Tokea
Dunia ianze, hapajawai toke Mtu yeyote alieishi kama Yesu Kristo. Yesu ni mtu
wa maana sana ambaye ni Mwokozi, Mungu katika Mwili “Emanueli” (Isaya 9:6). Yesu
sio Nusu Mungu na Nusu Binadamu kama watu na au imani nyingi zinavyo sema. Yesu
yeye ni Mungu na ni Binadamu kwa wakati mmoja. Kwa maneno mengine, Yesu alikuwa
na asilia Mbili tofauti ambazo ni Mungu na Binadamu kwa wakati mmoja.
Biblia
inasema kuwa, Yesu ni “Neno” ambaye ni Mungu na alikuwa kwa Mungu na akafanywa
kuwa Mwili na kuishi nasi, soma Yohana 1:1 na 14. Hii inamaanisha kuwa, mtu
huyu mmoja ambaye ni Yesu alikuwa ana asilia mbili za Mungu na Binadamu.
Hii
asilia ya Mungu haikubadirika pale ambapo “NENO” lilipo kuwa Mwili (Yohana 1:1,
14). Badala yake, Neno liliunga ubinadamu (Wakolosai 2:9). Hivyo basi, Umungu
wa Yesu Kristo haukuharibika na au badirika. Zaidi ya hapo, Yesu hakuwa mtu tu
ambaye alikuwa na Mungu ndani yake au Mtu aliye fanya kazi ya Mungu pekee, la
hasha, Yesu ni Mungu katika Mwili na ni sehemu ya Pili katika Utatu Mtakatifu.
Biblia inatuambia katika Waebrania 1 aya
ya 3 kuwa: Mwana ni mng’ao wa
utukufu wa Mungu na mfano halisi wa nafsi Yake, akivihifadhi vitu vyote kwa
neno Lake lenye uweza. Akiisha kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi aliketi
mkono wa kuume wa Ukuu huko mbinguni. Hivyo basi, asilia hizi mbili za Yesu
Kristo haziwezi kuchanganywa (Eutychianism), vile vile haziwezi kuwa pamoja na
kuwa Mungu-Mtu (Monophysitism). Hizi asili mbili ni tofauti na zinajitemea na wakati
huohuo ni moja katika Yesu (person of Jesus). Huu muungano unaitwa Hypostatic
Union.
Jedwari lifuatalo
litakusaidia uone hizi asilia mbili za Yesu Kristo:
MUNGU
|
BINADAMU
|
Yesu anaabudiwa (Matayo. 2:2, 11; 14:33)
|
Yesu anamwabudu Mungu Baba (Yohana 17)
|
Yesu anaitwa Mungu (Yohana 20:28; Waebrania 1:8)
|
Yesu anaitwa Mtu/Binadamu (Marko 15:39; Yohana
19:5)
|
Yesu aliitwa Mwana wa Mungu (Marko 1:1)
|
Yesu aliitwa Mwana wa Adam (Yohana 9:35-37)
|
Anaombwa/prayed(Matendo ya Mitume7:59)
|
Anamwomba Mungu Baba (Yohona 17)
|
Yesu hana dhambi/sinless (1 Petro. 2:22; Waebrania
4:15)
|
Yesu alijaribiwa (Matayo. 4:1)
|
Yesu anafahamu kila kitu (Yohana 21:17)
|
Yesu alikuwa na Hekima (Luka 2:52)
|
Yesu anatoa uzima wa milele (Yohana 10:28)
|
Yesu Alikufa (Rom. 5:8)
|
Adhama zote za Mungu zipo ndani ya Yesu (Wakolosai
2:9)
|
Alikuwa na Mwili na Mifupa (Luka 24:39)
|
USHAHIDI ZAIDI WA
ASILIA MBILI YA YESU
Mafundisho ya muungano
wa Hypostatic ni ya “communication idiomatum” (Ni maneno ya Kilatini
“Communication of properties”). Haya ni mafundisho ya adhama mbili za Yesu
Kristo za Mungu na Binadamu zote zipo ndani ya Yesu Mtu “person of Jesus”. Hii
inamaanisha kuwa, binadamu Yesu alikuwa na haki ya kusema kuwa “Alikuwa na
utukufu na Baba Mungu kabla ya dunia kuumbwa soma Yohana 17:5), vile ile kudai
kuwa alitoka Mbinguni (Yohana 3:13), na
kudai kuwa alikuwa kila mahalai “omnipresence (Matayo 28:20). Haya madai yote
ya Yesu ni adhama za Mungu na kuwa yeye Yesu alikuwanayo.
Moja ya Makosa makubwa
sana yanayo fanywa na wasio Wakristo ni kushindwa kwao kuelewa kuwa Yesu
alikuwa na ASILIA MBILI. Kwa mfano,
Mashahidi wa Yehova wao wanamwangali Yesu kama Binadamu na kupuuza adhama
zake za Umungu. Mara zote wao hutumia zile aya ambazo zinakiri Ubinadamu wa
Yesu na kuzipambanisha na aya ambazo zinasema kuwa Yesu ni Mungu. Kwa upande
mwingine, Masayantisti wa Kikristo wao hufanya kinyume chake. Wao wana angalia
zaidi upande wa Yesu ni Mungu na kusahau kuwa, Yesu alikuwa Binadamu vile vile.
Ili kumwelewa Yesu
vyema, basi kila mafundisho ambayo yanamuhusisha Yesu, hayana budi kuzumgumzia
Yesu kama Mungu na Yesu kama Binadamu. Hizo asilia Mbili ni zake. Kumbe ndio
maana Yesu katika Luka 2:52 inasema: Naye Yesu akakua katika hekima na
kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.
Na wakati huo huo alikuwa kila kitu “omniscient” Soma Yohana 21:17. Yesu ni
Neno la Mungu aliye kuwa Mwili/Binadamu (Yohana 1:1, 14).
Zaidi ya hapo, Biblia
inamhusu Yesu (Yohana 5:39. Mitume wote walimtabiri Yesu (Matendo ya Mitume
10:43). Mungu Baba anatoa ushahidi kuhusu Yesu, Soma Yohana 5:37; 8:18. Roho
Mtakatifu naye anato Ushahidi kuhusu Yesu, Soma Yohana 15:26. Kazi zake Yesu
nazo zinashuhudia kuhusu Yesu Soma Yohana 5:36; 10:25. Makundi ya watu nayo
yanashuhudia kuhusu Yesu, Soma Yohana 12:17. NA YESU anajishuhudia mwenyewe
Soma Yohana 14:6 ; 18:6.
Kuna aya nyingine
nyingi ambazo zinamshuhudia Yesu kuwa ni Mungu nazo ni
Yohana 10:30-33;
20:28; Wakolosai. 2:9; Wafilipi. 2:5-8; Waebrania 1:6-8; na 2 Petro. 1:1.
1 Timoteo 2:5 inasema , " Kwa maana
kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani,
mwanadamu Kristo Yesu, 6.
aliyejitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wanadamu wote, jambo hili
lilishuhudiwa kwa wakati wake " Hivi sasa, kuna Mtu Mbinguni ambaye yupo katika kiti cha
Enzi. Yeye ni Mpatanishi wetu kwa Mungu Baba (1 Yohana 2:1). Ni Mwokozi wetu
(Tito 2:13). Ni Bwana wetu (Warumi 10:9-10) Huyo Mtu anaitwa YESU.
Hakika Yesu Ni Mungu.
Kwa Maswali zaidi wasiliana nasi katika maxshimbaministries@gmail.com
Imeletwa kwenu na Max Shimba
Kwa Max Shimba Ministries Org.
@2015, April.
No comments:
Post a Comment