Friday, June 12, 2015

HIVI KATI YA ALLAH NA ISSA BIN MARYAMU NANI ALIUMBA, FUFUA WATU NA KUPONYA?

a. Isa Bin Maryam anaumba
b. Allah anaumba na wasaidizi wake.
c. Isa bin Maryam, anafufua wafu, lakini Allah na Muhammad hawakuwai fufua mtu hata mmoja.
d. Isan bin Maryam anaponya watu, lakini Allah na Muhammad hawakuwai ponya mtu hata mmoja.
Je, Kati ya Isan bin Maryam na Alla, nani ni zaidi? Hebu ungana nami katika somo hili fupi la nani zaidi kati ya Allah na Isa bin Maryam.

1.ALLAH NA WASAIDIZI WAKE!Q 7:11. Na hakika TULIKUUMBENI, kisha tukakutieni sura, kisha tukawaambia Malaika: Msujudieni Adam.Basi wakasujudu isipo kuwa Iblisi, hakuwa miongoni mwa walio sujudu.
Kama ni kweli kuwa Allah hana wasaidizi, mbona anatumia wingi? Hivi Allah na akina nani hao wanaumba? Hivi Allah alikuwa anaongea na nani hapo?

2.ISSA BIN MARYAM PEKE YAKE!Q 3:49. Na ni Mtume kwa Wana wa Israili kuwaambia:Mimi nimekujieni na Ishara kutoka kwa Mola Mlezi wenu,ya kwamba NAKUUNDIENI kwa udongo kama SURA ya ndege.Kisha nampuliza anakuwa ndege kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na ninawaponesha vipofu wa tangu kuzaliwa na wakoma, na ninawafufua maiti kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ninakwambieni mnacho kila na mnacho weka akiba katika nyumba zenu.Hakika katika haya ipo Ishara kwenu ikiwa nyinyi ni wenye kuamini.
Isan bin Maryam yeye anaumba kama ilivyo thibitishwa kwenye aya hapo juu. Zaidi ya hapo, Isa Bin Maryam anaponyesha wagonjwa na kuwafumbua macho vipofu.
Isa bin Marya anafufua na wafu. Je, mbona Allah hakuwa fufua wafu kwa kupitia Mtume Muhammad?
Je, mbona Allah hakuwai ponya watu kwa kupitia Mtume Muhammad?
Hivi, kuna muujiza wowote ule ulio fanywa na Allah au Muhammad au Jibril?

KWA AYA HIZO NAULIZA:1.Sifa ya kuumba ni ya nani? Kama ni ya Mungu,Je,Issa bin Maryam ni Mungu?
2. Nataka kujua ni watu gani waliumbwa na Allah na ni watu gani waliumbwa na Issa bin Maryam ?
3.Kwa kuwa Waislamu wanasema Issa ni Yesu,si kwamba tayari kwa aya hiyo tayari wanakubali kuwa YESU NI MUNGU?
4.Kati ya Issa na Muhamaad nani MBORA wa Viumbe vyote? Issa kaumba viumbe vyote,kafufua wafu,kawafanya vipofu waone lakini huyu Muhamaad hakuumba,hakufufua,hakuwaponya vipofu !


TOWENI ''ILIMU'' BILA MATUSI!
Kumbuka dini zote zinakataza matusi!

UISLAMU:
Amesema Muhamaad: "Hakika muumini wa kweli hawi ni mwenye kuwatuhumu watu, wala KUWALAANI watu, wala hawi na maneno MACHAFU" {Musnadu Ahmad juzu ya 1 ukurasa 416, hadith nambari:3948}

UKRISTO:
(Waefeso 4:31)-Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na MATUKANO yaondoke kwenu,pamoja na kila namna ya ubaya.

KUNA HUKUMU KWA WATUKANAJI!
(1Wakorintho 6:9-10)-Au hamjui wadhalimu hawataurithi Ufalme wa Mungu?Msidanganyike;Waasherati hawataurithi Ufalme wa Mungu wala wevi,wala walevi,wala WATUKANAJI.

ISIPOKUWA KWA WALE AMBAO SAA ZOTE WAMEJAMBIWA MIDOMONI,WENGINE TUWE WASTAARABU!

Abu Huraira (r.a) amesimulia kuwa: Mtume (s.a.w) amesema, Ye yote mwenye kutukana, basi huyo amejambiwa na Shetani katika Mdomo wake." (Fat'hul Baary J. 10, Uk. 176)
Karibu kwa Yesu Kristo aliye umba, fufua wafu, ponya wagonjwa na mwenye uwezo wa kukusamehe dhambi zako.
Mungu anawapenda sana
Okoka leo na upate uzima wa milele.
Max Shimba Ministries Org

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW