Leo nitajibu haya madai ya Upanga.
Waumini wa dini ya Kiislam katika
Mihadhara mbalimbali ya kidini wamekuwa na tabia ya kutumia aya YA UPANGA iliyopo
katika Mathayo 10: 34 inayo sema ''MSIDHANI NALIKUJA KULETA AMANI DUNIANI, LAAA!
BALI UPANGA!
Waislam wanadai kuwa, katika aya hii, Yesu alikuja kuleta UPANGA na si Habari
Njema kama tufundishavyo sisi Wakristo.
Kwa kuwa Waislam kazi yao ni kutoa
kashfa na kuutukana Ukristo, wahadhiri hao wa Dini ya Uislamu hufundisha jamii
kwa kutumia Qurani na Biblia na kusema kuwa eti Yesu alikuja kuleta UPANGA na Hivyo Basi Ukristo ni dini ya UPANGA.
Fundisho hili la "MSIDHANI
NALIKUJA KULETA AMANI DUNIANI, LAAA! BALI UPANGA! " wanalieneza kwa kupitia
Mitandao mbalimbali kama ya Radio, Vijarida, Mihadhara, vitabu na Kanda
(cassettes) za Video na Audio. Na hivyo kuwafanya baadhi ya Wakristo kuingiwa
na wasiwasi kutokana na jinsi hawa Wahadhiri wa Dini ya Uislamu wanavyo toa
kashfa chafu kwa Yesu Kristo ambaye ni Masiah. Na baadhi ya Wakristo wengine
ingawa hawajabadili dini wanaamini hivyo. Swali la muhimu la kujiuliza kwa kila
Mkristo, je, ni kweli Yesu alikuja kuleta UPANGA? Nakusihi fuatilia somo hili
kwa makini ili kujua Ukweli wa aya hii:
Ngoja
niiweke hiyo aya:
Mathayo
10:34''MSIDHANI NALIKUJA KULETA AMANI DUNIANI, LAAA! BALI UPANGA!
Ukitazama na kusikiliza kwa haraka
haraka namna wahadhiri hao wa Dini ya Uislamu wanavyoifunda hii aya ya Biblia
unaweza ukashawishika kuamini hicho wanachokifundisha, lakini ni vyema
tukajifundisha kwa undani kadiri maneno ya Yesu kuwa "MSIDHANI NALIKUJA
KULETA AMANI DUNIANI, LAAA! BALI UPANGA!" kisha tuone kama kuna ukweli juu
ya hayo mafundisho yao, ya kusema kuwa Yesu alikuja kuleta Upanga na si kutangaza
Habari Njema kwa Mataifa yote.
Haya tuanze utafiti wetu.
Kwanza tujiuluize, Je, Yesu analeta
Upanga wa ainga gani? Yesu anazungumzi Upanga ambao ni “Neno la Mungu”. Neno la Mungu linagawanya na au kukata Mabaya
na kuacha mazuri. Hebu kwanza tuyasome
maagizo yake kwa wanafuzi. Mathayo 10 aya 16: Inasema: Sasa, mimi nawatuma ninyi kama kondoo kati ya mbwa
mwitu. Muwe na busara kama nyoka, na wapole kama njiwa. Katika hii AYA,
Yesu anawaambia Wanafunzi wake wawe na Busara na Wapole, Hatusomi katia hii aya
kuwa anawaambia wabebe Upanga. Je, Yesu alipo sema Upanga, alimaanisha nini?
Hebu tuendelee na somo letu.
Sasa
tuangalie aya ya 1 inasema: “Yesu aliwaita wanafunzi wake kumi na wawili,
akawapa uwezo wa kutoa pepo wachafu na kuponya magonjwa na maradhi yote”.
Upanga unao zungumziwa hapa ni uwezo ambao Yesu aliwapa Wanafunzi wake. Unaweza
kuniuliza uwezo huo ni nini?
Hebu tusome Kitabu
cha Waefeso ili tuweze kuelewa nini hasa maana ya Upanga na Uwezo wa kutoa Pepo
na Kuponya kama alivyo wapa Wanafunzi wake.
Waefeso 6:17
17 Vaeni wokovu kama
kofia ya vita vichwani na chukueni UPANGA
wa Roho ambao ni neno la Mungu.
Kutokana na ayah hii
ya Waefeso, tumeweza kufunguliwa macho yetu ya Kiroho na kuelewa kuwa UPANGA NI NENO LA MUNGU.
Kwasabau Waislam
wanakubali kuwa Yesu kaleta Upanga ambao sasa tunaelewa nini maana yake kutoka
na Ushaidi wa Waefeso. Basi leo hii hawa Waislam hawatakuwa na jinsi ya
kujitetea bali kukubali kuwa Upanga ambao ni Neno la Mungu ni wa kufuatwa kama
alivyo sema Yesu katika Mathayo 10: 34.
Ni matumaini yangu kuwa leo hii umeweza
kujua kwa undani maana ya "MSIDHANI NALIKUJA KULETA AMANI DUNIANI, LAAA!
BALI (UPANGA) NENO LA MUNGU!" na Yesu alipo sema hayo alikuwa anatufahamisha kuwa neon
La Mungu ni Sawa na Upanga Mkali unao tenganisha na au toa Mabaya yote kwa
Binadamu.
Mungu awabariki sana
Katika Huduma Yake
Max Shimba
Copyright © Max Shimba Ministries 2013
No comments:
Post a Comment