Adhama ambazo zina Yahweh
pekee apatiwa Yesu Kristo:
1.
Yesu aliumba Ulimwengu:
Wakolosai 1: 16-17
Inasema: 16 Yeye ndiye aliyeumba vitu vyote mbinguni na duniani; vitu
vinavyoonekana na visivyoonekana; kama ni viti vya enzi au nguvu, au watawala
au milki na mamlaka: vyote viliumbwa na yeye kwa ajili yake. 17 Yeye alikuwapo kabla ya vitu vingine vyote na kwa uwezo wake
vitu vyote vinahusiana kwa mpango.
Jambo hili lauumbaji lazima tuliwekee msisitizo
kwasababu inafahamika kuwa ni Yahweh ndie aliye umba Ulimwengu, lakini katika
kitabu hiki cha Wakolosai tunaona kuwa Yesu nayeye anapewa adhama hiyo ya
uumbaji.
2.
Yesu anapewa adhama ya Umilele ambayo ni sifa pekee ya Mungu.
Yohana 8:58 Inasema: 58 Yesu akawa jibu, “Nawaambia wazi, kabla Abrahamu
hajazaliwa, ‘Mimi nipo.’
Katika hiyo aya, Yesu anadai na kusema kuwa Kabla ya Ibrahimu kuwepo,
yeye Yesu alikuwepo!!! Hii sifa ni ya Kimungu Pekee, kwani Mungu ndie pekee
alikuwepo kabla ya uumbaji.
Na kwababu hiyo, Wayahudi wakashika Mawe ili wampige nayo Yesu.
Sasa tujiulize, je hawa Wayahudi wangetaka kumpiga Mawe Yesu kama
haingekuwa ya kuwa alisikikika akikufuru kwa kusema yeye ni Mungu?
Ngoja tuongeze ushaidi zaidi wa Umilele kutoka
Yohana 17: 5
5 Na sasa Baba nipe mbele yako ule utukufu niliokuwa nao pamoja
na wewe hata kabla dunia haijaumbwa.
Katika hii aya, Yesu anadai kwamba aliishi na Baba kabla ya dunia
kuumbwa. Haya maneno ni ushaidi tosha kuwa kumbe Yesu aliishi kabla ya dunia
kuumbwa na alikuwepo wakati wa uumbaji wa dunia.
3.
Yesu
anapewa sifa ya kuwa kila mahali: (Omnipresent)
Mathay0 18:20, na Mathayo 28:20 Inasema:
20 Kwa maana wanapokutana watu wawili au watatu katika jina
langu, hapo mimi nipo pamoja nao.”
Sifa ya kuwa kila
mahali kwa wakati mmoja ni ya Mungu pekee, lakini Yesu anasema yeye hiyo sifa
ni yake na anayo.
4.
Yesu ana adhama ya kufahamu yote:
Mathayo 16:21
Yesu
Anazungumza Juu Ya Mateso Yake
21 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaeleza
wanafunzi wake kwamba hana budi kwenda Yerusalemu na kupata mateso mengi kutoka
kwa wazee, makuhani wakuu na walimu wa sheria; na kwamba atauawa na siku ya
tatu atafufuliwa.
5.
Yesu anapewa ADHAMA YA Mungu
ya MUWEZA wa Yote:
Yohana 11: 38-44
Yesu
Amfufua Lazaro
38 Yesu akafika penye kaburi akiwa amefadhaika
sana. Kaburi lenyewe lilikuwa katika pango ambalo mlango wake ulikuwa umezibwa
kwa jiwe.39 Akasema, “Ondoeni hilo jiwe.” Dada yake mare
hemu, Martha, akasema, “Bwana, patakuwa na harufu kali kwani siku nne zimepita
tangu azikwe.” 40 Yesu akamjibu, “Sikukuam bia kama
ungeamini ungeuona utukufu wa Mungu?” 41 Kwa hiyo
wakaliondoa lile jiwe. Yesu akaangalia mbinguni akasema, “Baba ninakushukuru
kwa kunisikia.
No comments:
Post a Comment