NINI MAANA YA KUOKOKA?
KUOKOKA ni lugha ya kawaida kabisa, yenye maana ya;
Kunusurika, kusalimika, kupona, kukombolewa,
kufunguliwa au kutoka katika janga au hatari fulani.Ambavyo jamii yetu maneno haya tunayatumia sana,
NINI MAANA YA WOKOVU?
Watu wengi neno hili wamelitafsiri vile wa pendavyo au
waonavyo sasa Swali hili acha lijibiwe na maandiko matakatifu, na
maneno haya yasibadilishwe kwamba ni wakati gani wa kuokoka kitendo
kikishamalizika cha kukiri kifuatacho ni uwokovu kwa mjibu wa neno, fuatilia
hapa chini,
“Kwasababu ukimkiri Yesu Kristo kwa kinywa chako ya kuwa
ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, UTAOKOKA. Kwa maana kwa moyo
mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa mtu hukiri hata KUPATA WOKOVU”. (Rum 10:9-10.)
Baada ya kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wako, ni
muhimu sana kupata mafundisho ya awali, yatakayokusaidia kujua kwa hakika,
maana ya KUOKOKA au WOKOVU; “ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa
huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa
ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu.” (Efe 4:14)
Lini unatakiwa ufanye uamuzi huu muhimu?
Hebu MUNGU na aseme nawe
kupitia maneno yake ambayo ni amina na kweli anasema:
Warumi 13:11
Naam, tukiujua wakati,
kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia; kwa maana sasa wokovu
wetu u karibu nasi kuliko tulipoanza kuamini
2Wakorintho 6:2
2Wakorintho 6:2
"Kwa maana asema,
Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia;tazama,wakati
uliokubalika ndiyo sasa; tazama siku ya wokovu ni sasa"
Biblia inaonya kuwa "tazama,wakati uliokubalika ndiyo sasa; tazama
siku ya wokovu ni sasa" yaani
wakati huu unaposoma hapa ndio wakati wako wa kutubu na kumgeukia Mungu kwa
njia ya kristo kama bado haujafanya hivyo kwani huu ni uamuzi ambao kila
mwanadamu lazima aufanye.Mungu ana kalenda yenye miaka mingi lakini kwenye
swala la kuukiri wokovu wa kristo wakati ni sasa..Ninakuomba umpe kristo maisha
yako,ili hata kama ukifa muda wowote akupokee na uishi naye milele.
WOKOVU SIO DINI
MAANA HALISI YA
WOKOVU
Wokovu ni mpango wa
Mungu mwenyewe wakumtafuta na kumkomboa Mwanadamu.
Baada ya Adam na Hawa
wanadamu wa kwanza kutenda dhambi na kuvunja uhusiano wa Mungu na Mwanadamu ,
bado Mungu aliendelea kumpenda mwanadamu na kutafuta ni kwa namna gani na kwa
njia ipi ya kurudisha uhusiano wake na mwanadamu aliyemuumba.
“kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda
ulimwengu,hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe
na uzima wa milele, Yohana 3:16”
“Kila mtu amwaminiye” hii ina maana kwamba wokovu ni kwa wale tu
watakao mwamini mwana pekee wa Mungu ambaye ni Yesu Kristo na ambao
hawajamwamini hawajaokolewa hivyo wamepotea na hawana uzima wa milele. Wokovu
ni njia pekee aliyoichagua Mungu ili kurudisha uhusiano wake na
Mwanadamu kwa Kumwamini Yesu Kristo.
Usidanganyike wala
mtu yeyote asikudanganye Wokovu unatoka kwa Mungu
mwenyewe kwa njia ya Kristo Yesu. “Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi
mtakuwa safi, nitawatakaseni na uchafu wenu wote na vinyago vyenu vyote. Nami
nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo
wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia
Roho yangu ndani yenu na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika
hukumu zangu na kuzitenda, Ezekiel 36:25-27”
“Maana hili ndilo agano nitakaloagana na
nyumba ya Israeli baada ya siku zile, asema Bwana; Nitawapa sheria zangu katika
nia zao, Na katika mioyo yao nitaziandika; Nami nitakuwa Mungu kwao , Nao
watakuwa watu wangu, kwa sababu nitawasamehe maovu yao na dhambi zao
sitazikumbuka tena, Waebrania 8:10,12” “Naye atazaa Mwana, nawe
utamwita jina lake Yesu, maana yeye ndiye atakaye waokoa watu wake na dhambi
zao, Mathayo 1:21” Hivyo mtu aliyepokea wokovu halisi wa Mungu hatendi dhambi yoyote kwani
anaongozwa na Mungu mwenyewe kwa njia ya Roho Mtakatifu na amri za Mungu kwake
sio nzito (Yohana 14:26). Anaishi maisha ya utakatifu, yanayompendeza
Mungu ( Zaburi 16:3)
MAANA HALISI YA DINI
Dini ni mpango wa
wanadamu wenyewe wa kumtafuta Mungu. Na Mungu ameukataa mpango huu Kwani
haufikii viwango anavyohitaji. “mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana
hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na
katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzuia tamaa za
mwili, Wakolosai 2:23”
“Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila
mioyo yao iko mbali nami, nao huniabudu bure, wakifundisha maf- undisho yaliyo
maagizo ya wanadamu. Mathayo 15:8-9”
Hivyo dini haiwezi
kumusaidia mtu kushinda dhambi kwani anakua hana msaada wowote wa Mungu
atajitahidi kujizuia kwa ukali lakini atashindwa. Na kwa mtu anayeshiklia dini
kwake amri za Mungu ni nzito.Mtu yey- ote anaweza
kuanzisha dini na kupata wafuasi wengi laki- ni sio wokovu kwani unatoka kwa
Mungu mwenyewe.
WOKOVU NI HAPA DUNIANI
Usikubali uongo
wowote wokovu ni hapa duniani na baada ya kufa ni
hukumu na hukumu hii itategemea uliishije hapa duniani.” Na
Kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, baada ya kufa hukumu, Waebrania
9:27”
“Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa
yaja, ambayo Watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake.Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa
ufufuo wa uzima na wale waliofanya mabaya kwa ufufuo wa hukumu Yohana 5:28-29”
Kwa hiyo maisha yetu
ya hapa duniani ndiyo yatakayoamua hukumu yetu itakavyokuwa.
Mungu amezibitisha
mwenyewe kuwa kuna Watakatifu Duniani.”Watakatifu
waliopo duniani ndio walio bora, Nao
ndio nliopendezwa nao, Zaburi 16:3”
Kataa uongo wowote
tunaokoka hapa duniani na tunaishi Maisha ya utakatifu yanayompendeza Mungu.
SALA YA TOBA
Inawezekana kabisa ya kuwa wewe
unayesoma ujumbe huu hujaokoka - yaani hujampokea Yesu Kristo ndani ya moyo
wako kama Bwana na Mwokozi wako. Lakini sasa umeona umuhimu wa kumpokea Yesu
Kristo katika maisha yako.
Naamini Roho Mtakatifu ameweka fursa
hii mikononi mwako kwa mpango maalum wa Mungu ili ufike mahali pa kutubu na
kuokoka. Inawezekana kabisa, pia ya kuwa hujawahi kuambiwa juu ya umuhimu wa
wewe kuokoka. Lakini napenda kukuambia ya kuwa ni mpango wa Mungu uokoke. Soma
Wakolosai 1:13,14 na Yohana 1:12-14 na 1 Timotheo 2:3-6 na Warumi 1:16,17 na
Yohana 3:7. Ni vigumu kuona baraka za Damu ya Yesu bila ya kuokoka.
Kwa hiyo kama unataka kuokoka -
tafuta mahali palipo na utulivu, na usome kwa sauti sala ifuatayo: (ukiweza
unaweza kupiga magoti unapoomba sala hii)
“Ee Mungu wangu ulie Mtakatifu.
Ninakuja mbele zako. Mimi ni mwenye dhambi. Naomba unisamehe dhambi zangu zote
nilizokukosea katika maisha yangu. Ninatubu kweli. Naomba damu ya Yesu Kristo
iliyomwagika msalabani kwa ajili yangu initakase sasa katika roho yangu na
nafsi yangu na mwili wangu. Nimefungua moyo wangu. Bwana Yesu Kristo
nakukaribisha ndani yangu. Ingia kwa uwezo wa Roho wako – uwe Bwana na Mwokozi
wangu kuanzia sasa na siku zote. Ahsante kwa kunisamehe na kwa kuniokoa.
Nimejitoa kwako nikutumikie katika siku zote za maisha yangu. Shetani hana
mamlaka tena juu yangu katika jina la Yesu Kristo. Amina.
Ikiwa umesoma sala hii kwa kukusudia
kabisa na kwa imani, basi wewe umeokoka na dhambi zako zimesamehewa na kusahauliwa
na Mungu sawasawa na alivyoandika katika neno lake. Damu ya Yesu iko juu yako
sasa.
Baada ya kuokoka
Unapoanza maisha haya mapya katika
Yesu Kristo nakushauri mambo yafuatayo:
1.Zungumza na Mungu kwa maombi kila
siku (Yohana 15:7)
2. Soma Neno la Mungu (Biblia) kila
siku (Matendo ya Mitume 17:11)
3.Mruhusu Roho Mtakatifu akutawale
(Wagalatia 5:16-25; Warumi 8:14-17)
4.Umtumaini Mungu kwa kila jambo
katika maisha yako (1Petro 5:7; Zekaria 4:6)
5.Usiache kukusanyika na kushirikiana
na wengine waliompokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wao kama wewe ili uimarike
zaidi (Waebrania 10:25)
Ukipenda unaweza kuniandikia kwa
anwani hii hapa chini juu ya uamuzi uliofikia leo wa kuokoka, ili tumshukuru
Mungu pamoja, na tuzidi kukuombea; na pia, tukutumie maandiko mengine ya
kukusaidia: maxshimbaministries@gmail.com.
Mungu akubariki sana
Max Shimba Ministries Org.
No comments:
Post a Comment