Thursday, September 25, 2014

Bibilia inasema nini kuhusu ndoa?

Mwanzo wa ndoa umenakiliwa katika Mwanzo 2:23-24: “Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu na nyama katika nyama nyangu, basi ataitwa “mwanamke,” kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.” Mungu alimuumba mwanamume na kisha baadaye akamuumba mwanamke ili amkamilishe mwanamume. Ndoa “iliwekwa” na Mungu kwa sababu kuwa “si vema huyo mtu awe peke yake” (Mwanzo 2:18).

Neno “msaidizi” limetumika kumwelezea Hawa katika Mwanzo 2:20 lamaanisha “kumzunguka, kumkinga, kumsaidia.” Hawa aliumbwa awe kando ya Adamu kama “nusu yake” awe msaidizi wake. Mwanamume na mwanamke, wakati wameoana wanakuwa “mwili mmoja.” Huu umoja umedhihirishwa mara nyingi katika tendo la ndoa. Agano Jipya inaongeza onyo kuhusu umoja huu. “Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe” (Mathayo 19:6).

Kunayo nyaraka nyingi za mtume Paulo zenye zinahusu ndoa na jinsi Wakrito wanastahili kuwa katika ndoa. Ukurasa mmoja ni 1 Wakorintho 7, na mwingine ni Waefeso 5:22-33. Tulijifunza pamoja, hizi kurasa mbili zinatoa kanuni za kibibilia ambazo zinaunda mwongozo wa ndoa ambayo ni ya kumpendeza Mungu.


Ufahamu wa Waefeso has ndio wa uzito hasa kuhusu ndoa yenye ufanisi. “Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili” (Waefeso 5:22-23). “Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake” (Waefeso 5:25). “Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa” (Waefeso 5:28-29). “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mana yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja” (Waefeso 5:31). 

Wakati mme Mkristo na mke Mkristo wanaitumia kanuni ya Mungu, ndoa ya Kibibilia hutokea. Ndoa ambayo imeanzishwa kwa misingi ya Bibilia ndio ile ambayo iko wastani, Kristo akiwa kichwa cha mwanamume pamoja na mkewe. Dhana ya kibibilia kuhusu ndoa ni umoja kwa wanandoa ambayo yaleta picha ya umoja kati ya Kristo na Kanisa.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW