Sunday, January 19, 2014

YESU ALIPOKUWA DUNIANI ALIKUWA EMANUELI (MUNGU PAMOJA NA WANADAMU).

( MATHAYO 1:23-25 ) “Tazama; bikra atachukua mimba; naye atazaa mwana;nao watamwita jina lake Emanueli; yaani ,Mungu pamoja nasi”.Tabia ya Yesu inaonyesha kuwa kama mwanadamu,kuzaliwa kwake kwa uwezo wa Roho mtakatifu.Hapa tunaona jinsi alivyo na uwezo wa tofauti na wanadamu akiwa anafahamu mambo yote kabla akiwa duniani..Yeye pia ajua yote yaliyomo ndani ya moyo wa mwanadamu (YOHANA 6:64,YOHANA 13:1,YOHANA 13:11,YOHANA 18:4,YOHANA 19:28).Tena Yesu alitabiri kabla jambo kutokea,pia alijitabiria mwenyewe yatakayomtokea mbele (MARKO 8:31,LUKA 9:22,LUKA 12:50,LUKA 22:37,LIKA 24:7-26,YOHANA 3:14,YOHANA 10:17-18,YOHANA 7:33,YOHANA 13:33,YOHANA 14:28,YOHANA 17:11,YOHANA 16:5,10,16,18 ).

Yesu aliabudiwa na kusujudiwa akiwa hapa duniani,Sifa ya kuabudiwa na kusujudiwa ni ya Mungu pekee hivyo Yesu ni Mungu.(MATHAYO 4:10).

Hata malaika wote wanamsujudia Yesu (UFUNUO 22:8-9,WAEBRANIA 1;6).
Ndiyo maana Yesu alisujudiwa akiwa mtoto mchanga alipozaliwa (MATHAYO 2:11,MATHAYO 14:33<LUKA 24;52).
Hata pepo wachafu walimsujudia Yesu (MARKO 5:2,6).

YESU ALIKUWA MWANADAMU ALIPOKUWA DUNIANI

A: Alizaliwa na bikira Mariamu(mwanadamu) ( LUKA 2:3-7 ).

B: Aliongezeka kimo ( LUKA 2:40-42-52)

C: Aliona njaa kama watu wengine ( LUKA 4:2)

D: Alilala usingizi kama binadamu wengine( LUKA 8:23)

E: Alikuwa na viungo kama binadamu( LUKA 24:36-40)

F: Alikula chakula ( LUKA 24:41-43)

G: Alichoka kama mwanadamu ( LUKA 4:6; WAEBRANIA 4:15 : 2:16-18

Msalabani alikufa kama mwanadamu hakufa kama Mungu ila alitupatanisha 1TIMOTHEO 2:5
Tunaona mama yake mariamu asema mimi ni mjakazi wa BWANA YESU ( LUKA 1:38-46-47)
Tunaona pia hapa wakati wamekusanyika kwa ajili ya maombi akiwemo na Mariamu waliomba kwa jina la BWANA wala si kwa jina la mariamu(MATENDO 1:13-15,1 YOHANA 4:1-2.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW