Monday, May 6, 2013

Yesu alikuwa wapi katika siku tatu toka siku ile ya kufa mpaka kufufuka?

Image may contain: outdoor and text
Kama Yesu alivyotabiri, alisalitiwa na mmoja wa wafuasi wake, Yuda Iscariot, na alikamatwa. Katika shitaka la kufedhehesha chini ya Gavana wa Kirumi, Pontio Pilato, alitiwa hatia ya uhaini na alilaaniwa kufa kwenye msalaba wa mbao. Kabla ya kupigiliwa misumari msalabani, Yesu alipigwa kwa ukatili kwa mjeledi wenye mifupa vyuma ambao ulinyofoa nyama. Alisukumwasukumwa, alipigwa mateke, na alitemewa mate.
Yesu akamwambia (mwizi aliyetubu) Amini nakwambia, leo utakuwa pamoja paradiso .
.
Luka 23:39 Mmoja wa wale wahalifu waliotundikwa msalabani, alimtukana akisema: "Je, si kweli kwamba wewe ndiwe Kristo? Basi, jiokoe mwenyewe, utuokoe na sisi pia." 40 Lakini yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake akisema: "Wewe humwogopi Mungu hata kidogo? Wewe umepata adhabu hiyohiyo. 41 Wewe na mimi tunastahili, maana haya ni malipo ya yale tuliyotenda. Lakini mtu huyu hakufanya chochote kibaya." 42 Kisha akasema, "Ee Yesu! Unikumbuke wakati utakapoingia katika ufalme wako." 43 Yesu akamwambia, "Nakwambia kwa hakika, leo utakuwa pamoja nami peponi."
Hii inathibitisha kuwa roho ya Yesu na yule Mwizi aliyetubu hazikukoma kuishi bali zilikwenda Paradiso . Je, huko ndipo alipo kuwa Yesu kwa siku tatu?
Petro wa kwanza 3:18-19 inaeleza, “kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi zetu, mwenye haki kwa ajili yao wasiohaki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake ukauawa, bali roho yake ikahuishwa, ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokuwa kifungoni akawahubiri.”
Siku tatu kuu za Pasaka ndizo kiini cha mwaka wa Kanisa.
Zinamuadhimisha Yesu mteswa, mzikwa na mfufuka, yaani siku ya kwanza (Alhamisi kuu jioni hadi Ijumaa kuu jioni) inaadhimisha mateso yake kuanzia karamu ya mwisho hadi kifo cha msalaba; siku ya pili (Ijumaa kuu jioni hadi Jumamosi kuu jioni) inaadhimisha maiti yake kubaki kaburini na roho yake kushukia kuzimu; siku ya tatu (kuanzia Jumamosi kuu jioni hadi Jumapili ya Pasaka jioni) inaadhimisha ufufuko wake mtukufu.
Petro wa Kwanza 3:18-22 inaeleza ushikamano wa kuteswa kwake Kristo (fungu la 18) na kutukuzwa kwake (fungu la 22). Petro ndiye anayefafanua yaliyotokea katikati ya matukio haya mawili. Neno “alihubiri’ katika fungu la 19 lina maana ya kuwa aliwasilisha ujumbe. Yesu aliteswa na kufa msalabani, mwili ukiuawa na roho yake pia kufa kwa kufanywa dhambi. Lakini roho yake ilifufuliwa naye akaikakabidhi Baba. Kulengana na Petro, muda huo baada ya kufa mpaka kufufuka Yesu aliwasilisha hali Fulani ya ujumbe kwa “roho waliokuwa kifungoni.”
Bwana wetu aliikabidhi roho yake kwa Baba, akafa na wakati Fulani toka kufa mpaka kufufuka, akatembelea kuzimu alikowasilisha ujumbe kwa viumbe vya kiroho 9 pengine ni malaika waasi tazama yuda 6) waliokuwa na uhusiano na nyakati za kabla gharika la wakati wa Nuhu. Kifungu cha 20 kinafafanua zaidi. Petro hakutuambia kilichoambiwa roho hawa waliokuwa kifungoni lakini haiwezi kuwa ilikuwa habari ya wokovu kwa kuwa malaika hawaokolewi (Waebrania 2:16). Pengine ilikuwa ni kutangazwa kwa kushindwa kwa shetani na milki yake (Petro wa kwanza 3:22; Wakolosai 2:15). Waefeso 4:8-10 pia inajaribu kueleza kuwa Kristo alienda “paradise” (Luka 16:20; 23:43) na akawachukua mpaka mbinguni wale waliokuwa wamemuamini kabla kufa kwake.
Biblia haifafanui wazi wazi kilichotendeka ndani ya muda wa siku tatu hizi toka kufa mpaka kufufuka. Haiwezi kueleweka ya kuwa alikuwa ameenda kuwapa watu nafasi ya pili ya kuokolewa kwa kuwa biblia inatuambia ya kuwa tunakutana na hukumu punde tu baada ya kufa (Waebrania 9:27).
Shalom
Max Shimba mtumwa wa Yesu Kristo.

No comments:

JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD "

 JESUS DECLARES THAT "HE IS THE LORD JEHOVAH GOD " Author: Dr. Maxwell Shimba  Jesus Declares, “I am the Alap and the Tau” – Under...

TRENDING NOW