Ndugu Msomaji,
Hebu rejea katika Surat Taha iliyo
teremka Maka katika aya ya 92 mpaka 95.
94. Akasema: Ewe mwana wa mama yangu!
Usinishike ndevu zangu, wala kichwa changu. Kwa hakika naliogopa usije sema:
Umewafarikisha Wana wa Israil, na hukungojea kauli yangu. ***
Aya hapo juu zinasema kuwa Musa alimkaripia
Harun na “Msamaria Mwema” kwa kutengeneza Ndama wa Dhahabu kwa wana wa Israeli
wakati Musa alipo kuwa katika Mlima wa Sinai. Je, haya madai ni kweli?
HEBU TUANGALIE USHAHID WA KIHISTORIA
Wa Assyria waliwashinda Wayahudi wa
Ufalme wa Kaskazini katika mwaka 722 BC (Kabla ya kuzaliwa Kristo), na kuhamia uhamishioni na kuleta watu wengine
walio tekwa kutoka falme mbali mbali, ambao baadae waliona na Wayahudi wa
kabila la chini ambao waliruhusiwa kukaaa hapo na wa Assyria.
Sasa basi, watoto wao ndio waliitwa
“Wasamaria” kwasababu walikaa katika ardhi ya Samaria ambayo iliitwa kutoka mwenye
ardhi hiyo aliye julikana kwa jina la “Shermer” (Soma 1 Wafalme 16:24) .
1
Wafalme 16: 24 Alinunua kilima cha Samaria kutoka kwa Shemeri kwa talanta
mbilia za fedha na akajenga mji juu ya hicho kilima, akiuita Samaria, kutokana
na Shemeri, jina la mmiliki wa kwanza wa kilima hicho.
Wayahudi waliwadharau Wasamaria kwa sababu mbili, moja kwa mchanganyiko wao damu “mixed race” na kwa ajili ya kuanzisha mahekalu yao wenyewe kushindana dhidi hekalu la Yerusalemu.
MASHAKA NA UTATA UNAANZIA HAPA:
Tukio la Ndama wa Dhahabu lililo tokea
karibu na Mlima Sinai kama lilivyo tajwa kwenye Quran Sura 20: 92-95 hapo juu
lilitokea miaka 1446 BC (Kabla ya Kristo), ambayo ilikuwa ni miaka 725 kabla ya
Msamaria wa kwanza kuzaliwa mwaka wa 721 BC.
Ndugu zanguni,
Leo kwa mara nyingine tena, tunaoana
jinsi Quran ilivyo jaa shaka na utata kila sehemu.
Katika aya za Quran hapo juu na
ukilinganisha na ushahid wa historia ya tukio la Wasamaria, unaona tofauti
kubwa sana tokea Wasamaria walipo anza kuzalia na tukio halisi la Ndama wa
Dhahabu. Tukio la Ndama wa dhahabu lilitokea miaka 1446 KK ambayo ni miaka 725
kabla ya Msamaria wa kwanza kuzalia, lakini Allah yeye anasema eti, kulikuwa na
Wasamaria wakati wa tukio hilo. Hivi,
kwanini Allah anashindwa kuweka takwimu zake vyema?
MASWALI:
1. Kwanini Allah
ameshindwa kusema ukweli wa tukio la Ndama wa dhahabu na kulazimisha kuwa
lilitokea wakati wa uzao wa Wasamaria?
2. Je, inawezekana kuwa
labda kuto kuwa na elimu kwa Muhammad kulisababisha Muhammad kushindwa elewa
nini Jibril alikuwa anasema?
3. Je, inawezekama kuwa
labda Jibril alipo pewa ujumbe na Allah nayeye Jibril alishindwa kumweleze
Muhammad kwa usahih?
4. Je, tunaweza iamini
Quran inayo shindwa kuweka takwimu zake kwa usahihi kuwa ni kitabu kisicho kuwa
na shaka ndani yake?
Histori ya Ndama wa dhahabu
ipo sio tu katika vitabu vya dini bali hata vitabu vya historia. Lakini katika
Quram hii habari imesemwa kwa uongo mkubwa sana.
Kama kweli Allah ndie
aliye iteremsha Taurat kwa Musa, kwanini alishindwa kusema ukweli?
Kama kweli Allah ndie
aliye iteremsha Taurat kwa Musa, je, Waislam na Allah, mnaweza tuonyesha ipo
wapi hiyo Taurat iliyo teremshwa kabla ya Quran?
Ndugu wasomaji, Quran
haikuteremshwa na Allah bali iliandikwa na watu hapa duniani, kama Waislam
wanabisha, basi watueleze kwanini Allah anashindwa kusema ukweli na kujaza
shaka kwenye Quran?
Hakika
Msingi wa Dini ya Uislam ni Allah ambaye amesha pokea sifa ya kuwa ni Baba wa
Uongo. Hebu rejea na soma hii aya kutoka Biblia kitabu cha Mungu:
Yohana
8: 44 Ninyi ni watoto wa baba yenu Ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya
baba yenu. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli maana
hamna kweli ndani yake. Asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewe kwa maana
yeye ni mwongo na baba wa huo uongo.
Biblia
imesha kujibu kuwa baba wa Uongo ni Ibilisi na husema yaliyo yake mwenyewe.
Kumbe basi, ndio maana Allah wa Waislam nayeye anasema yaliyo yake.
Nakukaribisha
kwa Mungu Mkuu ambaye yeye sio Baba wa Uongo bali ndie Muumba wa kila kitu na
alikufa kwa ajili ya dhambi zako.
Mpokee
Yesu leo na upate Uzima wa Milele.
Mungu
awabariki sana.
Max
Shimba Ministries Org.
MAX SHIMBA MINISTRIES ORG ©2015. ALL
RIGHTS RESERVED
Everyone is
permitted to copy and distribute verbatim copies of this license document, but
changing it is not allowed.
No comments:
Post a Comment