Zaheed alizaliwa kwenye familia ya Kiislamu. Baba yake na kaka zake wote walikuwa viongozi wa dini ya Kiislamu. Zaheed naye alifuata mkondo uleule.
Mara baada ya kuhitimu masomo ya dini na kukabidhiwa msikiti, chuki yake na kutokuwa na uvumilivu dhidi ya Wakristo kulianza kujionyesha waziwazi.
Zaheed anasema, “Nilikuwa nawakusanya vijana kwenye msikiti wangu na kuwachochea dhidi ya Wakristo. Niliwaambia kuwa Wakristo ni makafiri. Niliwaambia waende wakawapige Wakristo kwa fimbo na kwa nondo. Niliwaambia kuwa Allah anafurahi wakifanya hivyo. Tulikuwa tukichoma moto Biblia tunazozikusanya.”
Zaheed anaendelea kusema, “Lakini siku moja, nilijisikia tu nichukue Biblia moja niende nayo nyumbani. Nilikuwa naisoma ili niweze kutafuta mambo yanayotatanisha ili niweze kuyatumia dhidi ya imani ya Kikristo. Ghafla, nuru kubwa iliangaza kwenye chumba changu. Halafu nikasikia sauti ikiita jina langu. Nuru ile ilikuwa kali sana. Iliangaza chumba kizima. Ile sauti ikauliza, ‘Zaheed, kwa nini unanitesa?’ Niliogopa. Sikujua cha kufanya. Nilidhani ninaota. Kwa hiyo nikauliza, ‘Wewe ni nani?’ Kisha nikasikia, ‘Mimi ni njia, na kweli, na uzima.’”
Zaheed anasema, “Kila usiku, kwa siku tatu zilizofuata, ile nuru ilinilazimisha kukiri. Na usiku wa nne, nilimkubali Yesu kama Mwokozi wangu.”
Kutokana na kile kilichotokea, Zaheed alienda kwa ndugu zake msikitini ili kuwashirikisha kile ambacho kilimkuta. Matokeo yake, kwa kuwa sasa alihesabika kuwa muasi wa dini yake ya mwanzo, alikabidhiwa kwa askari.
Zaheed anaendelea kusema, “Niliwekwa gerezani kwa miaka miwili. Na katika kipindi hicho chote, askari walinitesa tena na tena. Wakati fulani walinining’iniza kwa nywele zangu kwenye feni na kuniacha hapo. Wakati mwingine walining’oa kucha zangu wakitaka niikane imani yangu katika Kristo. Lakini pamoja na kwamba niliteseka sana mikononi mwa washitaki wangu wa Kiislamu, sikuwa na chuki dhidi yao. Maana miaka michache iliyotangulia, nilikuwa mmoja wao.”
Zaheed anasema, “Wakati wa hukumu yangu, nilipatikana na kosa la kukufuru. Na kulingana na sharia, nilitakiwa kunyongwa. Walijaribu kunilazimisha kukana imani yangu kwa Yesu. Waliniambia kuwa nikikubali, hawatanipiga tena, ningeachiwa huru. Lakini nisingeweza kumkana Yesu. Muhammad hakuwahi kunitembelea mimi. Lakini Yesu alinitembelea! Ninajua kuwa Yeye ndiye kweli. Kwa hiyo nilimwomba tu Mungu nikitumaini kuwa na wao watafika mahali wamjue Yesu.”
Hatimaye iliwadia siku ambayo Zaheed alitakiwa kunyongwa. Akiwa hana hofu ya kifo, alijaribu hata kuwaambia askari habari za Yesu wakati akipelekwa kwenye sehemu ya kunyongewa, maana tayari alishakubaliana na hali yake – kwamba alikuwa ni wa kufa tu. Lakini Mungu alikuwa na mipango mingine kabisa.
Kabla tu ya kunyongwa, amri isiyotarajiwa ilitolewa na mahakama kwamba Zaheed aachiwe huru. Amri ile ilisema kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha dhidi yake. Hadi leo, hakuna mtu anayejua kwa nini Zaheed aliachiwa huru.
Zaheed anasema, “Sasa najisikia kuwa Yesu alinitembelea mara mbili. Kwanza, nilipokuwa mtesi wa watoto wake. Na pili, nilipokuwa niko karibu na kunyongwa.”
Zaheed alibadili jina lake na kuitwa Lazaro, ikiwa ni ishara ya kuponea chupuchupu kwenye mauti kama ilivyokuwa kwa Lazaro wa Biblia aliyefufuliwa na Bwana Yesu.
Ingawaje Wakristo wengi hawakumwamini mwanzoni, hivi sasa wamemkubali kama sehemu ya familia yao. Na anasafiri kutoka kijiji hadi kijiji.
Zaheed anasema, “Naishi kwenye nchi inayotawaliwa na mafundisho ya uongo ya Uislamu. Watu wangu wamepofushwa. Nami nilichaguliwa na Mungu ili niwe sauti yake. Ninajihesabu kuwa mateso niliyopitia si lolote si chochote ukilinganisha na furaha ya kumjua Yeye – Njia, na Kweli, na Uzima!”
**********
Ndugu msomaji, Mungu yuko kazini. Tumepewa muda huu mfupi katika maisha haya ili tuchague kumfuata Yesu au tuamue kufuata dini – ziwe ni za Kikristo au za aina nyingine. Si kila mtu atapata neema ya kutembelewa moja kwa moja na Kristo mwenyewe kama ilivyokuwa kwa Zaheed. Msingi wa kuingia mbinguni ni kumwamini Yesu Kristo PEKEE!
Dini yako haitakusaidia kamwe kuingia mbinguni. Yesu Kristo pekee ndiye Njia, na Kweli, na Uzima. Njoo kwake LEO upate uzima wa milele bure.
Huenda unatamani kuja kwa Yesu ila unaogopa kutengwa na ndugu zako. Ni kweli hayo yanaweza kutokea. Lakini, kama ulivyomsoma au kumsikia Zaheed, na hivyo ndivyo ilivyo, kumjua Yesu ndilo jambo kubwa na la milele kuliko kumkataa kwa sababu ya hofu ya kutengwa na ndugu. Ndugu hawana mbingu ya kukupeleka. Yesu anayo mbingu.
Labda pia umetishwa kwamba, ukiacha dini yetu hatutakuzika. Hii huwa ni sababu ya kuchekesha sana. Kwani wewe ukifa, kama hawataki kukuzika, anayepata shida ni wewe au ni wao? Tangu uzaliwe ulishawahi kuona watu wangapi walioacha kuzikwa kwa lengo la kuwakomesha?
Yesu ndiye Njia, na Kweli, na Uzima. Anakuita leo. Anakungoja siku zote kwa upendo na shauku nyingi ili akupe uzima wa MILELE alioandaa kwa ajili yako. LAKINI KUMBUKA, HATAKUNGOJA MILELE! AMUA SASA!
No comments:
Post a Comment