Tuesday, May 26, 2015

Neema katika Injili

Utangulizi

Ukurasa huu umeandikwa katika njia ya kusudi ya habari za Isa (Yesu) kwa Waislam, kutokana na mtizamo wao wa Kikuran. Ni injili ya Yesu (Injil) inayo elezwa kwa Waislam.
Katika Injili Yesu anahusu dhabihu ya Mungu kwa ajili ya dhambi zetu.

Karamu ya sadaka

Kuelewa sadaka ni ya muhimu kuangalia katika historia kuhusu sikukuu ya sadaka (Aid-Al-Adha) ambayo ni sikukuu ya Waislam. Sherehe wakati Mungu alimwita Ibrahimu (Ibrahim) kutoa mwana wake kama sadaka.
Hii inatuambia ilivyo muhimu sana kuhusu asili ya sadaka ya kweli kwake Mungu. Mwana - kondoo alikufa badala ya mtu ili kwamba wawe huru tokana na hukumu ambayo ingekuja juu yake. Kifo cha mwana - kondoo kilikubalika na Mungu kama toleo la sadaka (Fidia) katika nafasi ya yule aliye hukumiwa kifo. Mwana angetolewa tena maana mwana- kondoo alichukua mahala pake. Hangepata hii hukumu tena sababu Mungu amejipatia Mwenyewe mwana- kondoo wa sadaka iliyoweza kukubalika kama toleo machoni Mwake. Kuran inasema hivyo pia. Fidia inamaanisha ʼkukomboa toka mateka, utumwa, au kama hiyo, kwa kulipa gharamaʼ. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu alivyofanya kumwokoa mwana wa Ibrahimu toka kwenye hukumu iliyo kuwepo.
Uko wewe katika hali moja kama hivi ndivyo alivyokuwa mwana wa Ibrahimu. Wewe ni mwenye hatia aliyekufa. Kwa nini?
Hauwezi kujiokoa mwenyewe. Kila matendo mema, hayawezi kukuhakikishia kuvuka kwa usalama kuingia katika Paradiso (Pepo). Katika hatua hii, utaweza hakika kusema kwamba hauna hatia, sababu unakiri dhambi zako kwake Mungu. Walakini, Kuran inasema:
ʼNa lau kuwa kila nafsi iliyo dhulumu inamiliki kila kiliomo duniani, bila ya shaka ingelitoa vyote kujikombolea. Na watakapo iona adhabu wataficha majuto. Na patahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatadhulumiwaʼ (Kuran 10:54).
Katika maneno mengine, iwapo unaweza kumiliki ulimwengu wote na umtolee Mungu kama dhabihu ya dhambi zako, iwapo haiwezi kutoa tambiko la dhambi zake. Uko katika hali moja kama mwana wa Ibrahimu, una hatia katika kifo.

Mwana kondoo wa Mungu

Walakini iko wapi toleo la dhambi zake? Je kuna uwezekano wa Mungu kutoa sadaka kwa ajili ya dhambi zako?

Ndiyo, Mungu anayo. Yohana Mbatizaji (Yahya Ibn Zakeria) alikuwa mtangulizi wa masihi alipomwona Yeye mara ya kwanza. Alisema:
Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu! (Yohana 1:29).
Masihi anadhihirishwa katika Kuran kama asiye na kosa (Kuran 19:19). Muhammad katika kulinganisha, anaambiwa kuomba msamaha wa dhambi zake (Kuran 40:55-57;47:19-21;48:2). Masihi apaswa kutolewa sadaka. Katika uhiari wake. Alijisalamisha kwa mauti. Alafu amefufuka kutoka wafu. Yeye yuko Mbinguni. Na atarudi duniani. Ni lazima tumkabili adui: mauti. Manabii wote walikufa na hivyo hivyo kwako na mimi. Pia Yesu alikufa:
Wakasema katika (kukufuru), ʼSisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu - nao hawakumuuwa wala hawakumsulubisha, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini. Bali Mwenyezi Mungu alim- tukuza kwake, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikimaʼ (Kuran 4:157-158).
Hii haituambii sisi kwamba Kristo hakusulubiwa. Hii inakana tu madai ya kiburi cha Wayahudi kwamba wao ndio walimwua Yeye. Siyo wao.Iliweza tu kuonekana .Ili inaonekana kama hivyo ndivyo ilivyokuwa. Ukweli wa mambo ni kwamba Mungu mwenyewe alimwamuru Yesu kwa hiyari kutoa maisha yake. Ilikuwa ni mpango na makusudi ya milele ya Mungu kulingana na maneno ya manabii.[17]
Yesu peke yake alishinda mauti. Na yeye peke yake ndiye aliye hai miongoni mwa manabii wote. Yasikilize maneno yake mwenyewe:
Mimi ni Yeye aliye hai, niliyekuwa nimekufa Na tazama, ni hai milele na milele! (Ufunuo 1:18).
Pia:
Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye Mimi, hata akifa atakuwa anaishi (Yohana 11:25).

Masomo zaidi

Kwa maombi ukisoma Injili, Rafiki yangu. Katika haya nalijifunza ya kwamba dhambi zangu zinaweza kusamehewe katika maisha haya. Na sasa nina uhakika wa kufika mbinguni baada ya kufa. Yesu ndiye njia, na Kweli na Uzima (Yohana 14:6).Hakuna ajaye kwa Mungu ila ni kwake Yeye. Kumbuka aliyo ya sema:
Ye yote anayesikia maneno Yangu na kumwamini Yeye aliyenituma, anao uzima wa milele, naye hatahukumiwa, bali amepita kutoka mautini, na kuingia uzimani (Yohana 5:24).
Unaweza kukiri kwamba wewe ni mwenye dhambi na kwamba wewe unataka kumpokea Yeye ili dhambi zako zioshwe?

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW