Thursday, October 24, 2013

Yesu Kristo hajaumbwa bali alikuwepo tangu milele yote

Ni kweli kabisa kwamba Yesu alikuwepo tangu milele yote kabla ya kuumbwa kitu cho chote kile. Bwana Yesu kwa kauli ya kinywa chake mwenyewe anasema kwamba:
Na sasa, Baba, unitukuze Mimi pamoja Nawe, kwa utukufu ule Mimi niliokuwa nao pamoja Nawe kabla ya ulimwengu kuwako.” (Yohana 17:5)
Neno “UTUKUFU” maana yake ni heshima, uweza, uzuri, umaarufu, nguvu, sifa na mamlaka. Mambo hayo yote Yesu alikuwa nayo kabla hata ulimwengu haujaumbwa. Yesu Kristo alikuwapo hata kabla ya kuzaliwa na Mariamu; jambo hili pia Yesu Kristo kwa kinywa Chake Yeye mwenyewe ametuthibitishia alipokuwa akiwaambia Wayahudi kwamba:

Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.

Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Je! Sisi hatusemi vema ya kwamba wewe u Msamaria, nawe una pepo?

Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini Mimi namheshimu Baba yanguna ninyi mwanivunjia heshima Yangu. Wala mimi siutafuti utukufu Wangu; Yuko mwenye kutafuta na kuhukumu. Amin, amin, nawaambia, Mtu akilishika neno langu, hataona mauti mileleBasi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng’amua ya kuwa una pepo. Ibrahimu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akuilishika neno langu, hataonja mauti milele. Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa? Nao manabii wamekufa. Wajifanya u nani? Yesu akajibu, Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu si situ; anitukuzaye ni Baba Yanguambaye ninyi mwanena kuwa ni Mungu wenu. Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nalishika. Ibrahimu baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.

Basi Wayahudi wakamwambia, Wewe haujapata bado miaka hamsini, nawe umemona Ibrahimu? Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, Mimi niko.” (Yohana 8:47-58)

Katika kisa tulichokisoma katika maandiko hayo (Yohana 8:47-57) tunajifunza mambo kadhaa hapo. Tumeona dhahiri jinsi ambavyo hata baadhi ya Wayahudi ilivyo wawia vigumu sana kumwelewa huyu Yesu ni nani; hata wakadiriki kusema kuwa Yesu anayo mapepo (mashetani). Hawakumwelewa kwa sababu walimtazama Yesu kibinadamu kama jinsi wao walivyo, lakini hawakujua kuwa Yesu ni alikuwepo hata kabla ya Yeye kuzaliwa na Mariamu. Huyo Ibrahimu anayeongelewa hapo ni yule ambaye habari zake tunazisoma katika kitabu cha MWANZO cha Biblia (Ibrahimu baba yake Isaka na Ishmaili). Wayahudi walishangaa; Inawezekanaje huyu Yesu aseme alimwona Ibrahimu aliyeishi na kufa miaka mingi tena zaidi ya elfu moja iliyopita, wakati huyu Yesu tumemwona utotoni mwake na hata sasa bado hajatimiza umri wa miaka hamsini? Hayo yalikuwa ni mawazo ya kibinadamu; tena inaezekana hata wewe ukawa ni miongoni mwa waliokuwa wanawaza hivyo; lakini, Yesu mwenyewe anatuthibitishia kwa kinywa Chake kwa kusema:

...Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, Mimi niko.” (Yohana 8:58)
Pia Yesu amewaambia Wayahudi kuwa huyo ambaye wao wanamwita Mungu (YEHOVA), Yeye ndiye Baba wa Yesu; tena Yesu anamjua ingawa hao Wayahudi hawamju (Yohana 8:54,55). Vile vile tusomapo kitabu cha MITHALI tunaona habari zinazo mhusu huyu Yesu; imeandikwa kwamba:

BWANA alikuwa nami katika mwanzo wa njia yakeKabla ya matendo Yake ya kale. Nalitukuka tokea milele, tangu awali, Kabla haijawako dunia. Wakati visipokuwapo vilindi nalijidhihirisha... (...I was brought forth... – NKJV)...” (Mithali 8:22-24)
Usomapo Biblia ya Kiswahili; hapo nilipoandika “...Wakati visipokuwapo vilindi NALIJIDHIHIRISHA...” utaona baadhi ya Biblia za Kiswahili zimeandika “...NALIZALIWA...” lakini maana halisi hapo ni “...I was brought forth...” ambayo tafsiri yake ni “...NALIJITOKEZA...” au “...NALIJIDHIHIRISHA...

Kumbuka kuwa Wayahudi walimtambua Mungu kwa jina "YEHOVA" ambalo mara nyingi walitamka kwa kusema "BWANA." Hapo Biblia Takatifu inamtaja huyu Yesu likuwa pamoja na YEHOVA katika mwanzo wa njia za YEHOVAKabla ya YEHOVA kuumba cho chote (...matendo ya kale...) huyu Yesu alikuwepo. Hivyo basi; huyu Yesu alikuwapo “...tokea milele, tangu awali, Kabla haijawako dunia.” (Mithali 8:23) Neno “MILELE” maana yake ni wakati ambao hauna mwanzo wala mwisho; ni wakati usioweza kuhesabika.

Upo ushahidi mwingi sana ndani ya Biblia Takatifu unaotuthibitishia kuwa Yesu alikuwepo hata kabla ya kuumbwa kitu cho chote kile; kwani nao manabii pia walitabiri ujio wa Yesu ambaye alikuwepo tangu milele yote, na tena manabii hao walisema wazi wazi kuwa huyu Yesu ni Mungu

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW