Wednesday, April 16, 2014

YESU ALIISHI KABLA YA DUNIA KUUMBWA


Yohana 17:5 Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako. 

Katika aya hapo juu tunasoma kuwa Yesu aliishi kabla ya kuumbwa ulimwengu. 

Kumbe basi Yesu si Nabii tuu, kama wanavyo dai Waislam kuwa eti, Yesu ni Nabii tu na si zaidi ya hapo. Kumbe Yesu ni zaidi ya Nabii, maana aliishi kabla ya kuzaliwa. 

Ndugu zanguni, nani aliye ishi kabla ya Uumbaji? Hata Koran inakiri kuwa, kabla ya kuumbwa kwa vitu vyote, alikuwepo Mungu. YESU ANASEMA KUWA, ALIISHI KABLA YA UUMBAJI. (Yohana 17:5).

Kumbe basi, Yesu ni Mungu maana alikuwepo wakati wa uumbaji. Wakolosai 1: 16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. 17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. 

Tumesoma katika Wakolosai kuwa katika Yesu kila kitu kiliumbwa na tunasoma kuwa Yesu alikuwapo kabla ya kuumbwa kwa vitu vyote, kama ilivyo semwa katika Yohana 17:5.

Yohana 1: 3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika. Katika hii aya nayo inatuambia kuwa, katika Yesu vyote vilifanyika.

Ndugu zanguni, ni nani huyu mwenye mamlaka haya kama sie Mungu? Iweje Yesu aishi kabla ya kuumbwa Dunia? Iweje kila kitu kiliumbwa kupitia Yesu? 

Biblia inatuambia kuwa Mungu ndie muumbaji wa kila kitu. Biblia hiyo hiyo imetuambia kuwa kupitia Yesu, kila kitu kiliumbwa. Kumbe basi Yesu ni Mungu muumbaji. 

Leo tumejifunza kwa ufupi tu kuwa, YESU ALIISHI KABLA YA KUUMBWA DUNIA.

Katika huduma yake,

Max Shimba Ministries

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW