SEHEMU YA 1
UTANGULIZI:
Hii ni sehemu ya ushuhuda wangu, ambao nitaeleza ni sababu gani ambayo ilipelekea niachane na uislamu, na hatimae kuwa Mkristo, Katika DVD ya ushuhuda wangu, nilieleza kwa kifupi, na mengi sikuyasema, nilieze hasa harakati zangu katiks mihadhara, ila hapa nitachumbua mengi zaidi.
Nimezaliwa miaka 27 Iliyopita, katika JIJI LA MWANZA (Rock city) Jina langu ambalo nilikuwa nalitumia katika uislamu, ni Aboubakar, nimesoma Madrasa Pale THAQAAFATUL ISLAMIYA, Mwanza, karibu na Shule ya msingi Mirongo, shule hiyo imepakana na Lake Secondary School, pia na Ipo karibu na hospitali ya Seketule.
Miongoni mwa walimu wangu wa madrasa, ni:
Nimezaliwa miaka 27 Iliyopita, katika JIJI LA MWANZA (Rock city) Jina langu ambalo nilikuwa nalitumia katika uislamu, ni Aboubakar, nimesoma Madrasa Pale THAQAAFATUL ISLAMIYA, Mwanza, karibu na Shule ya msingi Mirongo, shule hiyo imepakana na Lake Secondary School, pia na Ipo karibu na hospitali ya Seketule.
Miongoni mwa walimu wangu wa madrasa, ni:
Ramadhani Maganga
Ustadh Kikatani
Ustadh Hassan Lolo.
Ustadh Kaisy
Ustadh Shekue.
Ustadh Kikatani
Ustadh Hassan Lolo.
Ustadh Kaisy
Ustadh Shekue.
Pia nilisoma Madrasa iliyopo TAQWA, maeneo ya Ghana, chini ya Sheikh Abdallah Panya, pia Ghana mtaa wa kifua Wazi, kwa Ustadh, Thuqmal bin Hussein (Huyu ni ustadh aliyekuwa ana diri na Elimu za dua za kafara, kuchinja mbuzi, kuku na kisha kutuchukya kwenda kufanya zindiko ndani ya nyumba, kwa kutumia vitabu mbali mbali vya kiislamu) Nitaeleza habari zake katika mwendelezo wa ushuhuda wangu....
Katika harakati zangu ambazo nilizifanya katika uislamu, ni ushiriki wa harakati za ujenzi wa Misikiti VIJIJINI, michango ya ujenzi huo ulikuwa ukifanyika ndani ya msikiti wa IJUMAA Mwanza, ambapo michango hiyo, ilikuwa ikifanyika siku ya ijumaa, na J'Mosi au J'pili tunakutanika na kuelekea vijijini, miongoni mwa vijiji hivyo, ni MSIKITI Uliopo Kigongo Fery, (Kwenye Kivuko cha Fery kwa waendaji wa Sengerema, Geita na Bukoba) Unaanza Usagara, pia Misungwi, tulikuwa napo tukifanya ujenzi wa misikiti pia, kubwa zaidi ni Msikiti wa MISASI, huo ni mmoja wa misikiti mkubwa ambao tulichukua muda kuujenga, Mwangalizi wake anajulikana kwa jina la OSAMA kwa Wakazi wa Misasi wanaufahamu, upo nyuma ya Center ya MISASI,
Kuna baadhi ya Waarabu ambao walikuwa wakitoa magari yao aina ya FUSO, kwa ajili ya kutubeba, na kutupeleka huko, na pia baadhi ya vijana, tulikuwa tunapatiwa kiasi cha fedha, kwa ajili ya kuwarubuni mabinti wa Kikristo huko vijini, kwa kuwatongoza, na kuwapa ahadi ya kuwaoa, pindi watakaposilimu na kuwa waislamu, na njia kubwa zaidi ambayo ilikuwa ni njia rahisi zaidi ni kuwajaza Ujauzito (Hapo unakuwa umeshamnasa kirahisi) kwani utakataa kumtunza ikiwa bado yu ngali Mkristo, Mabint ambao hawakuwa na msimamo kiukweli walinaswa na mtego huo, kuna jamaa yetu mmoja Anaitwa Rashid, yeye alimeza Suratul Yusuph, (Sura ya 12 ndani ya Quran) kwa njia ya KOMBE, na kusomewa dua nzito, Wanawake wampende kama alivyopendwa na Yusufu na mke wa Firauni, Wanawake hawakuthubutu kumkataa, baadae alikuja kuwa Mfanya mihadhara wa Mwanza, na (kwa sasa ni marehemu, amekufa kwa H.I.V ) Nami nikamuomba anifundishe njia hiyo Ili nipate kuwanasa mabinti wa Kikristo kwa urahisi, Akaniambia........ITAENDELEA
No comments:
Post a Comment