(Sehemu ya Nne)
“Marafiki na maadui wa Yesu waligawanyika tena na tena na kile alichosema na alichofanya [Yesu]. Alikuwa alitembea barabarani, dhahiri kama mtu yeyote, kisha akageuka na kusema kitu fulani mfano ‘Kabla ya Abraham kuwako, nipo.’ Au iIkiwa umeniona, basi umemuona baba. Kisha kwa utulivu baada ya kulaumiwa kukufuru, alisema, ‘Mwana wa Adamu ana mamlaka duniani kusamehe dhambi’ Kwa wafu, alisema ‘Njoo mbele’, au, ‘Inuka’ na walitii. Kwa tufani baharini aliweza kusema ‘Tulia’ na kwa kipande cha mkate, alisema ‘Kuwa vipande elfu moja’ na vilifanyika mara moja.”
Baadhi ya watu wanadai hakuwai waziwazi kusema “Mimi ni Mungu”. Je, ni kweli kwamba hakuwai kunena maneno hayo? “Mimi ni Mungu”. Vilevile, Yesu hakuwai waziwazi kusema “Mimi ni binadamu” au “Mimi ni Nabii” Na Yesu alikuwa binadamu bila shaka, na wafuasi wake walimchukulia kama nabii kama Musa na Eliya. Kwa hiyo hatuwezi kuamua kwamba Yesu kuwa mtakatifu ni kwa sababu hakusema maneno hayo, kama ambavyo hatuwezi kusema hakuwa Nabii.
“Wahubiri wa injili” wa Kiislamu huwa wanapinga kuwa Yesu ni Mungu na unapowakatalia wanakwambia, “Lete andiko.” Maandiko yapo mengi sana ndani ya Biblia juu ya ukweli kwamba Yesu ni Mungu. Ni mengi mno!
Ukishawapa andiko, wanabadilika na kusema, “Nataka maneno aliyoongea Yesu mwenyewe.”
Hiki ni kigezo POTOFU na si cha kibiblia hata kidogo. Ukweli ni kwamba, Biblia YOTE ni Neno la Mungu. Haijalishi amezungumza Musa, Isaya, Yohana, Petro au Yesu mwenyewe. Imeandikwa:
Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu. (2Petro 1:21).
Hivyo, kudai kwao eti, “Nataka maneno aliyosema Yesu mwenyewe,” ni kigezo batili na kisicho na mantiki hata kidogo.
Ufuatao ni ushahidi wa kibiblia kwamba YESU KRISTO ni Mungu.
Yohana 8:58
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye IBRAHIMU ASIJAKUWAKO, MIMI NIKO.
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye IBRAHIMU ASIJAKUWAKO, MIMI NIKO.
NIKO ni jina la Mungu peke yake. Tunakutana na jina hilo pale Musa alipoongea na Mungu na kutumwa kuwakomboa wana wa Israeli kutoka Misri. Imeandikwa:
Musa akamwambia Mungu, Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli, na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu; nao wakaniuliza, Jina lake n'nani? Niwaambie nini? Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO (Kutoka 3:13-14).
Mwanadamu yuko kwa sababu Mungu alisababisha awepo. Gari liko kwa sababu injinia au mbunifu alisababisha liwepo. Nyumba ipo kwa sababu fundi alisababisha iwepo. Lakini Mungu YEYE YUKO TU!! Hayupo kwa kusababishwa na yeyote! Ndiyo maana akasema MIMI NIKO AMBAYE NIKO! Yesu ni NIKO. Kwa hiyo, Yeye ni Mungu.
Yohana 10:30
Mimi na Baba tu umoja.
Mimi na Baba tu umoja.
Waislamu wana msemo wao kwamba eti, Yesu na Mungu ni wamoja katika malengo, si katika asili yao. Basi huwa nawauliza swali kuhusu aya ifuatayo ya Isaya, nao wanazimika na kukosa jibu: