UTATA MKUBWA KATIKA KORAN
NANI ALIKUWA MUISLAM WA KWANZA?
Ndugu zanguni:
Leo ningependa tuangalie kiundani kidogo kuhusu, “nani
alikuwa Muislam wa Kwanza” kutokana na Koran iliyo teremshwa na Allah.
Kwa mujibu wa vifungu kadhaa katika Quran, Muhammad
ni Muislamu kwanza :
Quran 6: 14. Sema: Je, nimchukue rafiki
mlinzi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ambaye ndiye Muumba mbingu na ardhi, naye
ndiye anaye lisha wala halishwi? Sema: Mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza wa
wenye kusilimu. Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina. 161. Sema:
Kwa hakika mimi Mola wangu Mlezi ameniongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka, Dini
iliyo sawa kabisa, ambayo ndiyo mila ya Ibrahim aliye kuwa mwongofu, wala
hakuwa miongoni mwa washirikina. 162. Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na
kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote. 163. Hana
mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu. (Wa ' Ana '
Awwalu Al- Muslimin ). S. 6:161-163
Sema (Ewe Muhammad): Hakika Mimi nimeamrishwa
nimuabudu Mwenyezi Mungu, kwa kumsafishia Dini Yeye ( tu ). Na nimeamrishwa
niwe wa kwanza wa wale ambao ni Waislamu ( kujisalimisha kwake ). S. 39:11-12
Pickthall
Sura hizo hapo juu na aya hizo ulizo zisoma
zinapingana vibaya sana na sura zingine katika Koran hiyo hiyo ambazo
ziliteremshwa na Allah huyo huyo na kusema Manabii walio tangulia kabla ya
Muhammad ndio walikuwa Waislam wa Kwanza.
Kuran inadai kwamba Adam, Ibrahim, Nuhu, mababu,
makabila kumi na mawili ya Israeli, Musa, Yesu nk, hao wote walikuwa waumini wa
Allah na walikuwa Waislam, kumbuka hao wote waliishi kabla ya Muhammad ambaye
anadai kuwa yeye ni Muislam wa Kwanza:
S.
02:30 , 34-35 , 37
30. Na pale Mola wako Mlezi alipo waambia
Malaika: Mimi nitamweka katika ardhi Khalifa (mfwatizi), wakasema: Utaweka humo
atakaye fanya uharibifu humo na kumwaga damu, hali sisi tunakutakasa kwa sifa
zako na tunakutaja kwa utakatifu wako? Akasema: Hakika Mimi nayajua msiyo
yajua. 34. Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam, wakamsujudia wote
isipo kuwa Iblis, alikataa na akajivuna na akawa katika makafiri. 35. Na
tulisema: Ewe Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani, na kuleni humo maridhawa
popote mpendapo, lakini msiukaribie mti huu tu; mkawa katika wale walio
dhulumu. 37. Kisha Adam akapokea maneno kwa Mola
wake Mlezi, na Mola wake Mlezi alimkubalia toba yake; hakika Yeye ndiye Mwingi
wa kukubali toba na Mwenye kurehemu. S. 02:30 , 34-35 , 37
163. Hakika Sisi tumekuletea wahyi wewe
kama tulivyo wapelekea wahyi Nuhu na Manabii walio kuwa baada yake. Na
tulimpelekea wahyi Ibrahim na Ismail na Is-haka na Yaakub na wajukuu zake, na
Isa na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman, na Daud tukampa Zaburi. S. 4:163
84. Na tukamtunukia (Ibrahim) Is-haq na
Yaakub. Kila mmoja wao tulimwongoa. Na Nuhu tulimwongoa kabla. Na katika kizazi
chake tulimwongoa Daud na Suleiman na Ayyub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivi
ndivyo tunavyo walipa wafanyao wema: S. 6:84
127. Na
kumbukeni Ibrahim na Ismail walipo inyanyua misingi ya ile Nyumba wakaomba: Ewe
Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe ndiye Msikizi Mjuzi. 128. Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe
ni wenye kusilimu kwako, na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe umma ulio silimu
kwako. Na utuonyeshe njia za ibada yetu na utusamehe. Bila shaka Wewe ndiye
Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. 129. Ewe
Mola Mlezi wetu! Waletee Mtume anaye tokana na wao, awasomee Aya zako, na
awafundishe Kitabu na hikima na awatakase. Hakika Wewe ndiye Mwenye nguvu,
Mwenye hikima. 130. Na nani atajitenga na mila ya Ibrahim isipo kuwa anayeitia
nafsi yake katika upumbavu? Na kwa yakini Sisi tulimteuwa yeye katika dunia; na
hakika yeye katika Akhera atakuwa miongoni mwa watu wema 131.
Na Mola wake Mlezi alipo mwambia: Silimu, Nyenyekea! Alinena: Nimesilimu, nimenyenyekea
kwa Mola wa walimwengu wote. 132. Na
Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu
amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu. 133. Je! Mlikuwapo yalipo mfikia Yaaqub
mauti, akawaambia wanawe: Mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu
Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is- hak, Mungu Mmoja tu,
na sisi tunasilimu kwake. S. 2:127-133 Shakir
52. Isa alipo hisi kuwa kati yao pana
ukafiri alisema: Nani wasaidizi wangu kwa Mwenyezi Mungu? Wanafunzi wake
wakasema: Sisi ni wasaidizi wa Mwenyezi Mungu. Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na
shuhudia kwamba sisi hakika ni Waislamu. S. 03:52
67. Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo,
lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina. S. 3:67
Shakir
113. Wote
hao si sawa sawa. Miongoni mwa Watu wa Kitabu wamo watu walio simama baraabara,
wanasoma Aya za Mwenyezi Mungu nyakati za usiku, na pia wanasujudu. 114. Wanamuamini Mwenyezi Mungu na Siku
ya Mwisho, na wanaamrisha mema na wanakataza maovu na wanakimbilia katika mambo
ya kheri. Na hao ndio miongoni mwa watenda mema. 115. Na kheri yoyote wanayo ifanya
hawatanyimwa malipwa yake. Na Mwenyezi Mungu anawajua wachamngu. S. 3:113-115 Shakir
110. Na pale
Mwenyezi Mungu atapo sema: Ewe Isa bin Maryamu! Kumbuka neema yangu juu yako,
na juu ya mama yako, nilipo kutia nguvu kwa Roho Takatifu, ukazungumza na watu
katika utoto na utuuzimani. Na nilivyo kufunza kuandika na hikima na Taurati na
Injili. Na ulipo tengeneza udongo sura ya ndege, kwa idhini yangu, kisha
ukapuliza ikawa ndege kwa idhini yangu; na ulipo waponesha vipofu na wakoma kwa
idhini yangu; na ulipo wafufua wafu kwa idhini yangu; na nilipo kukinga na Wana
wa Israili ulipo wajia na hoja zilizo wazi, na wakasema walio kufuru miongoni mwao:
Haya si lolote ila ni uchawi mtupu! 111. Na
nilipo wafunulia Wanafunzi kwamba waniamini Mimi na Mtume wangu, wakasema:
Tumeamini na shuhudia kuwa sisi ni Waislamu. S. 5:110-111
31.
Msinifanyie jeuri, na fikeni kwangu nanyi mmekwisha kuwa wenye kusalimu amri. 32. Akasema: Enyi wahishimiwa! Nipeni
shauri katika jambo langu hili, kwani mimi sikati shauri yoyote mpaka mhudhurie 42.
Basi (Malkia) alipo fika akaambiwa: Je! Kiti chako cha enzi ni kama hiki?
Akasema: Kama kwamba ndicho hichi. (Sulaiman na watu wake wakasema): Na sisi
tumepewa ilimu kabla yake (Malkia), na tukawa Waislamu. 44. Akaambiwa: Liingie
behewa la hili jumba. Alipo liona alidhani ni maji, na akapandisha nguo mpaka
kwenye miundi yake. (Sulaiman) akasema: Hakika hilo ni behewa lilio sakafiwa
kwa viyoo! Akasema (Malkia): Mola wangu Mlezi! Mimi nimejidhulumu nafsi yangu,
na sasa nanyenyekea pamoja na Sulaiman kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa
walimwengu wote. S. 27:30-31 , 42, 44 Pickthall
Koran inadai kuwa, makundi mbalimbali yaliyo kuwepo
kabla ya kuzaliwa Muhammad yaliitwa na kudaiwa kuwa yalikuwa ya Kiislam, Mfano:
Tumesoma kuwa Ibrahim ambaye aliishi miaka mingi sana kabla ya Kuzaliwa
Muhammad alidaiwa kuwa na yeye alikuwa Muislam, zaidi ya hapo, Koran inadai
kuwa, hata wanafunzi wa Yesu nao walikuwa Waislam, ( 3:52 , 67, 5:111 ). Hakika
inafahamika kuwa, wote Ibrahimu na wafuasi wa Yesu waliishi muda mrefu kabla ya
Muhammad kuzaliwa.
Kwa kweli, Kuran inadai kwamba waamini wote walikuwa
kimsingi Waislamu, ingawa hatusomi katika vitabi vingine vya dini kama Biblia
ambayo ilikuwepo kabla ya Koran kuwa, Manabii wa Biblia walidai na kukiri kuwa
eti wao nao ni Waislamu:
78. Na fanyeni juhudi kwa ajili ya Mwenyezi
Mungu kama inavyo stahiki jihadi yake. Yeye amekuteueni. Wala hakuweka juu yenu
mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim. Yeye (Mwenyezi
Mungu) alikuiteni Waislamu tangu zamani, na katika hii (Qur'ani) pia, ili awe
Mtume shahidi juu yenu, na nyinyi muwe mashahidi kwa watu. Basi shikeni Sala na
toeni Zaka na shikamaneni na Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mlinzi wenu, Mlinzi
bora kabisa, na Msaidizi bora kabisa S. 22:78
Je, nani alikuwa Muislamu wa Kwanza?
1. Katika Suran
6: 163 Koran inadai kuwa Muhammad ndie Muislam wa kwanza.
2. Katika S.
02:30 , 34-35 , 37 Koran inadai kwamba, ni Ibrahim na waumini walio zaliwa
kabla ya Muhammad ndio walikuwa Waislam wa Kwanza.
3. Katika S.
5:110-111 Koran inadai kuwa eti Isa Bin Maryam ndie alikuwa Muislam wa kwanza.
4. Katika S.
2:37 Koran inadai kuwa eti Adam ndie aliye kuwa Muislam wa Kwanza.
SWALI NI HILI:
Nani alikuwa Muislam wa kwanza?
Kwanini Koran ifanye makosa makubwa
namna hii na kudai eti Muhammad ndie alikuwa Muislam wa Kwanza?
Waislam wanaweza kudai kuwa kila umma
ulitumiwa nabii.
Kama hayo madai ni kweli, basi maswali haya
yanahitaji majibu:
1. Nani ni Nabii
wa Waafrika?
2. Nani ni Nabii
wa Wazungu?
3. Nani ni Nabii
wa Wamarekani?
4. Nani ni Nabii
wa Wachina?
HAKIKA KUNA UTATA MKUBWA SANA KATIKA
KORAN YA ALLAH ILIYO SHINDWA KUTUELEZA NI NANI ALIKUWA MUISLAM WA KWANZA.
Ndugu yangu,
Karibu kwa Yesu Kristo aliye kuja kwa Mataifa Yote.
Matayo 28: 18 Yesu akaja kwao, akasema nao,
akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Yesu Kristo alikuwa kwa Mataifa yote kama
Injili kutokana na Matayo inavyo sema hapo juu. Hakika Msamaha wa dhambi
unapatikana kupitia Yesu pekee. Soma: Luka 7 48 Kisha Yesu alimwambia mwanamke,
Umesamehewa dhambi zako.
KARIBU SANA KWA YESU KRISTO ALIYE HAI.
Mungu awabairiki sana
No comments:
Post a Comment