Sunday, January 19, 2014

SABABU SABA ZA KUTHIBITISHA KUWA YESU NI MUNGU.


1.YESU NI MUUMBAJI.

Sifa ya kuumba niya Mungu peke yake ( YOHANA 1:3,14 ) “vyote vilifanyika kwa huyo;wala pasipo yeye hakukufanyika chochote kilichofanyika.Naye Neno alifanyika mwili;nasi tukauona utukufu wake kama utukufu wa Mwana pekee atokaye kwa Baba,amejaa neema na kweli”.Yesu aitwa Neno la Mungu (UFUNUO 19:13) “Kwahiyo Neno ni Mungu “(YOHANA 1:1).. na huyo ndiye aliyevifanya kuwako vitu vyote.Aliyeshuka kutoka juu na kufanyika mwili ni Yesu pekee aliyezaliwa na bikira Mariamu bila mbegu ya kiume kama inavyotokea kwa wanadamu wengine..Katika yeye vtu vyote viliumbwa (WAKOLOSAI 1:13-16) vinavyoonekana na visivyoonekana;vya mbinguni na vya duniani.Maandiko yako wazi kabisa kwa mtu mwenye Roho wa Mungu anaelewa kwa urahisi.

2.YESU ALIKUWEPO KABLA YA VITU VYOTE KUWEPO DUNIANI.

( WAKOLOSAI 1:17 ) “Naye amekuwako kabla ya vitu vyote;na vitu vyote hushikamana katika yeye”.( MIKA 5:2 ) “Basi,wewe Bethlehemu,Efrata,uliyemdogo kuwa miongoni mwa maelfu za Yuda;kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli;ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale;tangu milele“.

Yesu Kristo alikuwako kabla ya Nabii Ibrahimu kuwako(YOHANA 8:52-58). Watu walioambiwa maneno hayo n a Yesu mwenyewe wliokota mawe ili kumpiga Yesu wakisema kuwa anakufuru.Hawa ni watu wa tabia ya mwilini wanaotumia akili kupambanua mambo ya Mungu (mambo ya kiroho huwezi kuyatambua kwa akili maana Mungu ni Roho,( YOHANA 4:24)..YOHANA 17:5,24.WAEBRANIA 7:3 ). Imasema “hana baba,hana nana,hana wazazi,hana mwanzo wa siku zake,wala mwisho wa uhai wake,bali amefananishwa na Mwana wa Mungu;huyo adumu kuhani milele”.YESU ni alfa na omega ,wakwanza nawa mwisho kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu yeye alikuwako (UFUNUO 22:13).Bali kwa damu ya thamani,kama ya mwana-kondoo asiye na ila,asiye na waa,yaani ya Kristo.Naye amejulikana kweli tangu zamani,kabla haijawekwa misingi ya dunia,lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yetu ( 1PETRO 1:19-20 ).



3.YESU NI MTAWALA JUU YA YOTE. HII NI SIFA YA MUNGU PEKEE.

(YOHANA 330 ) “Yeye ajaye kutoka juu,huyo yu juu ya vyote.Yeye aliye wa dunia asili yake ni ya dunia,naye anena mambo ya duniani,yeye ajaye kutoka mbinguni yuu juu ya yote” . ( YOHANA 13:13 ) “Ninyi mwaniita ,Mwalimu, na Bwana;nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo“. ( WARUMI 14:9 ) “Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii,awamiliki waliokufa na walio hai pia”. Neno kumiliki ni kutawala sifa ya kutawala ni sifa ya Mungu pekee.

4,YESU KRISTO NI ZAIDI YA MTU YEYOTE AU NABI AU MTUME YEYOTE YULE..

( WAEBRANIA 3:1-7 ) “Mustari 3 unasema,Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahiliutukufu zaidi kuliko Musa,kama vile yeye atengenezayenyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo nyumba”..Anayezungumziwa hapa ni Yesu Kristo Mungu muumbaji. YESU ,ameketi mkono wa kuume wa ukuu huko mbinguni (WAEBRANIA 1;3-4).

5,YESU NDIYE ATAKAYE HUKUMU WALIMWENGU (WATU) WOTE.

( ZABURI 58:11 ), ‘Hakika yuko Mungu anayetawala katika dunia“. (UFUNUO 18;8 ) “Kwasababu hiyo,mapigo yake yatakuja katika siku moja,mauti na huzuni na njaanaye atateketeza kabisa kwa moto.Kwa maana Bwana Mungu aliyemhukumu ni mwenye nguvu“.Tene ndiye atakaye ihukumu Dunia yote “Tena Baba hamhukumu mtu ye yote,bali amempa Mwana (YESU) hukumu yote“.( MATHAYO 25:31-32 ) “Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu (YESU) katika utukufu wake,na malaika watakatifu wote pamoja naye,ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake.Na mataifa yote yatakusanyika mbele zake,naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi” .( MATENDO 10:42 ) “Akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudiaya kuwa huyu ndiye (Yesu) aliyeamriwa na Mungu awe mhukumu wa wahai na wafu” ( WARUMI 2:16 ) “Katika siku ile Mungu atakapozihukumu siri za wanadamu,sawasawa na injili yangu,kwa Kristo Yesu“.( 2TIMOTHEO 4:1 ) “Nakuagiza mmbele za Mungu,na mbele za Kristo Yesu,atakayewahukumu waliohai na waliokufa;kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake’.

6.YESU HABADILIKI TENE HANA KIGEUGEU. {WAEBRANIA 13:8} “Yesu Kristo ni yeye yule jana na leohata milele“. ( WAEBRANIA 1:10-12 ) “Wewe ,Bwana,hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi.Na mbingu ni kazi ya mikono yako;Hizo zitaharibika,lakini wewe unadumu;Nazo zote zinachakaa kama nguo,Na kama mavazi,utazizinga,nazo zitabadilika;Lakini wewe u yeye yule,na miaka yako haitakoma“. ( MALAKI 3:6 ) “Kwa kuwa mimi,Bwana,sina kigeugeu” ( ZABURI 102:26-27 ) “Hizi zitaharibika,bali wewe utadumu;Naam,hizi zitachakaa kama nguo;na kama mavazi utazibadirisha,nazo zitabadilika.Lakini wewe U yeye yule;na miaka yako haitakoma“. ( YAKOBO 1:17 ) “Kwake hakuna kubadilika,wala kivulu cha kugeukageuka”.

YESU YUPO KILA MAHALI ,KOTEKOTE DUNIANI.

( MATHAYO 18:20 ) “Kwa kuwa walipo wawili watatu,wamekusanyika kwa jina langu,mimi nipo papo hapo katikati yao”. Mwenye uwezo wa kukaa mahali pote ni Mungu.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW