|
Ikiwa ni siku ya tatu ya mkutano wa ufufuo na uzima unaoendelea katika
viwanja vya vya shule ya sekondari ya morogoro mchawi mmoja
aliyejulikana kwa jina la Fatuma amekamatwa katika mkutano huo akiwa
yuko katika shughuli zake za kila siku za kichawi.
Dada huyo aliyekamatwa na Nguvu za Mungu alielezea akasema alikuwa na
wenzake ambao walitumwa na bosi wao ambaye ni mchawi na mganga wa
kienyeji maarufu kutoka mjini Bagamoyo wilaya ya pwani kuja katika mji
wa Morogoro kuchukua miili ya watu waliokufa katika nyumba za kuhifadhia
maiti za hospitali(mochuari) kwa ajili ya kitoweo.
Akizungumza alisema yeye na wenzake walipoteana walipofika karibu na
hospitali ya rufaa ya mji wa Morogoro ambapo ni eneo la jirani na sehemu
mkutano unapofanyika, alipofika maeneo hayo alisikia nguvu inamvuta kwa
nguvu na kumpeleka asipotaka yeye ndipo alipojikuta ametua katika
viwanja shule ya sekondari ya Morogoro ambapo ndipo mkutano unapofanyika
Dada huyo aliyeonekana kuwa na wasi wasi alisema tulikuja mimi na
wenzangu kwa usafiri wa njia ya fisi lakini tulipokaribia hospitali
sijui nini kimetokea na mimi nikasikia nguvu zinanivuta nikajikuta niko
mahali hapa
ALIANZAJE UCHAWI
Akielezea jinsi alivyoanza uchawi alisema miaka kumi na tano iliyopita
alikua anaumwa ndipo alipoamua kuondoka kwao Babati(Manyara) kwenda
kutibiwa mkoani Pwani kwa mganga aliyejulikana kwa jina la Idi.
Alipofika kwa mganga aliambiwa akachume pilini dawa Fulani na aitafune,
alipofanya sawasawa na maelekezo ya yule mganga ndipo alipojiona anaanza
kuingiwa na ukatili usiokuwa wa kawaida na akaanza kupata hamu ya kula
wanadamu wenzake, kuanzia siku hiyo ndipo alipoanza kuagizwa na Idi kwa
ajili ya kufanya shughuli za kichawi pamoja na wenzake.
NAMNA ALIVYOKUWA AKITENDA KAZI
Yeye na wenzake walikuwa wanawashughulikia hasa watu ambao waliokoka na
baada ya hapo wakarudi nyuma, akieleza jinsi walivyokua wakiifanya kazi
hiyo alisema mtu yeyote aliyewahi kuokoka na baada ya hapo kumuacha Yesu
anakuwa na majini mawili wanaotumwa kukaa ndani yake, na wachawi hawa
wanapomfuata mtu huyo wanaongea nayale mapepo na wanayaagiza yamnyonge
mtu huyo na mtu huyo anakufa mara moja
Katika utendaji kazi wake yeye ndiye aliyekuwa kiongozi wa kikundi chake
hicho walichokuwa wanatenda shughuli hizo za kichawi.Alisema mimi
niliwekwa kuwa kiongozi wa wenzangu kwasababu mimi nilikua nimefanikiwa
kuwaua watu watatu waliokua wameokoka na kurudi nyuma. Kule kwenye
uchawi mtu aliyefanikiwa kuwaua watu waliorudi nyuma ndie anakua na cheo
kuliko wengine, mimi niliua watu ambao walikua hawajawahi kuokoka zaidi
ya thelathini na waliokua wameokoka na kurudi nyuma watatu alisema dada
huyo.
Akielezea
alisema sisi tulikuwa na uwezo wa kuwaua watu kwa matukio tuliyokua
tunayatengeneza, unaweza ukakuta mtu anatembea njiani alafu akawa kama
ameumwa na nyoka lakini nyoka mwenyewe hamuoni, mtu huyo baada ya masaa
machache atakufa na sababu itakuwa kwamba aliumwa na nyoka lakini sivyo
tunakuwa ni sisi tumemtengenezea kifo ili tukamle nyama.
WATU ALIOWAHI KUWAUA
Alisema anakumbuka miaka mitano iliyopita alimuua mdogo wake aaliyekuwa
anajulikana kwa jina la Udiyomboli, watu watatu ambao waliwahi kuokoka
na kasha kurudi nyuma pamoja na wengine Zaidi ya thelathini
aliowaangamiza kwa kutumia uchawi
Baada ya hapo dada huyo akiongea kwa huzuni aliomba msaada akasema,
nimechoka kufanya uchawi siyapendi maisha haya na sitaki tena kurudi
kule Bagamoyo.
Dada huyo tayari ameshaachana na mambo ya uchawi na amempokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yake.
No comments:
Post a Comment