Wakristo wamo ndani ya Korani, na mara nyingi wanaitwa “Watu wa Kitabu kile” Huu ni utambulisho wa watu walioyapokea na kuyaamini maandiko yaliyotangulia.
1. Korani huwabariki Wakristo:
“Hakika utawakuta walio shahidi kuliko watu katika uadui kwa walioamini Mayahudi na washirika. Na utawakuta walio karibu mno kwa mapenzi wale wanaosema sisi ni manasara. Hayo ni kwa sababu japo miongoni mwao makasisi na wamonaki. Na kwa sababu wao hawafanyi kiburi” (Korani 5:82).
“Enyi mlioamini kuwa ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu, kama walivyosema Isa bini Mariamu kuwaambia wanafunzi wake nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Basi taifa moja la Wana wa Israel liliamini na taifa linguine lilikufuru. Basi tutawaunga mkono walioamini dhidi ya maadui zao wakawa wenye kushinda" (Korani 61:14).
"Semeni ninyi: tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyotelemshiwa sisi, na yaliyotelemshwa kwa ibrahimu na Ishmaili na Isihaka na Yakobo na wajukuu zake, na waliyopewa na Musa na isa, na pia waliyopewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao mlezoi. Hatutafautisha baina ya yeyote katika hao. Na sisi tumesilimu kwake. Basi wakiamini kama mnavyoamini ninyi itakuwa kweli wameongoka. Na wakikengeuka basi wao wamo katika upinzani tu. Na Mwenyezi Mungu atakutosheni kukukingeni shari yao. Na yeye ndiye Msikizi, Mjuzi" (Korani 2:136-137).
2. Korani inawaonya baadhi ya Wakristo:
Pia kuna maonyo katika Korani dhidi ya Wakristo, wanaoyatilia shaka mambo yale yanayotendeka katika Biblia watu wale wanaomfuata Yesu Kristo.
“Wote hao si sawasawa. Miongoni mwa watu wa Kitabu wamo watu waliosimama barabara wanaosoma Aya za Mwenyezi Mungu nyakati za usiku …. Na pia wanasujudu. Wanamuamini Mwenyezi Mungu siku ya Mwisho. Na wanaamrisha mema na wanakaza maovu wanakimbilia katika mambo ya kheri. Na hao ndio miongoni mwa watenda mema. Na kheri yoyote wanayoifanya hawatanyimwa malipo yake. Na Mwenyezi Mungu anawajua wacha Mungu" (Korani 3:113-115).
"Na lau kuwa wangeliishika Taurati na Injili na yote yaliyotelemshwa kutokana na Mola wa Mlezi. Basi hapana shaka wangelikula vya juu yao na vya chini ya miguu yao. Wapo watu miongoni mwao waliosawa lakini wengi wao walio sawa lakini wengi wao wanayoyafanya ni mabaya” (Korani 5:66).
3. Korani inasema Wakristo wanaenda Paradiso:
Hatimaye Korani inasema kwamba Wakristo wanaoiamini Biblia, na Kufanya Uanafunzi wanaenda Paradiso.
“Na wale walioamini na wakatenda mema hao ndio watu wa peponi na humo watadumu” (Korani 2:82).
“Hakika wanaoamini, na Mayahudi na Wakristo na Wasabai. Yeyote atakayemuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na akatenda mema, basi watapata malipo yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwako hofu juu yao wala hawatahuzunika" (Kurani 2:62, 5:69).
Kwa mujibu wa mtazamo wa Kurani, Yesu alisema “Mkristo aliye makini haogopi kitu, ndiye anayesifiwa.
“Ninyi mnayachunguza maandiko mkidhani yakuwa ndani yake mna uzima wa milele, maandiko haya ndio yanayonishuhudia mimi" (Yohana 5:39).
Wakati Uislamu ukitafuta na kutokuwa na uhakika, Mkristo ana amani na uhakika juu ya kwenda Paradiso.
No comments:
Post a Comment