Ndugu msomaji;
Je, unamfahamu Roho Mtakatifu?
Je, Roho Mtakatifu ni nani kwako?
Katika kijarida hiki kifupi, ningependa
tumzungumzie Roho Mtakatifu kama alivyo semwa na kutajwa katika Biblia
Takatifu.
Kuna utatanishi mkubwa sana na maelezo
mengi sana kuhusu Roho Mtakatifu. Kuna imani zingine kama Mashahidi wa Yehova,
wao husema kuwa Roho Mtakatifu ni Nguvu Fulani na au ni uwezo wa Mungu katika
kufanya mambo. Wengine kama Waislamu, wao husema kuwa Roho Mtakatifu ni Malaika
Gabriel. Wengine husema kuwa Roho
Mtakatifu ni sehemu ya Nafsi ya Mungu. Lakini, Biblia inasema nini kuhusu Roho
Mtakatifu. Ni vyema tujifunze kuhusu Roho Mtakatifu kwa kutumia aya za Biblia
na sio theologia na akili zetu.
ROHO MTAKATIFU NI MUNGU
Tuanze kwa ushaidi wa aya: Matendo ya Mitume
5:3-4. Petro akamwambia, “Anania, mbona shetani ametawala moyo wako kiasi cha
kukubali kumdanganya Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata? 4 Kabla hujauza hilo
shamba lilikuwa mali yako. Na hata baada ya kuliuza, fedha ulizopata zilikuwa
zako. Kwa nini basi umeamua moyoni mwako kufanya jambo kama hili? Ujue
hukumdanganya mtu ila umemdanganya Mungu.”
Katika aya hizo hapo juu, Petro anapambana na
anania aliyemdanganya Roho mtakatifu na anasisitiza yakuwa “hukumdanya mtu bali
Mungu. Kwa maana nyingine, Petro alikuwa anamwambia Anania kuwa, kumdanganya
Roho Mtakayifu ni sawa na kumdanganya Mungu. Huu ni uthibitisho wa kwanza kuwa,
kumbe Roho Mtakatifu ni Mungu.
ROHO
MTAKATIFU YUPO KILA MAHALI
Hebu tuangalie kama Roho Mtakatifu ana adhama za
Mungu aliye hai. Sifa, moja ya Mungu ni kuwa, yeye yupo kila Mahali. Je, Roho
Mtakatifu anayo hii sifa ya kuwa kila mahali? Fungua Zaburi 139:7-8, “nitaenda
wapi nijifiche na Roho? ama nitakimbilia wapi mbali na uwepo wako? Nikipanda
juu mbinguni, huko uko; nikifanya malazi yangu kuzimu, tazama uko huko,”
Daudi anatuambia kwa kupitia Zaburi kuwa, huwezi
kumkimbia Mungu. Daudi anamtaja Mungu na au anamwita Mungu kuwa ni Roho. Hii
sifa ya kuwa kila mahali ni ya Mungu pekee, na katika Zaburi 139: 7-8, tumesoma
kuwa, Roho Mtakatifu yupo kila mahali.
Tuendele na ushahidi zaidi wa kuwa kila mahali; katika
Wakorintho wa Kwanza, hapa Mtume Paulo anasema yafuatayo 1 Wakorintho 2 aya ya
10 Lakini Mungu ameyajulisha kwetu kupitia Roho wake mtakatifu. Kwa kuwa Roho
huyachunguza mambo yote, naam, mambo ya siri ya Mungu. Kwa maana ni nani
ayajuaye ya mwanadamu isipokuwa roho ya mwanadamu inayokaa ndani yake? Vivyo
hivyo, hakuna ajuaye mambo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu.”
Kama Roho Mtakatifu anafahamu kila kitu kilicho
ndani ya Binadamu, ambao wametapakaa Duniani kote, basi kitendo cha kuwa kila
mahali kwa wakati mmoja ni Mungu pekee ndie aliye na huo uwezo.
Tuendelee kwa Ushihidi mwingine katika aya hiyo
hiyo ya 10 ya Wakorintho wa kwanza Sura ya 2. Roho Mtakatifu ni Mungu kwasababu
ana akili, hisia, na mapenzi yake.
Katika Wakorintho wa kwanza 2:10 tumesoma kuwa
Roho Mtakatifu hufikiria na hujua siri iliyo ndani yako. Hii sifa ya kufikiria
na kujua, inavunja hoja ya Mashahidi wa Yehova kuwa Roho Mtakatifu ni “Nguvu”.
Nguvu haina uwezo wa kufikiria wala kufanya maamuzi.
ROHO
MTAKATIFU UHUZUNIKA
Katika Waefeso 4:30 inasema “Na msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu ambaye ni mhuri wenu
wa uthibitisho kwa siku ya ukombozi”
Unaweza jiuliza, ni kivipi unaweza kumhuzunisha
Roho Mtakatifu? Kama Roho Mtakatifu angekuwa ni “Nguvu –Energy” kama anaitwa na
Mashahidi wa Yehova, je, ni kivipi Nguvu ipate huzuni? Unapo tenda dhambi huku
Roho Mtakatifu akiwa ndani yako kama alivyo fanya “Anania – Matendo ya Mitume
5:3-4” Unamhuzunisha Roho Mtakatifu maana yeye hujua yote na akuna siri ambayo
haifahamu. Hii sifa ya kumhuzunisha Roho Mtakatifu ina pinga madai ya Mashahidi
wa Yehova na inapinga madai ya Waislam yanayo kama Uungu wa Roho Mtakatifu.
ROHO
MTAKATIFU HUTUOMBEA
Warumi 8:26-27 Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
26 Hali kadhalika Roho hutusaidia katika
udhaifu wetu. Kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo, lakini Roho mwenyewe
hutuombea kwa uchungu usioelezeka kwa maneno. 27 Na Mungu ambaye ana chunguza mioyo yetu
anafahamu mawazo ya Roho kwa maana Roho huwaombea watakatifu kufuatana na
mapenzi ya Mungu.
Katika aya hapo juu, tumesoma kuwa, Roho
Mtakatifu anatuombea na kutusaidia katika udhaifu wetu. Hii sifa ya upendo usio
na kipimo ni ya Mungu peke yake. Zaidi ya hapo, tunasoma kuwa, Mungu
anachunguza mioyo yetu kwa kupitia Roho Mtakatifu. Kumbe basi, Roho Mtakatifu
anafahamu mapenzi ya Mungu kwako. Hii sifa ya Roho Mtakatifu kuwa na uwezo wa
kufahamu nini Mungu anawaza inamfanya Roho Mtakatifu na yeye awe Mungu. Hakuna
mwenye uwezo wa kufahamu mawazo ya Mungu, isipokuwa Mungu.
ROHO
MTAKATIFU HUFANYA MAAMUZI YAKE
Roho mtakatifu hufanya maamuzi kutokana na
mapenzi yake mwenyewe (Wakorintho wa kwanza 12:7-11).
1 Wakorintho 12:7-11Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
7 Roho Mtakatifu hudhi hirishwa kwa kila
mtu kwa faida ya wote. 8 Maana mtu
mmoja hupewa neno la hekima na huyo Roho, na mwingine hupewa neno la ufahamu
kutoka kwa Roho huyo huyo. 9 Mtu mwingine hupewa imani na huyo Roho
na mwingine karama za kuponya. 10 Huyo huyo Roho humpa mwingine uwezo wa
kufanya miujiza, mwin gine unabii, mwingine uwezo wa kutofautisha kati ya roho
mbalim bali, mwingine aina za lugha na mwingine uwezo wa kutafsiri lugha. 11 Lakini ni Roho huyo huyo mmoja
anayefanya haya yote, naye hugawa karama kwa kila mtu, kama yeye mwenyewe
apendavyo.
Katika
Wakorintho wa kwanza hapo juu, tumesoma kuwa, Roho Mtakatifu ndie anaye toa
zawadi/karama ya hekima, ufahamu, imani, kuponya, miujiza, unabii, nk. Hii sifa
ya kutoa hizi Karama ni ya Mungu, lakini hapa kwenye Wakorintho tumesoma na
kugundua kuwa, Kumbe Roho Mtakatifu ndie anaye toa hizi karama za Mungu. Hivyo
basi, kwa kuwa Roho Mtakatifu ndie anaye toa hizi karama za Mungu, hufanya
hivyo kwa kuwa yeye ni Mungu na hizo karama ni zake.
ROHO
MTAKATIFU ANAFAHAMU MAMBO YOTE
Kama ambavyo Mungu anafahamu mambo yote na
anaweza yote, vivyohivyo Roho mtakatifu ni Mungu na anauwezo wa huohuo wa
kufahamu yote. Kama Mungu, Roho mtakatifu anaweza kufanya kazi ya msaidizi na
mshauri kama vile Yesu kristo aliyevyoahidi kuwa atakuja kufanya (Yohana
14:16,26; 15:26).
Yohana 14:26Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
26 Lakini yule
Msaidizi, yaani Roho Mtakatifu, ambaye Baba yangu atamtuma kwenu kwa jina
langu, atawafundisha mambo yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
Katika Yohana hapo juu, tunajifunza
kuwa, Roho Mtakatifu yupo nasi kila siku na anaishi ndani yetu. Huu uwezo wa
kuishi ndani yetu na kuwa kila mahali, na kufahamu yote ambayo Yesu aliyo
tuambia na kutukumbusha, huu uwezo ni wa Mungu na unamfanya Roho Mtakatifu kuwa
Mungu.
HITIMISHO
Roho Mtakatifuni Mungu, mwenye nguvu zote,
maarifa yote, anayepatikana kila mahali. Yeye pia anayo nafsi na kwa hiari yake
ameamua kuishi ndani ya mwili wa mwanadamu kwa kuzingatia mgawanyo wa majukumu
waliyokubaliana yaani nafsi ya Mungu Baba, Mungu Mwana(Yesu)
na Mungu Roho Mtakatifu. Kazi/lengo kubwa la ujio wake ni kuwa Msaidizi
wa mwanadamu kwenye
ulimwengu huu wa mwili, ili kumsaidia kuishi katika mapenzi ya Mungu.
Katika huduma yake
Max Shimba Ministries
@February 10, 2015
New York, NY 10019
No comments:
Post a Comment