Thursday, September 19, 2013

Mungu Amwonyesha Nabeel Njia ya Kweli Kati ya Uislamu na Ukristo - Sehemu ya 1




Nabeel alizaliwa na kukulia kwenye familia na maisha ya kiislamu. Uislamu ulikuwa ni kila kitu kwake. Lakini wakati ulipofika wa yeye kujua jema na baya, alianza kujihoji kuhusu maisha yake, Mungu wake, na hatima yake ya milele. Hatimaye alimwomba Mungu amwonyeshe kweli. Je, nini kilitokea? Tafadhali fuatilia sehemu hii ya kwanza ya ushuhuda huu.

……………………………………

 Nilipokuwa mdogo, wazazi wangi walikuwa wacha Mungu sana. Mimi nami nilikuwa mcha Mungu sana kwa sababu yao. Wazazi wangu walinifundisha kumwomba Allah kila wakati. Niliswali sala tano kwa siku ambazo ni za lazima. Lakini pia niliswali swala zaidi ya hizo. Swala ilikuwa ni sehemu muhimu kabisa ya maisha yangu. Kila nilipoamka asubihi niliomba mara tu nilipofungua macho yangu. Kisha nilipoenda bafuni, nilikuwa nikiomba swala ya wakati wa kuosha mikono yangu. Pia niliomba swala kabla ya kusoma Quran na mara baada ya kusoma Quran, ambayo niliisoma karibu kila siku.

Uislamu ulikuwa ndani yangu kabisa. Hivyo, wazazi wangu walikuwa wananifurahia sana maana nilikuwa ni aina ya mtoto wa Kiislamu ambaye walikuwa wanajivunia kumlea. Nilitokea kwenye familia ya kimisionari. Allah na mtume Muhammad walikuwa wanaheshimiwa sana. Allah alikuwa anaabudiwa muda wote.

Uislamu kwetu haukuwa tu ni dini, bali ulikuwa ni maisha yetu kabisa. Halikuwa ni jambo tulilofuata tu, bali zaidi sana hivyo ndivyo tulivyokuwa sisi wenyewe. Kwa hiyo, Uislamu ulikuwa ndiyo sehemu kabisa ya utu wangu.

Kulikuwa na mjadala wa wazi siku moja nikiwa niko chuoni. Ulikuwa ni mwaka wangu wa kwanza na nikiwa na miaka 18. Nilikuwa nina rafiki yangu mmoja aliyeitwa David, ambaye alikuwa kwenye timu ile ya wazungumzaji. Mimi na David tulikuwa tukikaa chumba kimoja. Usiku ule kabla ya kulala, alitoa Biblia akaanza kusoma. Kusema kweli, nilikuwa sijaona mtu akisoma Biblia wakati akiwa hana kazi (in free time).  Nilikuwa tu nikiona watu wakisoma wanapohubiri, au wananukuu maandiko wanapoongelea habari zake. Lakini sikuwa nimeona mtu akiisoma wakati akiwa tu amepumzika.

Nilimwambia, “David, unajua kuwa Biblia hiyo ilishabadilishwa na watu; si Biblia ileile ambaye alifunuliwa Kristo?”

David alikuwa ni mtu ambaye anasoma Biblia, anasoma kuhusiana na Biblia, anasoma sababu za kwa nini tunatakiwa kuamini Biblia – kwa hiyo, alikuwa yuko tayari kabisa kwa swali kama hilo kuliko ambavyo ningetegemea.

David aliniambia kwamba Biblia haijabadilika. Kuna sayansi ambayo inaitwa ‘textual criticism’ ambayo tunaweza kuitumia ili kubaini kama Biblia imebadilishwa au la. Tulifanya hivyo na nikagundua kwamba Biblia haijabadilishwa kama inavyodhaniwa.

Niligundua kwamba hakuna fundisho (doctrine) lililobadilishwa. Biblia imebakia ileile tangu mwanzo. Biblia inasema kuwa Kristo ni Bwana; na kwamba alikufa kwa ajili ya dhambi zetu; akafufuka kutoka kwa wafu siku ya tatu; na haijasema kitu kingine chochote.

Kwa hiyo, ilikuwa ni baada ya miaka michache, ndipo baadaye nikaanza kutambua kwamba, labda sikuwa kwenye njia sahihi. Ilinichukua miaka kadhaa ya mijadala na utafiti kugundua ukweli huu.

Upo ushahidi mwingi sana unaoonyesha kuwa Biblia imebakia ileile tangu mwanzo; jambo ambalo sivyo kwa Uislamu. Ilinichukua miaka mitatu na nusu kufikia pale, yaani kutambua kuwa mambo haya ni kweli; na kwamba kila kitu nilichowahi kufundishwa – nilimpenda Allah, niliupenda Uislamu, nilimpenda Muhammad, niliwapenda wazazi wangu, nilipenda kila kitu ambacho nilikulia humo. Lakini hilo halikufanya mambo hayo kuwa kweli.

Nilianza kumwuliza Mungu, nikisema, “Mungu, siwezi kujua ukweli mimi binafsi. Tafadhali, nionyeshe kweli ni ipi. Chochote ninachotakiwa kufanya; hata kama kitaniumiza – hata kama familia yangu itanikataa; hata kama marafiki zangu watanikataa – vyovyote iwavyo, nitafuata njia hiyo.”

Ninapotafakari leo, nagundua kuwa hata sikujua sawasawa nilichokuwa nakiomba. Nilimwomba na kumwomba sana Mungu. Siku moja nilikuwa hotelini na nilimwomba Mungu kwa unyenyekevu mkubwa sana. Nilisema, “Mungu, sielewi. Siwezi kujua. Uzima wangu wa milele umo mashakani. Nakuomba uniambie kweli ni ipi – iwe ni kwa maono, kwa ndoto, au vyovyote vile.”

Usiku ule, nikiwa kwenye chumba cha hoteli ile, baba yangu alikuwa amelala kwenye kitanda chake na mimi kwenye kitanda changu pembeni yake. Yeye tayari alikuwa ameshalala. Kulikuwa na nuru kidogo, lakini mara nilipomaliza kuomba hivyo, kila kitu kilikuwa giza. Hakukuwa tena na nuru chumbani. Nikaona mbele ya macho yangu, mamia au hata maelfu ya misalaba! Niliitazama kwa mshangao. Na mara ikapotea.

Nilijua nini kimetokea. Nilikuwa nimeona maono, lakini bado sikutaka kuamini. Kwa hiyo, nilitazama juu na kusema, “Mungu, hayo siyahesabu. Inawezekana ni macho yangu tu yamenichezea mchezo.”

Kisha nikasema, “Unajua Mungu, tusahau kuwa niliomba unionyeshe maono. Hebu nipe ndoto. Ndoto yoyote tu ambayo inathibitisha yale niliyoyaona kwenye maono. Ukifanya hivyo, basi nitakuwa Mkristo.”

Haikuchukua wiki; haikuchukua mwezi;  ilichukua saa chache tu! Aliniletea ndoto usiku ule! Katika ile ndoto, nilikuwa nimesimama mlangoni kwa nje. Vidole vyangu vya miguu vilikuwa vimegusa kizingiti.  Ulikuwa ni mlango mwembamba wenye urefu na upana wa kunitosha tu mimi.  Kwa ndani, alikuwapo rafiki yangu, David. Alikuwa amekaa mezani pamoja na mamia ya watu wengine. Walikuwa wako tayari kula chakula ambacho kilikuwa mezani, lakini walikuwa hawajaanza kula bado. Walikuwa wanamngoja mzungumzaji aje ili mlango ufungwe na aanze kusema chochote kile kilichotakiwa.

Nilimtazama David na kusema, “Nilidhani kuwa tutakula pamoja!” Bila hata kunitazama, David alinijibu, “Haukuitikia mwito.” [You never responded].

Hivyo tu ndivyo ndoto ilivyokuwa. Niliamka na mara moja nilitambua ndoto ile ilimaanisha nini. Chumba kile kilikuwa ni mbinguni; kilikuwa ni Ufalme wa Mungu.  Na mimi nilikuwa nimesimama nje tu ya mlango wa Ufalme huo.

……………………………

Ndugu msomaji, tafadhali fuatilia ushuhuda huu wa Nabeel katika sehemu ya pili na ya mwisho. Bwana Yesu akubariki sana.

Tafakari.

Jihoji.

Kweli imo ndani yako.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW