia (sehemu ya maneno "kama" inayotangulia kwenye kishazi.
(4) Ikiwa A, basi B. Ikiwa uislam huajajiboresha na kuwa mzuri kuliko ukristo kwa namna ya kihalisi inayoweza kuonekana, ni dhahiri kuwa haujajiboresha na kuwa mzuri kuliko ukristo katika mambo ya kinadharia ambayo ni ya kuwazika tu.
(5) A imethibitishwa. Uislam haujajiboresha na kuwa mzuri kuliko ukristo kwenye mambo ya kihalisi yanayoweza kuonekana.
(6) B imethibitishwa. Kwa hiyo, uislam haujajiboresha na kuwa mzuri kuliko ukristo katika mambo ya kinadharia ambayo ni ya kuwazika tu.
Hoja mbili za kwanza zinaweza kutetewa kirahisi.
(4) Ikiwa uisalam haujajiboresha na kuwa mzuri kuliko ukristo kwa namna ya kihalisi inayoweza kuonekana, ni dhahiri kuwa haujajiboresha na kuwa mzuri kuliko ukristo katika mambo ya kinadharia ambayo ni ya kuwazika tu.
Muhammad ni kielelezo cha uislam kwa kuwa alikuwa alikuwa ni mfereji kupitia huo Allah alifunua dini bora zaidi, kwa hiyo tunamtumia tena kuupima uislam. Kukagua tunda kunasema kuwa ikiwa nabii atashindwa kuwa nalo basi madai yake ya kuwazika zaidi yanatia mashaka. Kwenye muktadaha wa ulimwengu (usiokuwa wa kidini), kipimo hiki ni kikubwa mno kwani wanadamu wote wana mapungufu. Mtaalamu wa fizikia anaruhusiwa kuzumgumzia mambo ya kuwazika kuhusu nafasi (space) na muda hata kama maisha yake yamejichanganya au hata yaliyo jaa dhambi. Lakini kwenye muktadha wa kidini, hususani wakati kiongozi mmoja wa kidini (Muhammad) anadai kuwa yeye ni bora kuliko kiongozi mwingine (Kristo), kipimo hiki ni muhimu na hakiepukiki.
Isitoshe, habari za kweli zinathibitisha kushindwa kwa Muhammad kwenye mawazo ya kuwazika. Kwa mfano, ni ukweli unaoweza kuthibitishwa kuwa Agano Jipya linaaminika, wakatia ambapo Kurani ina sehemu yake ya lawama. (Kwa habari zaidi kuhusu somo hili tazama kurasa hizi hapa here na hapa here). Pia ni jambo linaweza kuthibitishwa kuwa Muhammad hakuwa amejifunza mambo yahusuyo fikra za juu. Alichokifanya ni kwamba alichukua mchanganyiko wa mawazo yaliyokuwa yameenea kwenye njia za biashara na akayaingiza kwenye Kurani yake (kama wazo lisilo na mantiki lenye kukana kifo cha Kristo msalabani kwenye Sura 4:157), na kudai kuwa ni ufunuo wa kiungu toka kwa Allah. Hivyo basi, kwa njia ziliyowazi na dhahiri Muhammad hakuwa anauboresha ukristo (na Uyahudi), lakini alikuwa anaziharibu dini hizo mbili zilizo mtangulia. Kwa hiyo, ukweli wa kihistoria unathibitisha kuwa anaweza kuwa si sahihi kwyenye mafundisho ya kinadharia—hafahamu kitu anachokiongelea.
(5) Uislam haujajiboresha na kuwa mzuri kuliko ukristo kwenye mambo yanayoonekana na yenye kuhusika na ukweli halisi.Baada ya kusoma orodha kwenye hoja ya pili, mtu yoyote anayetafuta kujua ambaye ana busara na uwezo wa kufikiri na ambaye mawazo yake hayajafunikwa na kujitoa kwa maisha yote kwenye uislam atafikia kwenye uamuzi kuwa Muhammad ameshindwa kwenye ukaguzi wa tunda katika njia za vitendo, zenye kuonekana na zenye kuhusika na ukweli halisi.
(6) Kwa hiyo, ni dhahiri kuwa uislam haujajiboresha na kuwa mzuri kuliko ukristo kwenye mambo ya kinadharia, ya kuwazika tu.
Maoni haya yanatokea kiwazi na kimantiki.
Kwa kutumia orodha ya tofauti kubwa sana kati ya Kristo na Muhammad kwenye hoja ya pili, kwa nini watu wenye mawazo yasiyo na upendeleo na walio tayari kusikiliza hoja wanasikiliza mafundisho yenye fikra kubwa na ya maneno tu ya Muhammad yanayokataa Utatu au uungu wa Kristo (Sura 2:116, 6:101, na 4:171, 5:73) au kwamba wanaunga mkono bila matata upotofu wa Kurani (isipokuwa tu awe na jeshi kubwa pamoja naye)? Wakaguzi wa tunda wenye mawazo yasiyo na upendeleo na walio tayari kusikiliza hoja wanaweza kuona kuwa kitabu chake Kilichovuviwa kinatia mashaka kwa sababu maisha yake ya kutia mashaka na kwa sababu kimejawa na matendo yasiyokuwa ya haki. Kwa kweli, watu wenye mawazo yasiyo na upendeleo wana haki ya kukipenda Kitabu cha Kristo cha kweli na chenye upole zaidi lakini chenye kudaiwa kuwa na "makosa", siku yoyote na siku zote kuliko Maandiko ya Muhammad yanayodai kuwa "sahihi" lakini yanayovuka mipaka. Kwanza, Muhammad anatuonyesha maisha yake ya mfano kabla hajaruhusiwa kuhubiri kuhusu thiolojia ya fikra kubwa au kabla hatuja yachukua mafunuo yake ya kuwazika kuwa ni ya kweli.
Kwa Wakristo wa kawaida, hasa wafuasi wa kwanza ambao Yesu alikuwa akiwafundisha kwenye Hotuba ya Mlimani kwa Waisraeli wakulima wa karne ya kwanza, Kristo anasema kuwa kwa matunda ya nabii wafuasi wa Kristo watamjua. Mara tunda la nabii linapokuwa baya, au linaanza kuzaa mti mbaya, basi hawahitaji kukagua madai yake ya kwazika tu. Mtu huyu anakuwa nabii wa uongo—maneno haya ni mazito sana kwa uhakika, lakini ni maneno ya Kristo (Matt. 7:15).
Maswali matatu: Je kushindwa huku kufaulu kukagua tunda kunaufanya mjadala wote usiwe wa maana? Kama wanathiolojia wa kikristo na kiislam kwenye chumba cha mikutano wanataka kujadili kuhusu Utatu, wana uhuru wa kufanya hivyo—ingawa kuna mashaka juu ya kiasi wanachoweza kufanya. Majadiliano yao ni ya kitaaluma tu. Hata hivyo, wasitegemee mamilioni juu ya mamilioni ya Wakristo wenye ufahamu wa Biblia ulimwenguni watajiona kuwa wanalazimika kujadili mambo haya. Lakini hata kama wanapenda kujadili thiolojia ya kuwazika wana uhuru wa kufanya hivyo. Waislam hawatakiwi kushangaa, hata hivyo, kama mwisho wa siku hawa Wakristo hawatamchukua Muhammad na mafunuo yake kuwa ya kweli kwa sababu Kristo aliishawaambia wafuasi wake mambo ya kuyaangalia: matunda mazuri (Matt. 7:15-20). Muhammad aliishi maisha yenye utata yanayotunzwa kwenye Kurani yake inayodaiwa kuwa ya milele na haina makosa, kwa hiyo Wakristo wanaruhusiwa kuitilia shaka Kurani kwenye mambo ya kinadharia.
Je uhusiano kati ya mambo ya kivitendo na kinadharia ni jambo lisiloweza kujipinga? Kristo kwenye Matt. 7:15-20 anadokeza kuwa ni kweli kwamba uhusiano huu hauwezi kujipinga. Kwa kurudia, kama Muhammad hakuwa sahihi kuhusu mambo ya kivitendo kama kuwapiga wake, kuwapiga mijeledi wazinzi, kuanzisha mashambulizi ya kijeshi ya Vita vya kidini, kuwaua watunga mashairi na maadui, na kuwaahidi wapiganaji wake Bustani zilizojaa mabikira kama watakufa kwenye vita takatifu, ni kwa nini basi Wakristo wamsikilize Muhammad kwenye mambo ya kinadharia, hasa kwa kuwa Agano Jipya kila sehemu linathibitisha, kwa mfano, kuwa Kristo ni Mungu na Roho Mtakatifu ni nafsi? Na jambo la muhimu zaidi ni kwamba, kwa nini Wakristo wanataka kubadili dini kuwa Waislam, ingawa mwenendo wa Muhammad unatilisha mashaka?
Je hakuna sifa nzuri (tunda) linalomhusu Muhammad? Hata kushindwa kwa kiasi kikubwa sana kwa ukaguzi wa tunda kunaweza kuwa na sifa nzuri, japo kidogo. Mwanzilishi wa harakati anapaswa kuonyesha kiasi fulani cha upole ikiwa anataka jumuiya yake iendelee kuwepo. Lakini sifa nzuri haziwapigi na kuwaumiza watu wengine. Hata hivyo, mienendo mibaya huumiza na kuwapiga na kuwaumiza watu wengine. Picha ya jumla ya maisha ya Muhammad huko Medina (mwaka 622-632) inamuonyesha akipigana vita dhidi ya watu wenye kuamini miungu mingi (anaiteka Maka); dhidi ya Wayahudi (akiwahamisha na kuwaua); na dhidi ya Wakristo (akianzisha vita vya kidini). Katika miaka kumi aliyoishi pale, alikwenda, alituma au kuanzisha mashambulizi, safari zenye malengo ya kivita au vita kamili sabini na nne, kuanzia majadiliano ya amani (machache sana kulinganisha na mashambulizi ya kikatili), hadi vikundi vya mashambulizi ya uuaji, hadi kuiteka Maka kwa kutumia wapiganaji 10,000, hadi vita vya kidini vyenye wapiganaji 30,000 dhidi ya Wabezantini (ambao hawakutokea). Hakuna anayeweza kuisafisha picha hii mbaya inayotia giza sifa zake nzuri.
Kwa hiyo, Muhammad hakamilishi wala kutimilisha misheni na huduma ya Kristo—tofauti na hivi, kwani Kristo alikuja ulimwenguni kuonyesha upendo wa Mungu. Ki ukweli, Muhammad na uislam ni tafsiri mbaya ya Kristo na ukristo, na Kurani ni mbaya kuliko Agano Jipya kwa kuiangalia kwa mambao yanayoweza kuchunguzika.
Je uislam unajijenga kuwa bora kuliko ukristo? Kwa kuangalia ushahidi unaoweza kuonekana, jibu ni hapana ya nguvu. Muhammad amesindwa kabisa kufaulu ukaguzi mdogo tu wa tunda.
[Makala hii inayo makala mwenzi companion piece]
James Arlandson (PhD) anafundisha utangulizi wa filisofia na dini za duniani kwenye chuo kikuu kusini mwa California. Ameandika kitabu, Women, Class, and Society in Early Christianity (Hendrickson, 1997). Anaweza kufikiwa kwa barua pepe jamesmarlandson@hotmail.com.
James Arlandson
No comments:
Post a Comment