UTANGULIZI
Imekuwa ni kawaida sasa kwa
miaka zaidi ya ishirini hivi, kusikia katika mihadhara inayoendeshwa na
wahadhiri wa dini ya Uislamu, ambayo imeenea sehemu mbalimbali Duniani na haswa
katika nchi za Africa Mashariki na Kati,(East and Central Africa). Wahadhiri
hao hufundisha jamii kupitia Qurani na Biblia kwa kusema kuwa Mungu ni Mmoja
tu. Wasema Mungu kwa Kiebrania anaitwa Yehova , kwa Kiarabu Allah, kwa
Kiingereza God na kwa Kiswahili ni Mungu. Kwa hivyo wasema Mungu Allah kama
Qurani inavyofundisha, ndiye Yehova kama Biblia inavyofundisha. Mihadhara hiyo
inayoendeshwa na Waislamu imeenea sana, mfano Nchini Tanzania kuna vikundi
vingi na kimoja wapo kinaitwa Al-Marid International Propagation Center. Hawa
wameandika katika bango lao kwa kunukuu katika Biblia maneno aliyoandika Mtume
Paulo katika Waefeso 4:4-6. Maneno waliyoyanukuu yanasema hivi “Bwana mmoja ,
Imani moja ….., Mungu mmoja , naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote.
Nilipotembelea mkoa wa Morogoro pale mjini, eneo la kiwanja cha ndege nikaona
Msikiti mmoja umeandikwa maneno haya ya Waefeso 4:4-6. Na nilipotembelea mji wa
Nairobi Nchini Kenya pia nikaona kuna vikundi vingi vinavyoendesha mihadhara na
kikundi kimoja wapo kinaitwa Kibera Islamic Propagation Centre. Hawa nao katika
bango lao wameandika ujumbe unaosema hivi “Acha Biblia Ijisemee na kunukuu
injili aya hii” Yohana 8:32 Tena mtaifahamu kweli nayo hiyo kweli itawaweka
huru.
Kwa hivyo utaona kuwa
wahadhiri hao wa Dini ya Uislamu hufundisha jamii kwa kutumia Qurani na Biblia
na kusema Allah Sub-Hana Wataala ndiye YEHOVA. Fundisho hili wanalieneza kwa
kupitia Radio, Vijarida, Mihadhara, vitabu na Kanda (cassettes) za Video na
Audio. Na hivyo kuwafanya baadhi ya Wakristo kuacha Imani yao na kuingia katika
Dini ya Uislamu. Na baadhi ya Wakristo wengine ingawa hawajabadili dini
wanaamini hivyo. Swali la muhimu la kujiuliza kwa kila mkristo, je, ni kweli
Mungu Allah kama inavyotuhadithia Qurani ndiye Yehova kama Biblia
inavyotufundisha? Nakusihi fuatilia somo hili kwa makini ili kujua Ukweli……
SEHEMU KUU ZA SOMO HILI NI
HIZI……
1. Hoja za waislamu kusema
Allah ndiye Yehova.
2. Je, jina la Mungu kadiri
ya Qurani na Biblia ni moja?
3. Je, Malaika mkuu wa
Allah ndiye wa Yehova?
4. Je, ni nani muumba,Allah
au Yehova?
5. Mji aliochagua Allah je,
ni sawa na wa Yehova?
6. Allah anavyofundisha
kuhusu kujitakasa nafsi je, ni sawa na Yehova?
7. Je, mbingu ya Yehova ni
sawa na ya Allah?
8. Mwisho wa wanaomwabudu
Allah ni wapi?
1. Hoja za waislamu kusema
Allah ndiye Yehova
Wahadhiri wa Dini ya
Uislamu wanasema Mungu Allah ndiye Yehova kwa sababu Manabii wa Mungu kadiri ya
Biblia na Qurani walifundisha kwa kusema Mungu ni mmoja tu. Na wanasoma aya
hizi…
Nabii Musa alivyosema
Kumbukumbu la Torati 6:4
Sikiza ee Israeli; BWANA
Mungu wetu BWANA ndiye mmoja.
Nabii Isaya alisema hivi
Isaya 45:18,21
Maana BWANA , aliyeumba
mbingu, asema hivi, yeye ni Mungu ,ndiye aliyeumba Dunia na kuifanya ….. si
mimi BWANA? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi. Mungu mwenye haki , mwokozi hapana
mwingine zaidi ya mimi.
Nabii Daudi Alisema
Zaburi 86:10
Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu,
wewe ndiwe mfanya miujiza , ndiwe Mungu peke yako.
Yesu alisema hivi
Yohana 17:3
na uzima wa milele ndio huu
wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliye mtuma
Paulo naye Alisema hivi
1 Wakorintho 8:4
Basi kwa habari ya kuvila
vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu; twajua ya kuwa sanamu si kitu katika
ulimwengu, na yakuwa hakuna Mungu ila mmoja tu.
Hapa wahadhiri wa Dini ya
Uislamu wanasema Manabii wote kadiri ya Biblia wanafundisha kuwa Mungu ni mmoja
tu. Je, Muhammad (s.a.w.) alifundisha nini kuhusu Mungu? Wanasoma aya hizi za
Qurani……..
Qurani 41:6 Suratul Haa Mym
Sajdah (Kusujudu)
Sema; bila shaka mimi ni
mtu kama nyinyi. Nimeletewa Wahyi (inafunuliwa kwangu)ya kwamba Mungu wenu ni
Mungu mmoja tu……
Hapa wahadhiri wanasema
kama vile manabii wote walifundisha Mungu mmoja ndivyo ilivyo fundisha
Muhammad.
Qurani 29:46-47 Suratul Al-
Ankabuut (Buibui).
Wala mshibishane na watu
waliopewa kitabu (kabla yenu) ila kwa yale (majadiliano) yaliyo mazuri,
isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Na semeni :tunaamini yaliyoteremshwa
kwetu, na yaliyoteremshwa kwenu. Na mungu wetu na Mungu wenu ni mmoja : nasi ni
wenye kunyenyekea kwake. Na namna hivi tumekuteremshia kitabu (hiki cha Qurani)
basi wale tuliowapa kitabu (kabla ya hiki kama taurati na injili) wanakiamini
(hiki kitabu ulichoteremshiwa kwani hakipingani na hivyo walivyoteremshiwa). Na
miongoni mwa hawa (Waarabu wasiokuwa na Kitabu chochote)wako wanaokiamini. Na
hawazikatai aya zetu isipokuwa wale wanaotaka kuficha haki.
Hapa wahadhiri wa kiislamu
wakisha soma aya hizi husema vitabu vya Torati na Injili havipingani na Qurani,
na vitabu hivyo walipewa Wayahudi na Manasara(yaani Wakristo) na Mungu wa
Waislamu na Wakristo ni mmoja tu.
Je, hoja hii ni kweli?
Nitaijibu huko mbele.
Majibu kuhusu Mungu mmoja
Ukitazama kwa haraka haraka
namna wahadhiri hao wa Dini ya Uislamu wanavyolinganisha aya za Qurani na
Biblia unaweza ukashawishika kuamini hicho wanachokifundisha, lakini ni vyema
tukajifundisha kwa undani kadiri ya Qurani na Biblia na kisha tuone kama kuna
ukweli juu ya hayo mafundisho yao, ya kusema Allah Sub-hana Wataala ndiye
Yehova.tukumbuke kuwa Mungu tunayeabudu alitutahadhalisha sana Wakristo kwa
kusema hivi…
Kutoka 20:1-3
Mungu akanena maneno haya
yote akasema Mimi ni BWANA Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika
nyumba ya utumwa usiwe na Miungu mingine ila mimi.
Tahadhari hii Ya Mungu wetu
ya kusema usiwe na Miungu inamaanisha kuwa Miungu mingine yenye kuabundiwa na
watu ipo. Kwa sababu katika Biblia neno Mungu Kiebrania“Elohim” Kiyunani
"Theos" limetanjwa mara 3979 lakini pia miungu ya uongo imetanjwa
mara 271. baadhi ya miungu hiyo ya uongo ni hii
mungu Dargoni Waamuzi16:23
mungu Baal Wafalme 18:21
mungu mke wa Waefeso aitwae
Artemi Matendo 19:24-28.
Aidha tusomapo Qurani pia
imetaja miungu mbalimbali iliyokuwa inaabundiwa kule Makka nayo ni hii;
Qurani 53:19-20,23 Suratul
An- Najm (Nyota).
19. Je, mumewaona Lata na
Uzza? 20. Na Manata (mungu wenu) mwingine wa tatu (kuwa ndio waungu hao badala
ya mwenyenzi mungu)? 23. hayakuwa haya (majina ya Lata mungu mwanamke na Uzza
mungu mwanamke mwenye enzi. Na Manata mungu mwanamke anayeneemesha ila ni
majina tu mliowapa nyinyi na baba zenu…..
Hivyo basi tunaona kuwa
miungu yenyewe kuabudiwa ni mingi na kila mwenye kuabudu humtegemea huyo mungu
wake na kusema ni mmoja. Mfano waliyemuabudu Dagoni walisema ni mungu mmoja,
waliyemwabudu Baali walisema ni mungu mmoja , waliyemwabudu Artemi walisema
Artemi ndiye mungu mkuu. Kadharika Manabii.
walimtumikia Mungu mmoja
aitwaye Yehova, naye Muhammad alimwabudu mungu mmoja aitwaye Allah. Ninachotaka
kukifundisha kwa jamii ijue je, huyo Allah ndiye Yehova?,
2: Je, jina la Mungu kadiri
ya Qurani na Biblia ni moja?
Jambo moja la msingi linalo
tambulisha kitu au mtu, mnyama au chochote kile ni jina , hivyo ili tuweze
kujua kama Mungu anayeabudiwa na Waislamu ndiye tunayemuabudu Wakristo, ni
lazima tuangalie jina. Je, ni moja?
Qurani 17: 110 Suratul Bani
Israil (Wana wa Israil)
Sema; muombeni (Mwenyenzi
Mungu) kwa (jina la )Allah au muombeni (kwa jina la ) Rahman. Kwa jina lolote
mnalomwita (katika haya itafaa). Kwani ana majina mazuri mazuri………
Hapa tunaona Allah
anafundisha kwa Waislamu kuwa wamuombe kwa jina la Allah au Rahman. Ukisoma
Qurani utaona jina Allah limetajwa mara 2,866, kumbuka Qurani ina Juzu 30 Sura
114. hivyo Mungu anaye abudiwa na Waislamu kadiri ya Qurani jina lake anaitwa
Allah.
Jina la Mungu anayeabudiwa
na Wakristo ni hili;
Kutoka 6:2-3
Kisha Mungu akasema na Musa
akamwambiaaa “Mimi ni YEHOVA Nami nalimtokea Ibrahimu, na Isaka na Yakobo, kama
Mungu mwenyenzi, bali kwa jina langu YEHOVA sikujulikana kwao.
Hapa tunaona Mungu
tunayemuabudu Wakristo analitambulisha jina lake kwamba ni Yehova katika Biblia
limetumika neno au jina BWANA, kwa Kiingereza wanasema LORD, likimaanisha jina
lililo Takatifu sana la Mungu katika Biblia jina hili limetanjwa mara 6751.
kumbuka Biblia ina jumla ya vitabu 66 Sura 1189 Aya 31,102.
3: Je, Malaika mkuu wa
Allah ndiye wa Yehova?
Ikiwa Allah ndiye Yehova,
basi ni wazi kuwa malaika mkuu atakuwa mmoja pia. Ikiwa si mmoja hata malaika
mkuu watakuwa tofauti. Tuanze kuangalia Allah anavyosimulia katika Qurani naye
anasema hivi
Qurani 81:19-21 Suratul
At-Takwyr( Kukunja/jua litakapokunjwa)
Kwa hakika hii (Qurani ) ni
kauli (aliyokuja nayo) mjumbe mtukufu (Jibrili) Mwenye nguvu,mwenye cheo cha
hishima kwa mwenyenzi Mungu. Anayetiiwa huko (mbinguni na malaika wenziwe)
kisha muaminifu.
Ufafanuzi wa aya hizi.
ulio ndani ya Qurani
unaelezea aya hizi 19-21, unafundisha hivi…….
Mjumbe mtukufu na mwenye
kutiiwa huko mbinguni ni Jibrili, ambaye ndiye mkubwa wa malaika wote
Malaika mkuu wa Mungu
Yehova ni huyu;
Yuda 1:9
Lakini Mikaeli Malaika
mkuu, aliposhindana na Ibilisi na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa,
hakuthumbutu kumshitaki kwa kumlaumu bali alisema Bwana na akukemee
hapa tunaona aya
zinatufundisha waziwazi kuwa malaika mkubwa wa Mungu aitwae Allah anaitwa
Jibril na Malaika mkuu wa Mungu wetu Yehova anaitwa Mikaeli. Swali; Kwa
kuwaMalaika hao ni tofauti, je, Allah ndiye Yehova? Kwa kujua zaidi tofauti ya
malaika, jipatie nakala ya somo la: Malaika Jibrili na Gabrieli, je ni Malaika
mmoja. Somo hilo tunalo, jipatie.
4: Je, ni nani muumbaji, ni
Allah au Yehova?
Kila mtu mwenye kufuata
Dini huamini kuwa Mungu ndiye muumbaji ambaye ameumba wanandamu, wanyama na
vyote tunavyoviona na vile tusivyoviona. Hivi yafaa tuangalie kile kinachosemwa
na Yehova kuhusu uumbaji na vile Allah anavyosema. Je, kauli zao zinapatana au
zinatofautiana?
Je, mtu ameumbwa kwa mfano
wa nani?
Allah anasema hivi;-
Qurani112:1-4 Suratul
Al-Ikhlas (utakaso)
Sema: Yeye ni Mwenyenzi
Mungu mmoja (tu) Mwenyenzi Mungu (tu) ndiye anayestahiki kukusudiwa (na viumbe
vyake vyote kwa kumuabudu na kumuomba na kumtegemea) Hakuzaa wala hakuzaliwa
Wala hana anayefanana naye hata mmoja.
Kadiri ya aya hii Allah
asema kuwa mungu hakuzaa wala hakuzaliwa wala hana mfano wa mtu au watu Yehova
anasema hivi kuhusu mtu au watu……
Mwanzo1:26-27
Mungu akasema “Na tufanye
mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale samaki wa baharini, ndege wa
angani na wanyama , na nchi yote, pia na kila chenye kutambaa kitambaacho juu
ya nchi.
Mungu akaumba mtu kwa mfano
wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Hapa tunaona Mungu wetu
Yehova ameumba mtu kwa mfano wake, lakini Allah anasema hana anayefanana naye hata
mmoja……Swali kwako mfuatiliaji: Je, Allah ndiye Yehova? Tafadhali usome aya
hizi ili kujua zaidi (Mwanzo 5:1-2, 9:6, 1Korintho 11:7, Kolosai 1:15, 3:10,
Matendo 17:28-29, Yakobo 3:9). Pengine waweza kusema Je, Mungu amefanana na
mimi kivipi?Jua kwamba Mungu ni Roho (Yohana 4:24) Naye alitupa pumzi(yaani
roho ya uhai (Mwanzo 2:7))isitoshe Mungu ndiye Baba wa roho zetu (Waebrania
12:9) Mungu anasema Roho zetu ni mali yake(Ezekieli 18:4,Hesabu 16:22)
Kuapa kwa Mungu kuhusu
viumbe
Qurani 91:1-7 Suratul
Ash-Shams (Jua)
Naapa kwa jua na kwa
mwangaza wake. Na kwa mwezi unapoliandama. Na kwa mchana unapolidhihirisha. Na
kwa usiku unapolifunika.Na kwa mbingu na kwa Aliyezijenga. Na kwa ardhi na
Aliyeitandaza. Na kwa nafsi (roho) na Aliyeitengeneza.
Qurani 92:1-3 Suratul
Al-Layl (Usiku)
Naapa kwa usiku ufunikapo
(kila kitu). Na kwa mchana uangazapo. Na kwa aliyeumba kiume na kike.
Hapa tunaona Allah Mungu
anayeabudiwa na Waislamu anaapa kwa mbingu na kwa aliyezinjenga, kwa ardhi na
aliyeitandaza. Je, huyo mtandazi wa ardhi na mjengaji wa mbingu ni nani? Qurani
inaendelea kuhadithia hivi……..
Qurani 45:22 Suratur AL-
Jathiyah (kiyama/ kupiga magoti)
Na mwenyenzi Mungu
ameziumba mbingu na ardhi kwa haki…
Qurani 44:7-8 Suratul
Ad-Dukhan (moshi)
Mola wa mbingu na ardhi na
vilivyomo ndani yake,ikiwa mnayo yakini (basi yakinisheni haya) Hakuna
aabudiwaye kwa haki ila yeye anahuisha na kufisha. Mola wetu na ni mola wa
wazee wenu (wote) wa mwanzo (na mola wa kila kitu)
Hapa tunaona kuwa Allah
kupitia Qurani anasema kuwa mwenyenzi Mungu ameziumba mbingu na ardhi na tena
anasema hakuna aabudiwaye ila yeye. mjengaji wa mbingu na mtandazaji wa ardhi
anajieleza hivi ……
Isaya 44:24
BWANA,mkombozi wako yeye
aliyekuumba tumboni, asema hivi, “Mimi ni BWANA, nifanyaye vitu vyote,
nizitandaye mbingu peke yangu, niienezaye nchi. Ni nani aliye pamoja nami?”
Mungu wetu Yehova anasema
mimi ninafanya vitu vyote.
(Soma Isaya 45:6-7, 11-12,
Yeremia 27:5) Bila shaka Yehova ndiye muumbaji wa vitu vyote
JE Mungu Yehova
aliapia vitu alivyoviumba kama Allah?
Isaya 45:22-23
Niangalieni mimi
mkaokolewe, Enyi ncha zote za dunia. Maana mimi ni Mungu hapana mwingine. Kwa
nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala
halitarudi, ya kwamba, mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa.
Waebrania 6:13-16
Kwa maana Mungu alipompa
Ibrahimu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa,
aliapa kwa nafsi yake. akisema “Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza
nitakuongeza, Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi. maana wanadamu huapa
kwa yeye aliye mkuu kuliko wao na kwao ukomo wa mashindano yote ya maneno ni
kiapo kwa kuyathibitisha.
Hapa tunaona Mungu wetu
Yehova haapi kwa mtu wala vitu alivyoviumba kama Allah anavyoapa, bali Yehova
anasema “Naapa kwa nafsi yangu”.Waweza pia kusoma jinsi Yehova alivyoapa kwa
nafsi yake katika aya hizi;-(Isaya 14:24 na Mwanzo 22:16)
5: Je, mji aliouchagua
Allah ni sawa na wa Yehova?
Mji wa Allah:
Qurani 27:91 An-Naml
(sisimizi/mchwa/wadudu chungu)
Bila shaka nimeamrishwa
nimuabudu mola wa mji huu (wa Makka) ambaye ameutukuza na ni vyake tu (Mwenyezi
Mungu) vitu vyote…
Qurani 3:96 Suratul Aal-Imran
(watu wa Imram)
Kwa yakini nyumba ya kwanza
iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ibada) ni ile iliyo Makka yenye baraka na
uwongozi kwa ajili ya walimwengu wote.
Qurani 106:3-4 Suratul
Quraysh (Makureshi-kabila)
Basi nawamuabudu Bwana wa
nyumba hii (Al-ka'ba) Ambaye anawalisha (wakati Waarabu wenzi
wao wamo) katika njaa na
anawapa amani wakati wenzi wao wamo katika khofu.
Hivyo tunaona kuwa Allah
ndiye bwana wa Al-ka'ba kadiri ya aya hii na Al-ka'ba iko katika Makka. Kupitia
aya hizi tunaona Allah mungu anayeabudiwa na Waislamu amechagua mji wa Makka
kuwa ndio mji wake mtakatifu na tena Muhammad (s.a.w) aliamrishwa amuabudu mola
wa mji huo wa Makka ambaye ndiye Allah.
Je, Mungu wetu aitwae
Yehova alichagua mji gani? Endelea ……..
Mji aliouchagua Mungu wetu
Yehova ni huu…
2 Nyakati 6:4-6
Akasema, BWANA, Mungu wa
Israeli, ahimidiwe, aliyenena kwa kinywa chake na baba yangu Daudi, akalitimiza
kwa mikono yake, akasema, Tangu siku ile nilipowatoa watu wangu katika nchi ya
Misri, sikuchagua mji wowote wa kabila zote za Israeli ili kujenga nyumba, jina
langu liwe humo; wala sikumchagua mtu yeyote awe mkuu juu ya watu wangu
Israeli, lakini nimeuchagua Yerusalemu, jina langu liwe humo, na Daudi nimemchagua
awe juu ya watu wangu Israeli.
Maandiko hayaelezi mji
mwingine wowote aliouchagua Mungu wetu hapa duniani bali ni mji wa Yerusalemu
tu. (tazama 2 Nyakati 12:13,Ezra 6:12; 7:15,27; Zaburi 26:8; Zakaria 2:12)
Kupitia aya hizi tunaona
Mungu wetu Yehova, mji wake aliouchagua niYerusalemu. Neno Yerusalemu ni la
lugha ya Kiebrania na maana yake ni "chimbuko la amani". Hata
Waisraeli walipokuwa mbali na mji wa Yerusalemu bado walipiga magoti na
kuelekeza nyuso zao Yerusalemu. (Tazama Danieli 6:10). Mji aliouchagua Yehova
ni Yerusalemu, na mji aliouchagua Allah ni Makka. Na hii ndio tofauti ya mji wa
Allah na Yehova.
6: Allah anavyofundisha
kujitakasa nafsi, je ni sawa na Yehova?
Allah anafundisha hivi….
Qurani 53:32 Suratul
Al-Najm (nyota)
Ambao wanajiepusha na
madhambi makuu na vitendo vichafu, isipokuwa makosa hafifu (hakuma
aliyesalimika nayo) bila shaka, mola wako ndiye mwenye maghufira mengi yeye
ndiye anayekujueni sana tangu alipokuumbeni katika ardhi na mlipokuwa mimba
matumboni mwa mama zenu. basi msizitakase nafsi zenu….
Qurani 12:53 Suratul Yusuf
Nami sijitakasi nafsi
yangu, kwa hakika (kila) nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu isipokuwa ile
ambayo mola wangu ameirehemu. Hakika mola wangu ni mwingi wa kusamehe (na)
mwingi wa kurehemu.
Kadiri ya Qurani Allah
anayo nafsi pia Tazama Qurani 5:116. Kwa hivyo hapa tunaonaAllah ana agiza watu
wasizitakase nafsi zao na tena anasema sijitakasi nafsi yangu. Hii ni ajabu
sana!
Mungu wetu Yehova
anavyosema kuhusu kujitakasa nafsi, yaani utakatifu:
Isaya 43:3
Maana mimi ni BWANA Mungu
wako, mtakatifu wa Israeli, mwokozi wako. Nimekutoa Misri kwa ukombozi wako,
nimetoa Kushi na Sheba kwa ajili yako.
Hapa tunaona Mungu anasema
‘Mimi ni mtakatifu’, hili pia ni jina la sifa la Mungu wetu Yehova kwa lugha ya
Kiebrania husema ‘kadosh’. Nabii Isaya ameandika kuwa Mungu ni Mtakatifu mara
32 kwa ufupi tu soma Isaya 40:25, 48:17 na 57:15. Isitoshe kwa kuwa Mungu wetu
Yehova ni mtakatifu pia aliagiza kwetu hivi.
Walawi 11:44
Kwa kuwa mimi ni BWANA
Mungu wenu takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni
mtakatifu, wala msitie uchafu nafsi zenu…
Mtume Petro anatuagiza
hivi;
1 Petro 1:15-16
Bali kama yeye aliyewaita
alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote.Kwa
maana imeandikwa, mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
Mtume Paulo pia ameagiza
kujitakasa nafsi na kuwa watakatifu(2 Wakorintho 7:1) waweza pia kusoma agizo
hilo la kuwa watakatifu katika Walawi 19:2, 20:26.
Kwa hivyo tunaona Yehova
anaagiza tujitakase nafsi zetu ili tuwe watakatifu, lakini Allah anaagiza kwa
Waislamu kuwa wasizitakase nafsi zao.
Swali kwako mfuatiliaji,
Je, Allah ndiye Yehova?
7: Je, mbingu ya Yehova ni
sawa na pepo (mbingu) ya Allah?
Mbingu ya Yehova:
Luka 20:34-36
Yesu akawaambia wana wa
ulimwengu huu huoa na kuolewa, lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili
kuupata ulimwengu ule. Na kule kufufuka katika wafu hawaoi wala hawaolewi. wala
hawawezi kufa tena. Kwa sababu huwa sawa sawa na malaika, nao ni wana wa Mungu
kwa vile walivyo wana wa ufufuo.
Maandiko haya
yanatuthimbitishia Wakristo kuwa tutakapofufuliwa na kuingia mbinguni, hakuna
mambo ya kuolewa wala kuoa, maana tutakuwa na miili ya kiroho (1 Korintho
15:43-54) Aidha maandiko yanatufundisha kuwa ufalme wa Mungu siyo kula wala
kunywa bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. (Tazama Warumi
14:17). Mungu wetu anafundisha wazi wazi kuwa kule mbinguni katika ufalme
hakuna njaa, wala kiu wala jua kutupiga (Ufunuo 7:16-17.)
Pepo au Mbingu ya Allah
itakuwa hivi:
i). Maghorofa
Qurani 39:20 Suratul Zumar
(makundi/vikosi)
Lakini waliomcha mola wao
watapata ghorofa zilizojengwa juu ya ghorofa chini (mbele) yake hupita mito.
Ndiyo ahadi ya Mwenyenzi Mungu, Mwenyenzi Mungu havunji ahadi yake.
ii) mito ya maji, maziwa,
ulevi, asali na matunda
Qurani 47:15 Suratul
Muhammad
Mfano wa pepo waliyoahidiwa
watawa (wacha Mungu itakuwa hivi). Imo mito ya maji yasiyovunda, na mito ya
ulevi wenye ladha kwa wanywao na mito ya asali iliyosafishwa. Tena humo
watapata matunda ya kila namna, na samahani kutoka kwa mola wao. Basi hao watakuwa
sawa na wale wataokaa motoni na kunyweshwa maji yachemkayo yatakayokata chango
zao?.
Je Matunda hayo ni sawa na
ya wapi?
Qurani 2:25 Suratul Al-
Baqarah (ngombe jike)
Na wabashirie walioamini na
kufanya vitendo vizuri, kwamba watapata mabustani yapitayo mito mbele yake.
Kila mara watakapopewa matunda humo kuwa ni chakula watasema “haya ndiyo yale
tuliyopewa zamani (ulimwenguni) kwani wataletewa (matunda hayo) hali yatakuwa
yamefanana (na yale waliyokuwa wakiyajuwa ulimwenguni wataletewa kwa sura hiyo
lakini
utamu mwingine kabisa) na
humo watapata wake waliotakasika (na kila mabaya na machafu) na watakaa milele
humo.
iii). Watapata wanawake
aina hizi na nyama za ndege
Qurani 56:15-23 Suratul Al
Waaqiah (Tukio) nanukuu aya ya 21-23 tu
Na nyama za ndege kama
watakavyotamani (wenyewe). Na wanawake wenye macho mazuri na makubwa (ya
vikombe). (wanapendeza na safi) kana kwamba ni lulu zilizofichwa (katika
machaza yake, ndio kwanza zinapasuliwa)
Qurani 37:48-49 Suratul
As-Saaffat (Wapangao mistari)
Na pamoja nao watakuwa
wanawake wenye macho mazuri makubwa. (Safi) wanawake hao kama mayai (ya mbuni)
yaliyohifadhiwa.
Qurani 37:44-46 Suratul
As-Saaffat (Wapangao mistari)
Wako juu ya vitanda (viti
vya enzi vya fahari), wamekabiliana (wanazungumza). Wanazungushiwa gilasi zenye
(vinywaji) safi.Vyeupe yenye ladha kwa hao wavinywao.
Kupitia aya hizi tumeona
kuwa Allah Sub-haana Wataala Mungu anayeabudiwa na Waislamu ametoa ahadi ya
kuwaingiza Waislamu peponi (mbingu) na kuwa watapata mito ya maji, mito ya
maziwa na ulevi na pia mito ya asali vilevile watapata matunda,nyama ya ndege
na pia wataozeshwa na Allah mungu wao wanawake wenye macho makubwa kama mayai
ya mbuni. na wengine makubwa kama vikombe.
Jambo la kushangaza zaidi
ni pale tunaposoma kitabu cha Hadithi, maana imani ya Dini ya Uislamu imejengwa
pia katika vitabu vya hadithi. Soma
Qurani 42:10 Suratul
Ash-Shuura (mashauriano)
Mkihitalifiana katika jambo
lolote (rejeeni kitabu cha Mwenyenzi Mungu na Hadithi za mtume kwani)…
Tunaposoma kitabu cha
Hadithi ya mtume kiitwacho Sunnan Ibn-1- Majah vol 5 ukurasa wa 546 Hadithi No:
4337 kuna maelezo haya
Imesimuliwa na Abu' Umama
ya kuwa mjumbe wa Allah (baraka na amani ya Allah iwe juu yake) alisema Allah
hatamruhusu yeyote kuingia peponi ila kwa idhini ya Allah, Mwenye nguvu na
utukufu naye atamwozesha mwanamume wake sabini na mbili. Wawili watakuwa
mabikira (mahurul-ain) yaani wanawake wa peponi wenye macho makubwa, na sabini
watakao warithi ambao watu (mabwana zao) wametupwa katika moto wa jahanamu kila
mmoja wao (hao wanawake) wana uke wa kupendeza. Na mwanamume, Nguvu ya uume
wake katika kujamiana hautapinda (kusinyaa) bali utadumu sana
Kwa kiingereza Hadithi hii
inasomeka hivi:-
Abu-Umama (Allah be pleased
with him) reported that Allah's messenger (peace and blessings of Allah be upon
him)said Allah will not admit anyone in the paradise but Allah the mighty and
Glorous, will marry him with seventy two wives two will from virgins (haurine)
with big eyes and seventy will be his inheritance from the people of the Hell-
Fire (1).Everyone of them will have apleasant vagina and he (the man) have
sexual organ that does not bend down (during sexual intercouse)
Hivi ndivyo Allah Mungu wa
Waislamu alivyoahidi. Hili ni jambo ambalo kwa Mkristo linamshangaza sana kwani
jambo hili linalofundishwa na Allah halipo kabisa kwa Mungu wetu Yehova hapa
ulimwenguni ndiko kwenye ulevi,matunda,nyama za ndege, kuoana, maghorofa,
magari, mito, bahari na vinginevyo.
Tafakari, je huyo Allah ni
nani?
8: Mwisho wa wanaomwabudu
Allah ni wapi?
Tunajua kuwa Wakristo
tutaishi na Mungu wetu Yehova milele (tazama 1Thesalonike 4:13-17 na Ufunuo
21:3-7) Hivyo Mungu wetu hana mwisho ni wa milele. Lakini tunaposoma Qurani na
Hadithi za Muhammad, mtume wa Waislamu tunaona mafundisho haya…
Qurani 51:56
Suratul-Adh-Dhaariyat (upepo)
Sikuwaumba majini na watu
ila wapate kuniabudu
Qurani 6:128 Suratul Al
An-Am (Wanyama)
Na (wakumbushe) siku
atakapowakusanya wote (awaambie) "Enyi makundi ya majini! Hakika nyinyi
mmechukua wafuasi wengi katika wanaadamu" na marafiki wao katika wanadamu
(watawagombania) waseme "mola wetu! Tulinufaishana sisi na wao, na
tumefikia muda wetu uliotuwekea" Basi (Mungu) atasema:"moto ndio
makazi yenu, mtakaa humo milele…..
Katika aya hizi tunaona
kuwa majini pamoja na watu wote watatupwa motoni. Je Allah naye ni vipi?
tunaposoma kitabu cha hadith za mtume (s.a.w) cha Sahih al-Bukhari Vol: VI
Hadithi No: 371.ukurasa wa 353 Kuna maneno haya:
Qurani 50:30 Suratul Qaf
(kuapa)
Siku tutakayoiambia
Jahanamu, ‘Je! Umejaa?’ Nayo itasema ‘Je kuna ziada (zaidi?Naije tu!
)
Imesimuliwa na Anas kuwa:
mtume alisema watu watatupwa jahanamu, Naye Allah ataiuliza jahanamu akisema je
umejaa nayo jahanamu itasema kwani kuna nyingine zaidi na ije tu? Mpaka Allah
atakapo ingiza mguu wake nayo jahanamu itasema inatosha! Inatosha
Kwa kiingereza Hadithi hii
inasomeka hizi:-
Allah's statement:It (Hell)
will say Are there any more (to come)? (50:30).
Narrated Anas: The prophet
said the people will be thrown into the (Hell) Fire and it will say Are there
any more (to come)?' (50:30) till Allah puts His Foot over it and it will say
Qai! Qat!(Enough! Enough!)
Katika aya hii tunaona
Allah mungu wa Waislamu anaiuliza Jehanamu kama imejaa, nayo Jehanamu
itamuuliza Allah je, kuna zaidi. Yaani swali hili linaonyesha kuwa Jahanamu
ilikuwa bado haijajaa,.
Maelezo ya Hadithi hii
inadhibitisha kuwa Allah ataingiza mguu katika Jahanamu na ndipo Jahanamu
itakaposema kuwa inatosha! Inatosha!, yaani imejaa kwa tendo la Allah kuingiza
mguu wake humo. Jambo hili ni tofauti kabisa na ilivyo kwa Mungu wetu Yehova.,
Mungu wetu ameiweka jahanamu maalum kwa ajili ya watu wabaya, na ibilisi,
pamoja na malaika zake. Tafadhali soma aya hizi; Mathayo 25:41,46, Ufunuo
20:10, 21:8.
Aya hizi zote zinaonyesha
kuwa mwisho wa wabaya, Ibilisi na malaika zake ni katika ziwa la moto. Swali
kwako Ndugu mpendwa, Je, Allah ni nani?
Ni matumaini yangu kuwa
umeweza kujua kwa undani kupitia Qurani na Biblia na vitabu vya Hadith za mtume
wa Waislamu aitwae Muhammad kuwa Allah Sub-Haana Wataala Mungu anayeabudiwa na
Waislamu. Siyo Yehova Mungu tunaye muabudu Wakristo.
No comments:
Post a Comment