Na. Mwl. Daniel Mwankemwa
Utangulizi:
Majini ni viumbe visivyoonekana kwa macho ya kawaida ya wanadamu. Hii ni kwa sababu viumbe hivi viko katika asili kutoonekana. Majini huitwa pia Ibilisi, shetani, pepo mchafu au joka la zamani.
ASILI YAO:
Kwa mujibu wa Biblia majini yalikuwa ni malaika kabla ya kuungana na yule muasi mkuu wa Mungu, yaani Lucifer aliyemuasi Mungu mbinguni na kutaka ukubwa wa kufanana na Mungu, na ndipo akatupwa huku duniani yeye pamoja na malaika zake, na huku wakiwa wamenyanganywa utukufu waliokuwa nao hapo awali. Vita hivyo viliongozwa na malaika mkuu wa Mungu wa Mbinguni yaani Yahweh(Yehova) kumtupa chini huyo malaika muasi pamoja na malaika zake. Viumbe hivyo vilivyotupwa ndivyo leo vinaitwa MAJINI au MASHETANI au PEPO WACHAFU au IBILISI au JOKA LA ZAMANI.
Uf. 12:7-12 “Kulikuwa na vita mbinguni, Mikael na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake, nao hawakushinda wala mahala pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa yule mkubwa nyoka wa zamani aitwaye ibilisi na shetani audanganyaye ulimwengu wote, akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. Nikasikia sauti kuu mbinguni ikisema sasa kumekuwa wokovu na nguvu na ufalme wa Mungu wetu kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu yeye awashtakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. Nao wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo na kwa neno la ushuhuda wao ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. Kwa hiyo shangilieni enyi mbingu, nanyi mkaaao humo. Ole wa nchi na bahari! Kwa maana yule ibilisi ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi akijua ya kuwa ana wakati mchache tu.”
Hivyo kwa mistari au aya hizo unaanza kupata taswira ya kile tunachojifundiza kuusiana na majini.
Ki-Biblia malaika ni viumbe walio katika hali ya roho ila wanaweza kuonekana kwa umbile la mwanadamu. Mw. 18:1-18, Lk 1:26-28, Kut 3:1-6
Katika Ebr 1:13-14 “Yuko malaika aliyemwambia wakati wowote uketi mkono wangu wa kuume hata nitakapowaweka adui zako chini ya nyayo zako? Je, hao si ROHO watumikao wakitumwa kuwahudumia wale watakaourithi wokovu?”
Biblia inazidi kubainisha namna ya kuubwa kwao
Mw.2:1 “Basi mbingu na nchi zikamalizika na JESHI LAKE LOTE”
Ni katika jeshi hilo ambapo tunapata hawa viumbe vya kiroho.
Na katika Kol 1:1-16 “Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa vilivyoko mninguni na vilivyo juu ya nchi. Vinavyoonekana na visivyoonekana……….”
Jeshi hilo ni huru linaweza kujiamulia lolote na ndiyo maana 1/3 ya hao hao roho yaani malaika waliasi na kufanya machukizo mbele za Mungu na wakafukuzwa (Uf 12:7-12) na wengine wamefungwa.
Katika Yuda 6 “Na malaika wasiolinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu”
Kwa hiyo majini ndiyo mashetani na mashetani ndiyo majini. Katika kitabu cha
Lawi 17:7
“Wala hawatatoa tena sadaka zao Kwa wale MAJINI ambao huwafuata ili wafanye uasherati nao, sheria hii itakuwa sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao kizazi baada ya kizazi.”
Kwa sababu majini hayo tangu yalipotupwa toka mbinguni wana wa Israeli hawakuwa na ufahamu kwa kutosha kuyahusu, baadhi yao walijikuta wakiyatolea sadaka huku wakiamini kuwa wanamtolea Mungu sadaka. Na kumbuka kuwa mara nyingi wana wa Israeli walipotoa sadaka zao nyingi zilikuwa za wanyama na hivyo kutakiwa kujinja na kutoa damu ambayo ni sehemu kubwa ya chakula cha majini.
Katika Zaburi 106:34-40.
“ hawakuwaharibu watu wa nchi kama BWANA alivyowaambia, bali walijichanganya na mataifa wakajifunza matendo yao, bwakazitumia sanamu zao nazo zikawa mtego kwao naam walitoa wana wao na binti zao kuwadhabihu kwa MASHETANI wakamwaga damu isiyo na hatia, damu ya wana wao na binti zao walio watoa dhabihu kwa sanamu za kaanani. Nchi ikatiwa unajisi kwa damu.”
Ndivyo walivyotiwa uchafu kwa kazi zao, wakafanya uasharati kwa matendo yao. Hasira ya Bwana ikiwa juu ya watu wake akauchukia urithi wake.
Hivyo kutokokamana na kutokuonekana kwao hayo majini yaliwahujumu wana wa Israel hata yakawasababishia wamwasi Mungu kwa kuyatolea sadaka kinyume cha Mungu wa mbinguni aliyehai.
Katika Kumb. 32:17-20
“ walitoa sadaka kwa pepo si Mungu, kwa miungu mipya iliyotokea siku zilizo karibu ambayo baba zetu hawakuiogopa. Hamkumbuki muumba aliyekuzaa Mungu aliyekuzaa humkumbuki. Bwana akaona akawachukia kwa sababu ya kukasirishwa na wanawe na binti zake. Akasema nitawaficha uso wangu nitaona mwisho wao utakuwaje maana ni kizazi cha ukaidi mwingi watoto wasio imani ndani yao.”
Pia katika Math 12:43-45
“Pepo Mchafu amtokapo mtu hupitia mahali pasipo maji akitafuta mahali pa kupumzikia asipate. Halafu husema natarudi nyumbani kwangu nilikotoka hata akija aiona tupu imefagiwa na kupambwa, mara huenda akachukua pamoja naye pepo wengine Saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo, mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza..”
Katika Biblia tunaona kipindi Yesu alipotwaa mwili na kuja duniani, hao majini, au mashetani au ibilisi au mapepo wachafu yalimfahamu na yalianza kulalamika mbele zake.
Math 8:28-31 “ Naye alipofika ng’ambo katika nchi ya wagerasi, watu wawili wenye pepo (majini) walikutana naye, wanatoka makaburini wakali muno, hata mtu asiweze kuipitia njia ile. Na tazama wakapiga kelele wakisema wakisema tuna nini nawe Mwana wa Mungu? Je, umekuja kututesa kabla ya muhula wetu…(MK 5:1-9)
Majini hayo yanafahamu kuwa Yesu ndiye atakayewahukumu ila yalichoshangaa ni kwamba mbona amewahi kabla ya kipindi chenyewe cha yeye Yesu kuyahukumu kwenda jehanamu ya moto!?
Yesu alikuja duniani ili kumwokoa mwanadamu kutokana na mateso ya hayo majini au mashetani kwa sababu katika Uf 12:12 Malaika Mikaeli alipokuwa anawafukuza hao malaika waasi yaani majini au mashetani alisema OLE WA NCHI NA BAHARIndiyo maana Yesu ilipidi aje duniani kupambana na huyo shetani, Joka, Ibilisi kwa niaba yetu maana sisi tusingeweza na wale majini walisema kumwambia Yesu kumwambia Yesu " ukitutoa tuache tukawaingie nguruwe na nguruwe wale wapatao 2000 waliona bora wafe baharini kuliko kuishi na viumbe hivi majini au mashetani miilini mwao na hivyo kutimiza ujumbe wa Malaika Mikaeli “ Ole wa nchi na bahari”.
Bahari ni sehemu mojawapo ambapo majini huishi.
Nguruwe hawa ni bora kuliko watu wa zama hizi zetu wanaokaa na majini kwa hiari yao na wengine hata kufunga ndoa na hawa majini.
Unabii wa kuangushwa mji mkubwa uliojisifu sana [ Babeli] ulipotolewa, ilitabiriwa kuwa, hayatakuwa tena makazi ya wanadamu, bali patabaki makazi ya majini..
Isaya 13:12. “Lakini huko watalala hayawani wakali wa nyikani na nyumba zao zitajaa bundi, mbuni watakaa huku, na majini watajeza huko.”
Ndipo tunasoma katika Yoh 12:31 Yesu anasema
“Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo, sasa Mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje”.
Na katika 1 Yoh 3:8
“ Atendaye dhambi ni wa ibilisi Kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi ili mwana wa Mungu alidhihirishwa ili azivunje kazi za Ibilisi.
Kama tulivyosoma toka sura na aya mbalimbali ndani ya Biblia kuwa majini hayo yanasubiri adhabu, Biblia inatueleza atakaye yahukumu.
Math 25:31, 41 “ Hapo atakapokuja mwana wa adamu pamoja na Malaika watakatifu pamoja naye……… Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto ondokeni kwangu mliolaniwa mwende katika moto wa milele aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake.”
Hivyo kwa mujibu wa Biblia majini yaani mashetani ni adui zetu na ndiyo maana alipokuja Muhammad yalianza kukanusha kuwa Mungu hana Mwana ili kuwavuruga waislamu wasijue kweli. (Soma Qurani 112:1-4, Al-Kahf, 18:3) ya kumwamini Mwana wa Mungu Yesu.
Kwa bahati mbaya sana mambo yanayohusu majini katika imani ya kiislamu ni tofauti sana na vile tulivyosoma katika Biblia. Ingawa Qurani na Hadithi za Muhammad, Mtume wa waislamu vinatutaka sisi Wakristo tumwamini Allah S.W. Mungu anayeabudiwa na Waislamu Misikitini
Katika Suratul Waqia 51:56.
“Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu”
Katika Qurani Suratul Al-Ankabut (Buibui), 29:46-47
“Wala msibishane na Watu waliopewa Kitabu kabla yenu ila kwa yale majadiliano yaliyo mazuri isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao na semeni tuyaamini yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu na Mungu wetu na Mungu wenu ni mmoja nasi ni wenye kunyenyekea kwake.”
Waliopewa Kitabu kwa mujibu wa Qurani ni Wayahudi na Wakristo. Je, hoja kuwa Mungu wetu na Mungu wao wanayemwabudu kuwa ni mmja je ni sahihi?. Tuchunguze kuhusiana na mafundisho ya Allah S.W wa misikitini kuhusu majini ndipo tutajua ni mmoja au la!.
Muislamu yeyote ili imani yake ikamilike ni lazima aamini yanayoonekana na yasiyoonekana.
Katika Suratul Al- Baqarah (ng’ombe Jike wa Njano), 2:1-3.
“Alif lam mym. Hiki ni kitabu kisochokuwa na shaka ndaniyake ni uongozi kwa wamchao Mwenyezi Mungu ambao huyaamini yasiyoonekana (maadamu) yamesemwa na Mwenyesi Mungu na Mtume wake) husimamisha sala na hutoa katika yale tuliyowapa.
Qurani peke yake ukiichunguza utaona kuwa majini yamechukuliwa kama ni viumbe tofauti na mashetani, , wanasema hivyo kwa sababu katika uislamu majini yamepewa hadhi kubwa sana na ya kipekee. Hadhi hiyo ni kwa sababu majini waliamini Qurani.
tusomapo katika Qurani SuratulAl- Ahqaf, (Kichuguu Cha mchanga) 46:29
“ Na wakumbushe tulivyokuletea kundi la majini kuja kwako kusikiliza Qurani. Basi walipohudhulia walisema (kuambiana: ‘Nyamazeni (msikilizeni maneno ya Mwenyesi Mungu’ na ilipokwiza’ na ilipokwiza somwa walirudi kwa jamaa zao wakiwaonya.”
Na ndani ya Qurani kuna sura nzima inayoitwa surah ya majini (Mashetani) hiyo ni surah ya 72. katika Surah hiyo inasema 72:1-3, 14 “ Sema: imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikia Qurani likasema hakika tumesikia Qurani ya ajabu inaongoza katika uongofu. Kwa hivyo tumeiamini wala hatutamshirikisha yeyeote tena na Mola wetu na kwa hakika utukufu wa Mola wetu umetukuka kabisa. Hakujifanyia mke wala mwana ……
Nasi wamo miongoni mwetu waliosilimu Na wamo waliokengeuka. Waliosilimu hao ndiyo waliotafuta uwongofu.
Kwa hiyo aya hizi zinaonyesha kuwa Qurani ilipokuja ndipo majini waliposilimu. Kumbuka kuwa Qurani imeanza mwaka 610 B.K kipindi ambacho Biblia tayari ili kuwepo kwa karibu karne 6.
Akifafanua asili ya majini mwanazuoni mkubwa wa kiislamu aitwaye Abdallah Saleh Farsy aliye kuwa Kadhi Mkuu Zanzibar, kasha akawa Kadhi Mkuu Kenya katika kitabu alichoandika kiitwacho “Maisha Ya Nabii Muhammad”.Ule Uk 31 anasema
“ Katika safari yake ya kurejea Taif ndipo walipomjia majini wakasilimu Kama inavyoonyesha haya katika suratul Jinn. Majini ni viumbe vyebesi vinavyokaa angani havina viwiliwili kwa hiyo haviwezi kuonekana na wanadamu ila vinapojibadili kwa umbo lenye kiwiliwili. Na vina uwezo huo wa kujibadili kwa sura ya kuweza kuonekana. WAO NA MASHETANI WANA ASILI MOJA.
Kwa hiyo asili ya majini ni shetani.
Suala linalohusu malaika linawasumbua sana Waislamu hata hawana uhakika wake.
Tumesoma ndani ya Biblia kuwa kuna kundi la malaika waliokosa ambao ndiyo wanaitwa majini lakini tusomapo Qurani inatoa maelezo tofauti.
Quran Suratul- al- sajdah, (kusujudu) 32:13
“ Na tungelitaka tungempa kila mtu uwongofu wake (kwa lazima kama tulivyowapa Malaika lakini binadamu amepewa huria ya kufanya alitakalo- liliyo jema na baya).
Katika ulimwengu wa kiislamu malaika wote ni wema na wanamwabudu Mungu.
Hapa ndipo penye tatizo linapoanzia. Qurani ilipokuja baadaye inasema Malaika wote wema wakati Biblia kitabu kilichotangulia Qurani kinasema kuna malaika walioasi Na wakafukuzwa katika utukufu WA Mungu.
Katika Qurani Suratul al kahf (Pango) 18:50
“ Na kumbukeni tulipowaambia Malaika, Msujudieni Adamu. Basi wakasujudia isipokuwa Ibilisi yeye alikuwa miongoni mwa majini na akavunja amri ya Mola wake ……”
Katika aya hiyo tunaona Ibilisi akilaumiwa kwa kutomsujudia Adamu ingawa amri ya kusujudu walipewa Malaika kumbe kwa mujibu wa Qurani Ibilisi alikuwa miongoni mwao hao Malaika yaani yeye akiwa Malaika.
Kwa sababu Qurani haina habari kuhusu Malaika waliosi yaani majini ndiyo maana wanapata tabu kuhusu jambo hilo. Na ndiyo maana pamoja na kujua kuwa hao majini ni mashetani, Mwislamu amehiari kushirikiana nayo kwa kuswali nayo msikitini. Na hata Mwislamu huyo anapomaliza kusali husalimia kulia na kushoto akiwasalimia watu, malaika na majini (mashetani) waliokuja kushiriki naye katika ibada yake, soma katika
(Irshadul Muslimiin, sheikh Said Musa, Uk 38)
Katika Tafsiri ya Qurani ya Imam Jalalaini Uk 6:151 anasema kuhusu majini
“ Hao ni watoto wa Ibilisi”
Hii ndiyo sababu hata Wanawake wa Kiislamu wakiwa katika kipindi cha hedhi hawaendi Msikitini kwa sababu mle ndani kuna majini na chakula cha majini ni damu.
Tafakari kwa hiyo sifa ya hayo majini au mashetani kwa ujumla ni kuwa “ hujaribu kwa bidii sana kuwa karibu na waumini (Waislamu) wale wanaosali, kufunga na kusoma Qurani” (Asili ya majini, DK. Ahmed H. Sakr Uk 28) Ndiyo maana baadhi ya Waislamu wao binafsi wasingependa kuwa waislamu lakini majini huwashurutisha kwenda kuswali.
Kwa sababu wao Waislamu hawajui kubambanua kati ya majini ambayo ni roho chafu na wale Malaika watakatifu wa Mungu Yehova, ndiyo maana hata akiwa katika sala yake hana uhakika kwa sababu huyo jinni (shetani) amemteka na amemfanya atakavyo na yeye ni mtumwa wa huyo jinni (shetani)
Katika kitabu kiitwacho Mkweli Mwaminifu cha Sheikh Said Moosa Mohammad Al- Kindy wa Muscut Oman, juzuu 1-2 Uk 42 hadith Na 74.
“ Anamwijia mmoja wenu shetani (jinni) katika sala basi anapuliza katika matako yake, basi (Yule mtu) inamuijia fikra ya kuwa umemtoka upepo (kafusa) naye haukumtoka, basi akiona namna hiyo asiondoke (kwenye sala) mpaka asikie sauti (ya kutoka upepo) au anuse harufu (ya huo upepo uliyomtoka, ndio aondoke).
Huyo shetani, au jinni anakuwa karibu sana na huyo Muumini wa kiislamu hamchezei tu Mwislamu katika matako yake kama tulivyosoma hapo juu bali pia anapofanya tendo la ndoa.
Katika kitabu kiitwacho Asili Ya majini cha Dr Ahmad h. Sakir Uk 116anasema
“ Hadithi ya Mtume inathibitisha jambo hili kuwa majini (mashetani) na watu wanaweza kuoana aliposema kwamba iwapo mtu ataingia katika uhusiano wa kindoa na mkewe anatakiwa ataje jina la Mwenyezi Mungu ajilinde kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya shetani aliyefukuzwa mbali na rehema. Vinginevyo shetani hujivingirisha katika dhakari (sehemu ya siri za mwanaume) ya mtu huyo na atashirikiana naye katika tendo hilo. Tafakari yetu kuwa huyo jinni anayeshiriki naye tendo la ndoa pamoja kwa mkewe ametumwa na huyo huyo Mungu wao. Hiyo ni kesi ya ngedere kumpelekea nyani! Utashindwa tu!
v Huhakikisha haweki wazi utambulisho wake vinginevyo watu wanaweza kumkwepa au hata kumkimbia. Jina lake linawatisha watu wengi. Hivyo ni vyema asijitambulishe kama ni shetani, jinni.
v Huwapotosha watu kutoka kwa Mwenyezi Mungu ili waende naye jehanamu, badala ya kwenda peke yake. (Kumbuka hukumu ya Yesu kwa Ibilisi na Malaika zake Math 25:41)
v Huwakatisha watu tamaa kwa sababu kwa sababu hana la kuwapa ila matumaini ya uongo ( mf Q. 52:20)
v Huhakikisha kwamba watu wanamheshimu. Kumfuata shetani maana yake ni kuwa mtu amejisalimisha (kumbuka Waislamu wanaposalimia majini kulia na kushoto katika sala {Irshadul Muslimin Uk 38}).
v Huhakikisha kwamba hadhihirishi jina lake kama shetani lakini kama rafiki aliyejificha anayewatakiwa mema.
v Huanziza vurugu vinginevyo maisha yake huwa ya taabu. Huwa anafurahia kuona watu wakipigana wao kwa wao.
Katika kipengele hiki tunaposoma katika Qurani, suratul- Al- maidah, (Meza) 5:14
“ Na kwa wale waliosema sisi ni Wakristo tulichukua ahadi kwao, lakini wakaacha sehemu (kubwa) ya yale waliyokumbushwa kwa hivyo tukaweka baina yao (wenyewe kwa wenyewe) uadui na bughudha mpaka siku ya kiyama na Mwenyezi Mungu atawaambia waliyokuwa wakiyafanya”
Allah S.W ndiye anayewaletea uadui na bughudha Wakristo. Yeye atakuwa nani?
Tafakari.
· Hufundisha uchawi watu wanapaswa watoe kiapo cha utii kwake kabla ya kufundisha uchawi wa aina yeyote. Elimu ya uchawi ya kuwadhuru watu wengine hasa waume na wake.
Katika sehemu hii tumwangalie huyo shetani au jinni anayeruhusu na kufundisha uchawi.
Katika Suratul Al- Baqarah, (Ng’ombe jike), 2:102
“ Wakafuata yale waliyoyafuata Mashetani wakadai yalikuwa katika ufalme wa nabii Suleiman na Suleiman hakukufuru bali Mashetani ndio waliokufuru, wakiwafundisha watu uchawi waliokuwa wakiujua wenyewe tangu zamani. Na uchawi ulioteremshwa kwa malaika wawili Haruta na Maruta katika mji wa Babeli wala malaika hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie hakika sisi ni mtihani wa kutazamwa kutii kwenu basi usikufuru, wakajifunza kwao ambayo waliweza kumfarakisha mtu na mkewe na mengineyo wala hawakuwa wenye kumdhuru yeyote kwa hayo ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu ……”
Katika aya hiyo inaeleza kuwa uchawi ni kazi ya Allah na ndiye anaye idhinisha. Yeye atakuwa nani? Na pia kuna waganga wa kienyeji wa kiislamu ambao hutumia Qurani katika uganga wao. Hiyo Qurani na majini na uchawi ulioletwa na Allah S.W vina uhusiano gani? Tafakari
“ Juhudi kubwa anayoifanya shetani (jinni) ni kuleta mfarakano baina ya waume na wake. Kwa kufanya hivyo huhakikisha kuwa wanachukiana wao kwa wao. Kwa ajili hiyo huishia, katika talaka. Kwa hiyo matatizo yanajengwa kisawasawa na mzazi mmoja. Watakosa uimara katika utu wao, shetani (jinni) anapata urahisi kuingia ndani ya mioyo na akili za watoto. Atawaongoza kuelekea mahali pasipofaa na hapo anawafanya wawe wahalifu katika jamii.” (Asili ya Majini, Sheikh Dr. Ahmad H. Sakr Uk 39)
Kwa mujibu wa Qurani na vitabu vya kiislamu huyo anayeamuru talaka ni Allah S.W Mungu wanayemwabudu Waislamu.
Katika Suratul, Ahzab (Makundi), 33:49
“ Enyi mlioamini mtakapowaona wanawake wenye kuamini, kasha mkawapa talaka kabla ya kuwagusa hamna eda juu yao mtakayohesabu. Wapeni cha kuwauliza na muachane muachano mzuri.”
Katika Suratul Baqarah, (Ng’ombe) 2:230.
“ Na kama amempa talaka ya tatu basi mwanamke huyo si halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwingine, na mwanamme huyo mwingine, akimwacha basi hapo hapana dhambi huyo kurejeana wakiona watasimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu.”
Kama shetani (Jinni) huleta faraka ili talaka zitokee, basi Allah S.W yeye ameruhusu talaka kwa wafuasi wake bila kujali athari za watoto zitakazotokea. Tafakari yeye ni nani?
Kumwabudu shetani (shetani)
Katika Suratul Sabaa, 34:40-41
“ Na kumbuka siku atakapowakusanya wote, kasha atawaambia Malaika “Je hawa walikuwa wakikuabuduni?” waseme umeepukana na kila upungufu! Wewe ndiwe kipenzi chetu si hao bali walikuwa wakiwaabudu MAJINI; wengi wao waliwaamini hao majini.”
“ Shetani anapoamuru watu wamfuate pia anawaauru wafanye madhambi na wakose maadili. Huwataka waseme uongo kuhusu Mwenyezi Mungu kutokamana na kutojua kwao. Wanaweza kusema kuwa sisi wanadamu tumeumbwa kwa mfano wa Mungu. Mungu alijifanyisha na kuwa umbile la kibinadamu. Mungu amezaa, na Mwanawe ni wa pekee. Zaidi ya hayo pia huyo Mwanaye si mtoto tu bali ni Mungu pia. Huyo Mwana ni Bwana Yesu. Asiyeamini hivyo ni kafiri au muasi hivyo ameangamia na atakwenda jehenamu” (Asili Ya Majini, Sheikh Dr. Ahmad H. Sakr Uk 54)
Hapa ndipo sura halisi ya huyu shetani yaani jinni inapojitokeza. Yesu alipokuwa duniani kabla ya Muhammad hajazaliwa, wala uislamu haujaanzishwa na Muhammad wala Qurani haijaandika na wale waarabu waandishi, Seyidna abubakar, Omar, Othuman, Ally na wenzao, majini yaani Mashetani yalipomwona Yesu yalimwita Mwana wa Mungu tuna nini nawe? Je, umekuja kututesa kabla ya muhula wetu? (Math 8:28-31) mwaka wa 610 B.K majini hayo hayo yakaanza kuwadanganya Waislamu kuwa Mwenyezi Mungu hana Mwana (Q.72:1-3). Na bila kuitafakari. Nao wao wanaamini tu kuwa Qurani ni maneno ya Mungu bila kupambanua huyo ni mungu yupi?
Katika Suratul An- Nisaa (Wanawake) 4:120
“ Shetani hawaahidi ila uwongo ……”
Hii ndiyo sababu Muhammad mtume wa Waislamu katika kitabu “ Wakeze mtume Wakubwa na Wanawe” kilichoandikwa na marehemu Sheikh Abdallah Saleh Farsy uk 12
Muhammad anasema,
“ Najikhofia nafsi yangu kuchezewa na Mashetani na kuniharibu akili yangu na kunuzuga ………”
Aliyasema maneno hayo baada ya kubanwa na kiumbe kule pangoni mwa Hirra alimokuwa. Baada ya hapo akaanza kujiita Mtume. Hoja yetu ni Mtume wa nani?
Katika kitabu cha Ibnu Ishaq 132-133
“Kama huyu shetani (jinni) ambaye amekupagaa wewe ni yule ambaye huwezi kumtoa, tutamtafuta mganga na tutatumia vyote tulivyonavyo kukutibu kwa kuwa mara kwa mara shetani (jinni) humpagaa mtu, lakini anaweza kuondolewa. Mtume alikuwa akisikiliza kwa makini.”
Kasha baadaye yeye Muhammad katika Sahih muslim Juzuu 4 hadithi na 2814 kasema;
“Wala hakuna yeyote katika ninyi isipokuwa amepewa nguvu zinazotokana na majini. Wakasema (maswahaba) hata wewe mtume wa Allah? Akasema hata mimi isipokuwa Allah hunirahisishia juu yake hunyenyekea wala hayaniamrishi ila yaliyo mazuri.”
Kwa hiyo majini ni ndugu za Waislamu Q. 46:29 ufafanuzi wake. Katika kitabu Asili Ya Majini Sheikh Dr. Ahmad Sakr Uk 80 anasema “ Imepokewa na Khalid Ibn Walid kuwa kuna wakati alipatwa na ukosefu wa usingizi basi Mtume (S.A.W) akamwambia.
“ Nikufundishe maneno ambayo ukiyasema utapata usingizi? Sema; Ewe Mola! Wewe ni Mola wa mbingu saba na kile kilichofunikwa nazo. Na wewe ni Mola wa ardhi na kilichomo humo. Nawe ni Mola wa Mashetani (Majinni) na maovu yao. Nakuomba uwe mlinzi dhidi ya viumbe vyako vyote..”
Hadithi hii inaonyesha jinsi Allah S.A.W alivyo na uhusiano wa karibu na Mashetani. Je, yeye ni nani? Pia katika Q: 21:82, 34:12, 38:37 zinaeleza Allah alivyomtiishia majini Suleiman wa kwenye Qurani na yeye Allah akiwa mlinzi wao hata kuwaadhibu wasiofanya kazi vizuri.
Katika Q. 19:83 “ Je, huoni ya kuwa tumewatuma Mashetani juu ya makafiri wanaowachochea kufanya mabaya?”
Katika Sahih Muslim Vol. IV Hadith Na. 2667, Sahih al- Bukhari Vol VII Na. 6243, Sunnan Abuu Daud VOL. II Na 2152
“Hakika Allah amemkadiria kila mtu kipimo chake cha zinaa, ambacho haikosi kutimia kwake”
Tumeona kuwa majini au Mashetani au Pepo Wachafu au Ibilisi walikuwa Malaika walioasi wakatupwa chini huku duniani, walitaka kurudi huko mbinguni lakini walishindwa.
Katika Q. Suratul al- Jinn (Majinni) 72:8-10
“ Nasi tulizigusa mbingu (tulikwenda mbinguni) tukaziona zimejaa walinzi wenye nguvu na nyota (zing’arazo) na hakika tulikuwa tukikaa humo katika baadhi ya makao ili kusikiliza lakini anayetaka kusikiliza sasa atakuta kimondo (kijinga cha moto) kinamvizia. Nasi hatujui kama wanatakiwa shari wale wanaokaa katika ardhi au Mola wao anawatakia kheri.)
Majini yanajieleza kuwa hayajui Mungu anawatakia mazuri au mabaya wale wakaao duniani.
Yer. 29:11 “ Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi asema BWANA ni mawazo ya amani wala si ya mabaya kuwapa nyinyi tumaini siku zenu za mwisho.”
Majini (Mashetani) yanajua tu kuwa Yesu atayahukumu na hayajui lolote kuhusu mpango wa Mungu kumwokoa mwanadamu toka kwa shetani (majini)
Moja kati ya majina ya sifa ya Allah ni AL-MUQADIM yaani WA ZAMANI(majina 99 ya Allah)
Biblia kupitia Mtume wa Mungu Paulo, katika 2 Kor 11:14 inasema
“ Wala si ajabu shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa Malaika wa nuru …..”
Pia katika 1 Tim 4:1 “ Basi roho anena wazi wazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine (Waislamu) watajitenga na imani wakisikiliza roho zitanganyazo na mafundisho ya Mashetani (majini)
Tafakari Kuu: Allah katuma Mashetani (majini), wako katika dini yake ya Uislamu, Yeye mwenyewe pamoja na majini yake na wafuasi wake walikuwa wakimfanyia Suleiman wa ndani ya Qurani kazi yeye Allah S.W akiwa msimamizi (Foreman) wao.
Mwisho wao wote pamoja na Allah Mwenyewe ni kama alivyokiri katika Sahih Bukhari VOL VI Hadithi Na 370 ni katika JEHANAMU YA MOTO.
Yeye Allah atakuwa nani??? Tafakari wewe ndugu yangu Mkristo, shika sana ulichonacho asije mtu akakunyang’anya!!!!
Na wewe rafiki yangu Mwislamu okoa roho yako. Nenda kanisani ukajisalimishe upate nusura ya Mwenyezi Mungu!!
Tuandikie:
Anwani yetu ni
P.o Box 84430-0800
MOMBASA
AU
P. O. Box 24430-00502,
Nairobi, Kenya.
Au
Huduma Ya Uinjilisti Ya Biblia Ni Jibu
S.L.P 45290 Dar es Salaam, Tanzania
Simu:
Email: d_mwankemwa@yahoo.com,
No comments:
Post a Comment